mwanakijiji
11-28-2008, 10:22 AM
Mojawapo ya vitu vya kushangaza na ambavyo vimezua maswali kwa watu ni kitendo cha Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha kwenda kutembelea gereza la Keko ambako waliowahi kuwa mawaziri wanashikiliwa rumande.
Hicho peke yake kisingeshangaza isipokuwa mazingira ya safari yake hii yanatufanya tuamini kuwa kama alifanya kwa nia njema basi ameonesha kushindwa kupima maamuzi yake na pia kutufanya tuhoji uwezo wake wa kuwa kiongozi huru hasa saa na wakati huu ambapo Taifa letu limeanza kupambana na ufisadi wa ngazi zajuu.
Mjadala uliopo mbele yetu siyo kwanini yeye Waziri ametembelea Gereza kwani itakuwa ni kituko kama Waziri hatembelei magereza kujiona hali iliyopo au kwa sababu yoyote iliyomo ndani ya kazi yake.
Hata hivyo kitendo cha Waziri Masha kwenda Keko siku moja baada ya marafiki zake wa karibu wa familia kwenda rumande na hasa kwenda kwa gari lake binafsi bila kutoa angalau taarifa kwa vyombo vya habari kuwa atakuwa na ziara ya namna hiyo kinazua maswali ambayo majibu yake hadi sasa hayajatosheleza.
Kama kweli alikuwa katika shughuli za kawaida, iweje iwe katika gereza la Keko na siku moja baada ya kina Basil Mramba na Yona kutupwa huko? Yawezekana mtu akasema kuwa alienda kuangalia hali zao zikoje n.k lakini tutahoji mbona kuna wafungwa wengi wanaoshikiliwa kwenye magereza yetu kwanini hawa kina Mramba na Yona wapate upendeleo huu maalum?
Yawezekana mwingine akasema kuwa alienda pale kuwapelekea ujumbe wa aina fulani au kuchukua ujumbe wa aina fulani. Hilo nalo litatufanya tuhoji kiini cha ujumbe huo. Ni ujumbe gani huo mzito ambao ulishindwa kupitishwa kwa Kamishna wa Magereza au Mkuu wa Gereza kumuhitaji Waziri kwenda kusikiliza? Kama ni suala la rufaa au hali mbaya, si ndio maana watuhumiwa wana mawakili wao na wangeweza kwenda mahakamani kutoa malalamiko yao kama walivyofanya?
Kwa ufupi ni kuwa Waziri Masha ameonesha ukosefu mkubwa wa hekima na upendeleo wa wazi na hivyo kutishia mchakato mzima wa utafutwaji na upatikanaji wa haki katika suala la kina Mramba. Bw. Masha aombe radhi na kuwahakikishia wananchi kuwa jambo kama hilo halitatokea tena kwani siyo tu linahoji uwezo wake wa kuongoza lakini zaidi linatufanya tujiulize kama kweli serikali yetu iko impartial na kumuacha Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kufanya kazi yake.
Ni matumaini yetu kuwa kitendo hicho alichokifanya hatokifanya tena katika mazingira kama haya na kwa namna ya kificho kama hivi. Vinginevyo kama kuna mchezo wameamua kucheza basi wajue kuwa wananchi wako macho wakati wote.
M.M.