mwanakijiji
11-29-2008, 09:53 AM
Kuna tetesi ambazo tunazifanyia kazi kuwa Mbunge wa Igunga Bw. Rostam Aziz amekutana/atakutana na Mfanyabiashara maarufu nchini Bw. Yusuph Manji ambaye amekimbizwa Nairobi kwa matibabu.
Ingawa inajulikana Bw. Aziz alikuwa mjini humu kwa shughuli zake Bw. Manji yeye alikimbizwa huko kutokana na kile kinachodaiwa "kuoverdose".
Wafanyabiashara hao wawili wanadaiwa kuhusiana katika sakata la EPA ambapo kuna habari kuwa Bw. Manji alitumiwa kurudisha kiasi cha fedha ambacho kinadaiwa kuwa kilichukulikwa na Bw. Aziz kupitia kampuni ya Kagoda.
Wakati huo huo siku ya Alhamisi vyanzo vyetu vya kuaminika vimedokeza kufanyika kwa kikao cha mkakati kati ya vyombo mbalimbali vya usimamizi wa sheria katika kuendelea na mapambano dhidi ya ufisadi nchini hususan hatua zinazofuata.
Hata hivyo kwa maoni yetu kuna mapungufu makubwa sana ya hatua hizi za kisheria jambo ambalo tunatarajia kulichambua katika matoleo yetu ya Cheche na makala mbalimbali za magazeti.
Kujipatia nakala yako tuandikie mhariri@klhnews.com
omondi
11-29-2008, 05:19 PM
Kama serikali imethubutu kuwakamata former cabinet members wawili huyu Aziz ni nani hadi anaogopwa na serikali? Hivi ile Preventive Detention act ilikwishafutwa?
Mpita Njia
11-29-2008, 07:35 PM
Kama serikali imethubutu kuwakamata former cabinet members wawili huyu Aziz ni nani hadi anaogopwa na serikali? Hivi ile Preventive Detention act ilikwishafutwa?
Wenyewe wanamuita King Maker
duru langu
11-29-2008, 08:38 PM
Ukiona hao wenyewe wameachwa kulihali mawaziri wawili wa zamani
wapo lupango (mmoja kakosa harusi ya binti yake) ujue hiyo mtu mbili
Rostam na Manji wamewashika pabaya wanaotakiwa kutoa amri wawekwe
ndani.
mwanakijiji
12-01-2008, 04:48 PM
Kutoka kwa Mpelelezi wetu:
.. Kagoda ni ya Rostam Aziz, na vyema umesema inashangaza kwa Yusuf Manji
kuhusishwa/Kujihusisha na Kagoda. Nitakuambia hapo ngoma ikoje. Ni
hivi....
Kagoda ni kweli mtupu ni ya Rostam, ila waliosajiliwa na msajiri na kwenye
document halali za usajiri wamiliki hisa Kagoda in wakina JOHN KYOMUHENDO
& FRANCIS WILLIAM lakini nyuma yao yuko
Rostam. Upelelezi uligundua kuwa Pesa kwenye Benki ya Kagoda CRDB pesa
zilikwenda kwa Caspianna pia kila pesa zilipokuja chukuliwa, Rostam alikuwa mstari wa mbele.
Baadhi ya Pesa za kagoda pia zilikuwa zimekuwa transferred kwenye
makampuni mbalimbali yaliyo karibu na Rostam kama kampuni kama Associated
Breweries(Serengeti Breweries). Mwenyekiti wao Mr. Bomani alisema kuwa wao
waliomba mkopo tu kutoka kwa Rostam lakini hawakujua pesa hizo source yake
ni ipi, na hivyo kurudisha serikarini US$ 2M mara moja ili kuepuka balaa
zaidi. Kampuni hizo nyingi zilizokutwa zimepokea pesa toka Kagoda lazima
zichukuliwe hatua pia. Sasa wakati upelelezi unaendelea, na kabla
hatujafikia ratiba ya kumwita Rostam kumuhoji mara sisi wapelelezi
tukashangaa Yusuf Manji anajitokeza bila kuitwa na akidai yeye ndiye
mmiliki wa Kagoda na sio Rostam, sis tukashangaa sanaaa, lakini kushangaa
kwetu kukakatizwa na wakuu wetu kuwa tuendelee kumuhoji tu hivyo hivyo.
Tukajua hili limesukwa hata wakuu wetu, mwanasheria mkuu, DPP, DCI, IGP na
TISS walikuwa lao moja. Yusuf Manji hakaja na stori hii. Kagoda ilikuwa
kampuni sio yake bali ya babayake mzee Manji ambaye ni Marehemu kwa sasa.
Eti yeye Yusuf Manji angependa kusafisha jina la familia ya Manji kwa
kujitolea kuzilipa pesa hizo Bilion 40 alizochukua Manji Marehemu
serikalini.
Eti nia yake bora yaishe, na pia alieleza kuwa Baba yake
Marehemu aliingizwa katika mambo hayo na marehemu Balali na yeye
alimuamini kwa kwamba Balali alimwambia pesa hizo zilikuwa za kusaidia
uchaguzi CCM. Yusuf Manji alikuja na cheki ya malipo ya hawali kama TZS 20
billion, na cheki za malipo ya mbeleni. Mchezo mzima ni kuwa kama kuna mtu
kajotokeza, ka-voluntee information, na kakubali kosa kwa niaba ya
marehemu baba yake, na kashaanza kulipa deni polepole, sasa Rostam
mnamtafuta wa nini?.
Ni vyema kujua Rostam alikuwa Treasurer(???) wa CCMkipindi chote hicho za wizi wa EPA. Hivyo yeye kuhusishwa na EPA mojakwa moja CCM inahusika na raisi anahusika. Hivyo mchezo mzima unachezwa kwa kigezo cha Mzee Manji marehemu ndiye alikuwa mmiliki wa Kagoda wakiti siokweli.
Mzee Manji marehemu anataka kubebeshwa mzigo sio wake, kufuru tupu,
kuiokoa CCM. Wabunge wengi wanafahamu Kagoda ni ya Rostam. Yusuf Manji
kajitokeza kununua kesi hiyo tu kwani yeye ni mtoto wa mjini na hajali
sana mambo ya kashfa.
CCM itamlipa kwa fadhila zake hizo huko mbeleni. Atapewa tenda za mahindi, mchele na miundombinu mabalimbali kwa inflated prices. Pia CCM imeona kuwa kumtoa kafara Yusuf Manji kwa Kagoda, itatoa faraja kwa wananchi kwa wananchi wanalilia damu ya kigogo. Yusuf Manji ni kigogo kama alivyo Rostam lakini Rostam si rahisi kumtoa kafara, ni nguzo
ya CCM kifedha na fadhila, pia anasiri nyingi sana.
Ni bora kumkumbatia, CCM inafikiri huko baadae mambo yakiwa shwari watamshughulikia Rostam kimya kimya, lakini hawajui na ni ninja fulani. Yusif Manji anajua pamoja
na kununua kesi ya Kagoda hawezi sota jela kwani kesi ameinunua kwa niaba
ya Marahemu baba yake. CCM inajua uchaguzi mwaka kesho tu 2010, na mpaka
sasa ufisadi imetawala habari, na vyanzo vya pesa vimewekewa ngumu, hali
ya pesa CCM ni mbaya sana, Benki kuu kwa sasa wakaguzi wakali wa Ernest &
Young bado wako huku hakuendeki, itachobaki ni mikataba tu, nakini pia
mikataba sasa ni moto, sasa CCM inawahitaji wajanja wa kuifundisha
mikakaki ya kutengeneza pesa, labda dumping ya mafuta kiasi, petrol
kuingizwa Tanga port bila ushuru na tenda za strategic grain reserves ziwe
inflated price.
WANANCHI TULIE NA ROSTAM TU, YUSUF MANJI PIA AADHIBIWE KUTAKA KUHARIBU USHAHIDI, HILO NI KOSA LA JINAI PIA. LAKINI TUTAMBUE KUWA HILO LIMESUKWA NA DPP, DCI, AG, TISS. PESA ALIZOLIPA YUSUF MANJI SERIKALI IZICHUKUE NA PIA DENI LIWEPO PALEPALE KUTOKA KWA ROSTAM. SERIKALI IKAMATE MARAMOJA ILE KAMPUNI YA CASPIAN
DPP, DCI, AG, TISS MUWE WAZALENDO NA WAADILIFU NCHI YETU IENDELEE.
My more
12-01-2008, 06:55 PM
Sijui niseme shetani, ulafi, au laana? kama watu wamefikia kununua kesi kubwa hivi ya kuangamiza nchi.....! Even Adolf Hitler would never behaved that way.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.