PDA

View Full Version : JK apangua makatibu wakuu



Mpita Njia
11-29-2008, 03:50 PM
http://www.mwanakijiji.com/images/resized//images/stories/habari/people/graymgonja_phixr_265_198.jpg

Rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika safu ya makatibu wakuu katika mabadiliko ambayo ymemgusa pia aliyekuwa \katibu mkuu wozara ya fedha, Gray Mgonja(pichani). Mgonja ameachwa kwa kile kinachoelezwa kuwa amekwenda likizo ya kustaafu.
Habari kamili inatengenezwa hivi sasa na itawekwa kwenye ukurasa wa mbele baada ya muda

Ach-F
11-29-2008, 07:27 PM
Huyo Mgonja ni muhujumu wa uchumi anatakiwa kukiona cha mtema kuni.

Mpita Njia
11-29-2008, 07:54 PM
Nadhani wanamuandaa kwa ajili ya kukiona cha mtema kuni

duru langu
11-30-2008, 01:37 AM
Sasa hii imekaaje? Mbona yule jamaa anayeitwa
Rutabanziba alikuwemo kwenye ile orodha ya Dr. Slaa
bado yumo? Au mwendo wenyewe ni "Mramba style" unaachwa
ujiamini kwamba huguswi kisha unashtukizwa kupelekwa Kisutu
huku umevaa kandambili.

Mpita Njia
12-01-2008, 01:14 PM
Duru Langu, naona wateuzi wanakosa watu wa kuwateua kwa sababu wamezoea kuangalia ndani ya box. Nina uhakika kama mteuzi akiamua kuangalia nje ya box alilonalo, atapata wengi tu ambao hawana tuhuma kama alionao kwenye box lake

My more
12-01-2008, 06:31 PM
Nadhani wanamuandaa kwa ajili ya kukiona cha mtema kuni

Kisutu lini huyu??

mwanakijiji
12-01-2008, 07:11 PM
Lakini Mgonja amekuwa hapo muda huu wote hivi kweli hatuna uwezo wa k uwasimamia watu hawa? Hadi haya yote yanatokea Benki Kuu halafu leo tunamuacha mtu astaafu kwa heshima?