PDA

View Full Version : Mkapa ashughulikiwaje?

mwanakijiji
11-30-2008, 01:10 AM
Kama ungeombwa kutoa ushauri wa jinsi ya kumshughulikia aliyekuwa Rais wa JMT Bw. Benjamin Mkapa katika kupambana na vitendo vya ufisadi vilivyomhusisha yeye au vile ambavyo vinaonesha kuwa alikiuka maadili ya uongozi.

My more
11-30-2008, 01:19 AM

Hapa kazi ninayo mwaka huu. Maana huyu jamaa siku hizi mambo yanavyomwendea .....karibu anakuwa jirani yetu pale kijiweni. Hivi lipi rahisi kumchimbia kaburi marehemu mtarajiwa au kumpelekea sanda huku bado mahututi?. Ngoja nikune kichwa kwanza

duru langu
11-30-2008, 01:57 AM
Naamini anahitaji kutoa maelezo kwa vitu ambavyo amefanya lakini
matunda yake hayakwenda kwa wananchi bali walikula matunda
hayo ni yeye mwenyewe au ndugu na jamaa zake tu.

My more
11-30-2008, 04:48 PM
Naamini anahitaji kutoa maelezo kwa vitu ambavyo amefanya lakini
matunda yake hayakwenda kwa wananchi bali walikula matunda
hayo ni yeye mwenyewe au ndugu na jamaa zake tu.

Kwa hilo sipingi, shida inakuwa pale inapotakiwa kumfunika nguo baba/ mama mkwe aliyejisahau akakaa vibaya hadharani, inakuwa ngumu ndugu yangu. sijui unanielewa?

duru langu
12-01-2008, 02:01 AM
Si unamfunika mkweo huku ukiwa umefumba macho.
Hakuna ugumu my more.
Mwezi February 2006 kama sikosei JK alisema umefika wakati wa
kufanya maamuzi magumu lakini naona akaahirisha sasa naamini
ni wakati muafaka wa kufanya hayo maamuzi magumu.

Ukitaka kuuwa nyani usimtazame usoni, wahenga walisema.

mwanakijiji
12-01-2008, 06:56 PM
Lakini kumchukulia hatua Rais aliyetangulia kunafungulia mlango wa wewe mwenyewe kufunguliwa mashttaka baadaye..

My more
12-01-2008, 07:00 PM
Lakini kumchukulia hatua Rais aliyetangulia kunafungulia mlango wa wewe mwenyewe kufunguliwa mashttaka baadaye..

Kama ni mtu safi kuna haja gani ya kuwa na woga huo? ... Hapo ndo palipo na hekima!!

Lusajo L.M.
12-02-2008, 12:50 PM
Lakini kumchukulia hatua Rais aliyetangulia kunafungulia mlango wa wewe mwenyewe kufunguliwa mashttaka baadaye..

Nadhani kwanza kinachohitajika ni marekebisho ya katiba ili kutoa hii kinga ambayo marais wanaipata akati wakiwa madarakani na baada ya kuachia ngazi. Hii itapelekea hawa ndugu zetu kufahamu ya kwamba kabla ya kitu chochote na wao ni Watanzania wenye haki sawa kama yule Mtanzania anayeishi Makandana...

Husiana na kumshughulikia BWM, kwa kweli ingekuwa ni hatua ambayo ingeashiria mapinduzi ya kweli maana kama unaishia kukata matawi na shina ukaliacha sidhani kama utakuwa ni ufumbuzi wa tatizo linalokukabili. Sema kwa mtazamo wangu nahisi ya kwamba kuna kitu ambacho kinawafanya wahusika washindwe kushtakiana kwa kuwa kwa namna moja ama nyengine hili suala linawahusu watu wote ambao wapo katika utawala, uwe uliopita ama wa sasa...

Sasa pale Mzee wetu atapowekwa Kizimbani jambo ambalo waliobaki watakuwa wanajiuliza itakuwa ni nini kinafuata. Nina hakika ya kwamba BWM alikmtengenezea njia JK aingie ikulu na hii ilifanyika 'By any Means Necessarry!' Sasa je katika kushtakiana na hayo yakifunuliwa tutafika wapi?

Nadhani ni muda wa Siasa safi na Uongozi bora kushika hatamu.

mwanakijiji
12-02-2008, 05:04 PM
Kinga ya Rais inasema kuhusu mambo aliyoyafanya "Kama Rais" lakini haisemi moja kwa moja kuwa ana kinga ya mambo aliyoyafanya katika uwezo wake kama mtu binafsi. Nadhani kubwa zaidi ambalo linaweza kubishaniwa ni kuwa wakati Rais akiwa madarakani kuna wakati ambapo hawi "Rais"? Je Urais ni shughuli za ofisini tu na akitoka basi yeye siyo Rais?

magoma
12-02-2008, 07:22 PM

Watanzania nadhani si wavivu wa kufkiri kiasi hicho, mi nadhani hawa wanaojiita wana sheria pale UDSM/mzumbe/tumain/sauti WAFUNUE misaafu yao watoe nyanga za kumshitaki huyu jamaa ingekuwa mi wanataka scientific input za kumshitaki ningewapa kama ingekuwa ni swala la Kisayansi lakini ni swala la usanii/linguistic mi nadhani huyu jamaa ni kufanya kila namna ya kutafuta njia za kumpeleka mbele ya sheria kama wakishindwa sisi watalaamu tutaingia MAABARA/WORKSHOP kutafuta njia mbadala ya kumuweka BWM mbele ya pilato.
natoa hoja