mwanakijiji
11-06-2008, 04:02 PM
Dayosisi ya Pare bado kwawaka moto
na Charles Ndagulla, Mwanga (Tanzania Daima)
HALI ya mambo bado si shwari ndani ya Dayosisi ya Pare ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), baada ya wachungaji 16 waliotoa tamko la kuunga mkono kuzaliwa wa Dayosisi mpya ya Mwanga kukataa kukana tamko lao.
Tukio hilo lilitokea juzi katika kikao baina ya wachungaji hao na Askofu Stephano Msangi wa Dayosisi ya Pare kilichofanyika kwenye shule ya watoto viziwi wilayani hapa.
Katika kikao hicho ambacho hata waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia huku ulinzi wa polisi ukiwa mkali,wachungaji hao walikataa agizo la Askofu Msangi la kuwataka kukana tamko lao la Oktoba 20 mwaka huu.
Tamko hilo lililotumwa kwa Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa, maaskofu wote wa KKKT, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, linamtaka Malasusa kushughulika haraka mgogoro katika Dayosisi ya Pare.
Wachungaji hao walisema mgogoro katika dayosisi hiyo upo na suluhu ya kuumaliza ni kuruhusu kuwepo kwa Dayosisi ya Mwanga ambako kumeshuhudiwa matukio mengi ya uvunjifu wa amani.
Habari ambazo zilipatikana kutoka ndani ya kikao hicho, zimedai wachungaji hao walisema hawako tayari kukana tamko hilo na kuongeza kuwa ukweli wa walichokisema unaendelea kubaki kama ulivyo.
Kwa mujibu wa mmoja wa wachugaji aliyekuwepo ndani ya kikao hicho bila kutaja jina lake, wachungaji hao wamekataa kushurutishwa na Askofu Msangi wakidai tamko hilo halikupelekwa kwake bali kwa mkuuu wake wa kanisa.
Mchugaji huyo alisema hakuna kilichofikiwa katika kikao hicho kutokana na mvutano mkali uliokuwepo baina ya Askofu Msangi na wachugaji hao ambao wote wanatoka eneo la mwanga.
Mbali na wachugaji hao, pia kikao hicho kilihudhuliwa na wachugaji wanane wa dayosisi hiyo kati yao watano wanatoka eneo la Same na watatu wanatoka eneo la Mwanga.
Hata hivyo, baadhi ya waumini waliozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho,wamelaani kitendo cha polisi kutumia nguvu katika mgogoro huo wakidai kuwa, wanaweza kuukuza na kuendelea kufukuta bila utatuzi.
Waumini hao wametoa rai kwa Malasusa kuutatua mgogoro huo haraka, ili kuepusha ghasia na machafuko ambayo yanaweza kutokea na kuondoa hali ya amani na utulivu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko, jana alitetea hatua ya Jeshi la Polisi kumpa ulinzi mkali Askofu Msangi na kuweka wazi kuwa kulikuwepo na taarifa za waumini wa eneo hilo la Mwanga kuleta vururgu.
Wiki iliyopita,waumini sita wa kanisa hilo kutoka eneo la Mwanga, walitoa tamko la kuunga mkono tamko la wachugaji hao la kutaka kanisa kuruhusu kuwepo na Dayosisi mpya ya Mwanga.
Waumini hao, Joseph Msuya, Amani Amini, Aminiel Mnzava, Paul Senzia na Nazahed Malisa, walimtaka Malasusa kutopuuza tamko la wachungaji hao na kuongeza kuwa mgogoro katika dayosisi hiyo upo.
Nilionalo:
Kama ilivyo migogoro mingine, kuna njia mbalimbali za kutatua. Njia ya kulazimisha ndiyo njia dhaifu zaidi kwani mara zote husababisha kisasi.