View Full Version : Gen. Mboma Fisadi?
mwanakijiji
12-01-2008, 09:32 AM
Katika pita pita zetu tukifuatilia kampuni ya Meremeta (utaona kwenye "Cheche" Jumanne jina la Mkuu huyo wa zamani wa JWTZ limeanza kujitokeza kwa namna isiyopendeza kabisa. Yeye na Vincent Mrisho (aliyekuwa Katibu Wizara hiyo na amestaafuta mwishoni mwa juma) wanatajwa kuhusika na vitendo vya kifisadi.
Endapo Bw. Mrisho atafikishwa mahakamani basi ndio mwanza wa kumfuatilia Gen. Mboma. Je yawezekana kuhusika kwa Mboma kwenye Meremeta na usiri uliopo ndiyo sababu ya wananchi kuambiwa kuwa masuala haya ya ufisadi ni sawa na "taifa kutekwa nyara"?
Mpita Njia
12-01-2008, 10:44 AM
Labda habari hizo ni sehemu ya clue ya kauli ya Mwema kuwa mafisadi walikuwa wameiteka nchi kama magaidi wafanyavyo
Mkongwe
12-01-2008, 11:38 AM
Labda habari hizo ni sehemu ya clue ya kauli ya Mwema kuwa mafisadi walikuwa wameiteka nchi kama magaidi wafanyavyo
You are absolutely right Mpita Njia! Ya kwangu macho
mwanakijiji
12-01-2008, 04:51 PM
Sasa kama ni mwelekeo huo, nani atakuwa na ujasiri wa kuwashughulikia watu hawa kama kina Mboma?
My more
12-01-2008, 06:28 PM
Sasa kama ni mwelekeo huo, nani atakuwa na ujasiri wa kuwashughulikia watu hawa kama kina Mboma?
Ujasiri utapatikana tu, kinachotakiwa ni kutengeneza mazingira mazuri yatakayowapa hao wanaotakiwa kuwashughurikia BIG POTATOES wapate huo ujasiri. Hili Linawezekana ???
Mfano wa kufikirika,(may be kitatokea) , Mtu anaweza kupata ujasili wa kujirusha au kutumbukia ziwani/ mtoni hata kama hajui kuogelea pindi anapojikuta kundi kubwa la simba limemzunguka linamshambulia. Kwa vyovyote atafikiria may be anaweza kuokoa maisha yake akijaribu kuogelea.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.