mwanakijiji
12-01-2008, 09:48 PM
(Mwananchi)
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imepanga Januari 25 mwakani kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijijini, uchaguzi ambao utafanyika kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Richard Nyaulawa aliyefariki hivi karibuni baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa tangazo hilo, sasa purukushani, mbwembwe na vikumbo vya wanasiasa vitaelekezwe jimboni humo ikiwa ni takriban miezi mitatu tangu kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime, ambako Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilifanikiwa kutetea kiti chake kilichoachwa wazi na Chacha Wangwe aliyefariki kwa ajali ya gari.
Mgombea wa Chadema, Charles Mwera alinyakua kiti hicho baada ya kushinda kwa tofauti ya kura nyingi dhidi ya mgombea wa CCM.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame aliliambia gazeti hili jana kuwa alipokea barua rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta kumjulisha kuwa nafasi ya ubunge wa Mbeya vijijini ipo wazi baada ya kifo cha Nyaulawa, aliyefariki Novemba 9 mwaka huu.
Jaji Makame alisema kwa mujibu wa sheria, uteuzi wa wagombea unatakiwa kufanyika kabla ya siku 50 tangu kifo cha mbunge kilipotokea, hivyo uteuzi wa wagombea wa kiti cha ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini utafanyika Desema 27 mwaka huu ikiwa ni siku ya 48 tangu Nyaulawa afariki dunia.
"Kuhusu uchaguzi Mbeya Vijijini, wiki iliyopita tulikutana na kupanga ratiba. Nafikiri sio siri. Desemba 27 mwaka huu utafanyika uteuzi wa wagombea," alisema Jaji Makame.
Alisema kampeni za uchaguzi huo zitaanza siku moja baada ya uteuzi wa wagombea hao, yaani Desemba 28 na kwamba sheria inataka uchaguzi ufanyike ndani ya siku 30 tangu kuanza kwa kampeni.
"Kwa mantiki hiyo uchaguzi wa jimbo la Mbeya Vijijini utafanyika Januari 25 mwaka 2009," alisema.
Akitoa maelezo ya jinsi tume hiyo ilivyojiandaa kwa uchaguzi huo, Makame alisema wanachosubiri sasa ni kuwezeshwa kifedha na serikali ili kuweza kutekeleza wajibu wao kwa Watanzania wa Mbeya Vijijini.
Mwananchi ilipotaka kujua hatua ambazo Nec imechukua ili kudhibiti yasitokee machafuko kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa Tarime, Jaji Makame alisema kuwa tume yake haina sababu ya kufikiri kwamba kutatokea vurugu katika uchaguzi huo.
Alisema Nec ilifanya semina hivi karibuni kwa lengo la kuvikumbusha vyama vya siasa na vingozi wao kuwa uchaguzi si ugomvi bali ni kuuza sera mbele ya wapiga kura na kuwashawishi wachague wagombea wao na kwamba ana imani wameelimika.
Hata hivyo, alisema kuwa vyombo vya usalama vipo na vitakuwa tayari wakati wowote kudhibiti uvunjaji wowote wa amani au machafuko yatakayotokea kama ilivyokuwa kwa uchaguzi wa Tarime.
My Take:
Hadi hivi sasa Upinzani bado hawajajionesha kuwa wana uwezo wa kushinda kwenye majimbo yaliyokuwa CCM katika uchaguzi mdogo. Je wataweza kushinda Mbeya Vijijini?