View Full Version : Nini kinachokukera Bongo?
mwanakijiji
12-02-2008, 05:11 PM
Kuna vitu ambavyo vinakera sana. Iwe Bongo au ugenini. Lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo kwa wanaoishi Bongo inawezekana kama wamevizoea hivi lakini ukweli vinawakera kweli na hawajui wafanye nini kukabiriana navyo. Kuna vitu ambavyo mtu mwingine anafanya vinakera, jamii inafanya vinakera au hata serikali inafanya vinakera. Na vingine sisi wenyewe tunavifanya na tunajua vinawakera watu wengine.
Fikiria ukipanda daladala (express, mzunguko) ni kitu gani cha kwanza kinaanza kukukera? Kugombania kuingia ndani ya daladala, kugombea kiti au kukaa na mtu mwenye kunuka kikwapa? Au kusimama halafu nyuma yako kuna mtu kumbe amepatwa na mfadhaiko na huna ujanja isipokuwa kuendelea kusimama tu?
Je unakereka kuona jinsi gani watu wanahatarisha maisha yao kwa kuvuka barabara mahali ambapo si pa kuvukia na miongoni mwao ni watoto wa shule?
Nini hasa kinakukera?
magoma
12-02-2008, 07:46 PM

vyote ulivyovitaja hapo juu vinakera tena sana tu ila umesahu na UFISADI BONGO nao unakera sana mwanakijiji, na mwishoe Rushwa nayo ina kera kwelikweli.
My more
12-03-2008, 04:24 PM
Wafanyabiashara wa vyakula hasa (take away) wasivyojali afya ya mteja. katika uandaaji wa vyakula vyao hata wakati wa kuhudumia. Uchafu mwingi na kuchanganya vyombo, kijiko kimoja kinatumika kupakulia a lot of things au sometimes mkono na kajikkaratasi kadogo sana.
mwanakijiji
12-03-2008, 04:43 PM

duh hapa umenikumbusha zile hoteli za barabarani wakati wa kusafiri (kama pale Mombo, au Igalula) yaani huwa tunakula kwa imani tu!
My more
12-03-2008, 06:21 PM
duh hapa umenikumbusha zile hoteli za barabarani wakati wa kusafiri (kama pale Mombo, au Igalula) yaani huwa tunakula kwa imani tu!
Ushawahi kupita Salanda (kwa gogo ie chuma kwa chuma?), Mbalamaziwa wilaya ya Mufindi?
Sitaki kukumbuka hizo enzi, bahati mbaya kulikuwa hakuna ujanja lazima ule kwa vile muda wala siku kufika uendako haujulikani
Watanzania kuridhika na maisha waliyonao na kuona kwamba CCM ndio chama pekee cha kuwaokoa wakati wenyewe wanavimbisha matumbo yao na familia zao kwa kutumia vibaya pesa za walipa kodi.
Matigari
04-03-2010, 11:35 PM
Nachukia foleni ya magari na ajali za barabarani ambazo zingeweza kuzuwiwa kama watu wangeendesha kistaarabu na kuwa defensive, ni kweli ajali haina kinga lakini kuna jali nyingi tu tunazojitakia. Pili ni kama hatujui kuwa kwa kukaa katika hizo foleni tunajinyima matunda ya uhuru kwa njia nyingi, kwanza tungeweza kutumia muda huo kufanya kazi nyingine ya kulipwa au burudani, pili tunapata kero kwa kukaa bila ya kufanya kitu kingingine.
Tabasamu
04-04-2010, 01:33 AM
Vumbi la bongo linanikera sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, miundo mbinu ipo ovyo sana. Hata kama unakauwezo ka kujenga nyumba kama mamtoni na kupata angalau mkweche wa kukusukuma, lakini vumbi bongo halikwepeki. Hii hali inanikera sana mieeeeeeeee argrhhhhhhhhhhhhhhhh
mwanakijiji
04-04-2010, 06:41 AM
Tabasamu umenichekesha kweli.. sasa vitu kama vumbi wataliondoaje bila kutengeneza feeder roads na kuziweka lami, kuhamasisha ujenzi wa nyumba ambao unatunza mazingira.. si unajua tena hatuthamini sana kutengeneza lawn.. maana mtu akijenga nyumba tu hapo nje uwanja ni vumbi tu safi.. badala ya manyasi..
Sofia
04-05-2010, 06:53 PM
kuna hii show ya kina Origino Komedi hivi majuzi wameonesha uchafu sokoni jinsi gani vyakula vimepangwa karibu na uchafu kabisa. Mimi kinanikera kweli.
Mtizamo
04-06-2010, 11:13 AM
kwenye daladala ni ishu ya kubanana na kukanyagana aisee
janny
04-08-2010, 04:03 PM
nakereheka sana na porojo za viongozi wetu mala nitaweka maji,nitajenga barabara lakini mwisho wa siku hawafanyi lolote ..sipendi hata kuwaona wakiwa wanatoa speech zao
Matigari
04-18-2010, 06:35 PM
kuna vitu vingine tunajiendekeza tu. Hivi kufagia uchafu kubahitaji nini? Tunahitaji serikali au Raisi wa nchi atuambie tufagie barabara au mahali tunapopanga mihogo na maembe kwa ajili ya biashara? Hiyo si common sense tu na good customer service?
Mimi nadhani tuna katabia ka uvivu wa aina fulani, hatutaki kujituma.
Speaking of customer service hilo nalo ni kero Tanzania, ukienda mahali pa biashara ya mtu anakufanya kama vile anakusaidia wewe ( doing you a favor) No! when I come to your stall to buy tomatoes, you are not doing me a favor, treat me well, because I have choice I can go to buy the same in another store.
Mimi nakereka na wakazi wa kariakoo ambao wanasubiri mvua zinyeshe ndio wafungulie maji machafu ya vyooni, tuanaofanya manunuzi kariakoo tunapita tunaogelea kwenye hayo maji machafu kwa kweli nakereka sana
Yooooote Tisa Kitu Kikubwa pamoja na hayo yote wanakijiji wenzangu mliyoorodhesha ...mimi KERO YANGU KUBWA....ni ahadi za Uongo za wanasiasa.... Eti Maisha bora kwa kila mtanzania.....HOW!......aaaagrrrrrrrrorororor gash!!! kwa kweli kwa mtazamo wangu haya yalikuwa ni maisha bora kwa kila fisadi....
nakereheka sana na porojo za viongozi wetu mala nitaweka maji,nitajenga barabara lakini mwisho wa siku hawafanyi lolote ..sipendi hata kuwaona wakiwa wanatoa speech zao
Yaaani hapo umesema I HATE THEM!!!!>>>> Unajua hawa wameshatuona waTz mambumbumbu ile mbaya.....eti mtu anakuambia Kila mt atakuwa na maisha bora halafu hasemi kivipi na sisi wenyewe hatuhoji tunabakia kushabikia tu yeeeeee ndiyoooo mpe kuraaaaaaa
Wacha
05-25-2010, 10:10 PM
Hakuna kiongozi aliyepo kwenye Chama Cha Majambazi mwenye nia ya kutatua matatizo tuliyonayo. JK ameamua kutatua matatizo ya Ridhiwani kuchukua mikoba mara atakapong'atuka na WTZ wanachekelea tu maana hakuna wa kumgusa. Walahi hii yote itamtokea puani muda tunao tusubiri.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.