PDA

View Full Version : Wakaguzi wa Minara 2 ya BoT hawastahili



mwanakijiji
12-02-2008, 05:32 PM
Kinyume na ilivyoandikwa mojawapo ya magazeti ya kila siku kuwa kampuni ya kimataifa ya wakaguzi wa hesabu wa katika masuala ya majengo M/S Mekon Arc Consult Limited ikishirikiana na kampuni mbili za kimataifa AQE Associates and Bureau for Industries Ltd wameshaanza kazi na wameanza kuuliza maswali kuhusu gharama za ujenzi wa Minara Pacha ya Benki Kuu.

Ukweli ni kwamba tenda ya ukaguzi huo ? Value for Money, ilikuwa ya ushindani wa kimataifa na makampuni makubwa ya ukaguzi huo wa kitaalamu kutoka nje ya nchi ? Africa Kusini, Uingereza, Marekani, Kenya, Uganda walilita tenda zao lakini wote walipigwa chini kwa kuogopa mambo yasiwe kama yale ya wakaguzi wa EPA.

Inasemekana kuwa viongozi wenye hekima serikalini waliopendekeza Ernest & Young wachaguliwe kufanya uchunguzi wa EPA wamelaumiwa vibaya sana na vigogo mbalimbali mafisadi serikarini kwani Ernest & Young waliwashikia bango serikari pamoja na kupigwa mikwara kibao na kuahidiwa tenda kibao za consulting iwapo wangeisaidia serikali kuficha ukweli.

Kampuniya Mekon Arch Consult Limited inamilikiwa na Mtu anaita Moses Mkony yeye hapo zamani alishakuwa Engineer wa serikalini akifanyakazi National Housing Corporation (alikuwa rubani???). Kwa sasa amestaafu na kufungua kampuni yake hiyo ya Mekon Arch Consult Limited iliyokuwa na ofisi zake sehemu ya Kijitonjama kichochoro cha karibu na Shule ya Msingi Kijitonyama.

Kampuni hiyo imeshirikiana na kitengo cha Bureau for Industrial Cooperation (BICO) ni kitengo cha chuo kikuu cha Dar es Salaam chenye kutoa ushauri (consultancy) kwa mambo mbali mbali ya ufundi kwa ujumla. Ni mradi wa Chuo Kikuu na sio kampuni binafsi lakini kiongozi wa BICO ni Dr. B.B. Nyichomba. Angalia web page ya BICO katika web site ya chuo kikuu Dar es Salaam

Aqe Associates Ltd pia ni kampuni ya hapa hapa ndani ya Quantity Surveyors wako pale Samora Avenue Dar es Salaam,. Tel 255 22 2118225; Tel 255 754 261482 na inamilikiwa na maofisa wa chuo cha Ardhi Institute pale Chuo kikuu, Mmoja wa washirika wake ni Dr. Aldo Lupala mhadhiri pale Ardhi. Wote hawa ni watanzania wala ?ya kimataifa?

Hizi ni kampuni za kimataifa za kukagua mahesabu ya ujenzi kweli? Makao makuu ya MEKON yako uchochoroni kijitonyama nyumba ya kupanga. Hii kampuni kweli ina ubabe wa kukagua mambo ya benki Kuu? Kutokana na udogo wao na uzoefu inashangaza jinsi kampuni hizi changa na ambazo zinatakiwa kuchunguza mradi mkubwa kabisa katika historia ya ujenzi nchini? Kwanini kampuni za kimataifa za kweli kama Pricewaterhousecooper, Deloitte & Touche au Ernst and Young hawakupewa kazi hiyo na hivyo kuhakikisha uhuru zaidi wa mchakato mzima?


Chanzo chetu kimoja cha KLHN kinadokeza kuwa ?Benki Kuu wanajuta kualika makampuni ya kimataifa ?kwani wamejifunza baada ya kuajiri makampuni ya kimataifa yanakuwa ngangari na kuwashikia bango na kuleta matatizo?

Taarifa kwa vyombo vya uchunguzi:

Ofisi za Mekon ziko Kijitonyama, ukiwa unatokea makumbusho kuelekea mwenge, unakata kona ya kushoto ya lami pale ?Sciencee? kuelekew Tandale. Ukiwa barabara hiyo ya Tandale hesabu kona ya tatu kushoto, inaangaliana na na ?car show room? moja kata kona hiyo ya kushoto kama unaenda kanisa la KKKT Kijitonyama utaona bango mkono wa kushoto, wanauza makuti ya kusuka, Ukipotea ulizia wanakouza makuti ya kusuka na mafuta ya taa.

Ofisi ya Mekon iko hapo. Mekon, Plot 602, Kijitonyama, P O Box 31924 Dar es Salaam, Tel. +255 22 2700784, Fax. +255 22 2647552, Mobile. +255 744 262 249 email
moses_mkony@hotmail.comau mekon@africaonline.co.tz

KLHN inauliza Je kampuni hizo zina utaaalamu wa wa uchunguzi wa kina wa kimahesabu na uwezo wa kugundua wizi wa kalamu?