PDA

View Full Version : Mwinjilist anapoinjilisha visivyoinjilishwa!

mwanakijiji
12-02-2008, 09:19 PM
na Charles Ndagulla, Moshi (Tanzania Daima)

MWINJILISTI Sadiki Moshi wa Usharika wa Mdawi Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi.

Mbali na hukumu hiyo, pia mshtakiwa huyo alitakiwa kumlipa mwanafunzi huyo fidia ya sh 500,000 baada ya kumaliza kutumikia dhabu yake.

Hukumu hiyo imetolewa hivi karibuni na Hakimu Sofia Massati wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alifutiwa shitaka la kubaka hatua ambayo ilizua utata wa kisheria na kubaki na shtaka moja la kumpa ujauzito mwanafunzi huyo ambaye mapema mwaka huu alijifungua mtoto wa kike.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi, Lwitiko Kibanda, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa, ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye mawazo na tabia kama ya mshtakiwa huyo hasa ikizingatiwa ni kiongozi wa dini.

Alidai mshtakiwa huyo amekwenda kinyume na kauli mbiu ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na viongozi kuwa mtoto ni taifa la kesho na anayo haki ya kupata elimu bora.

Aliongeza kuwa kitendo cha mshtakiwa kumpa ujauzito mwanafunzi ni kinyume na sheria inayosimamia elimu na kitendo hicho kimemwaathiri mwanafunzi huyo kwa kumharibia masomo na maisha yake ya baadaye.

Akitoa utetezi wake kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mshtikiwa huyo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa afya yake si nzuri na pia ana watoto yatima watatu wanaomtegemea.

Hata hivyo Hakimu Maasati alitupilia mbali utetezi huo na kumhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Wakati hukumu hiyo ikitolewa, mshtakiwa huyo kupitia akaunti ya baba mzazi wa mwanafunzi huyo,Japhet Urio, alikuwa ameweka sh 300,000 ikiwa ni sehemu ya sh milioni nne alizoahid kimaandishi kuzitoa kama gharama za kumtunza mwanafunzi huyo.

Kiasi hicho cha fedha kilikuwa kikijumuisha matunzo ya mtoto baada ya kukiri kimaandishi kumpa ujauzito mwanafunzi huyo na kuahidi kumtafutia shule pahala popote zikiwamo shule binafsi za sekondari.

My more
12-03-2008, 03:16 PM
Ama kweli yamemkuta mwinjilisti. Sasa swali langu ni hili hivi adhabu hii ya 5yrs jela inaaply hata kwa Waheshimiwa wabunge? au Wenzetu wana kinga katika jambo hilo?:D:D

mwanakijiji
12-03-2008, 03:41 PM
Ama kweli yamemkuta mwinjilisti. Sasa swali langu ni hili hivi adhabu hii ya 5yrs jela inaaply hata kwa Waheshimiwa wabunge? au Wenzetu wana kinga katika jambo hilo?:D:D

Labda wenzetu kutokana na nafasi ya Ubunge wana "haki" na vibonuses vya kazi...! Hadi mmoja tutakapombamba na kumuumbua ndio wataelewa.

My more
12-03-2008, 05:39 PM
Labda wenzetu kutokana na nafasi ya Ubunge wana "haki" na vibonuses vya kazi...! Hadi mmoja tutakapombamba na kumuumbua ndio wataelewa.

Yanamwagwa Ma-YUDA kibao, mtoto hajazaliwa wazazi wake washahamishiwa kwenye nyumba mpya. Mwalimu mkuu keshanunuliwa baskeli yeye na mkewe. :mad: :mad:

Kepa
12-03-2008, 11:37 PM
Yanamwagwa Ma-YUDA kibao, mtoto hajazaliwa wazazi wake washahamishiwa kwenye nyumba mpya. Mwalimu mkuu keshanunuliwa baskeli yeye na mkewe. :mad: :mad:

Mwenye pesa si mwenzio... !!! Hata hivyo siku hizi, Aliye juu kamsubiri keko...!!

Hao wote watafika tu kunako mkono wa sheria, Dawa yao imeshafikia degree 98.6 ikifika 100C. Wameumia.:cool:

Kepa
12-03-2008, 11:45 PM
Wakati hukumu hiyo ikitolewa, mshtakiwa huyo kupitia akaunti ya baba mzazi wa mwanafunzi huyo,Japhet Urio, alikuwa ameweka sh 300,000 ikiwa ni sehemu ya sh milioni nne alizoahid kimaandishi kuzitoa kama gharama za kumtunza mwanafunzi huyo.

Mbona nachanganyikiwa? ina maana pesa 300,000 zililipwa kabla ya hukumu? walijuaje angehukumiwa na faini pia? Najua adhabu yoyote kama ipo inayotolewa mahakamani, kama ni pesa basi hulipwa mahakamani then mdai anakabidhiwa na mahakama. Sasa inakuwaje zimewekwa direct kwenye account ya baba?

Nisaidieni kabla sijaonekana namtetea baba Mwinjilisti.

mwanakijiji
12-04-2008, 04:59 PM
Kepa nimeipenda hiyo ya "Aliyejuu mngoje Keko"!

Kepa
12-05-2008, 04:40 PM
Kepa nimeipenda hiyo ya "Aliyejuu mngoje Keko"!

Ni kweli mkuu, NINACHOSUBIRI KUONA KWAMBA YAMKINI wahusiika watajaribu kutupia macho hali ya usalama, usafi, maradhi, mlundikano na chakula huko magereza bse kutakuwa na additional demand from a new customer group.

Kuna mwaka mmoja kwenye shirika fulani tulitaka kupeleka huduma ya TV , mabranketi, net, nk kwenye magereza , wakuu walikuwa hawataki vipelekwe direct kwa wafungwa ila vikakabidhiwe kwa viongozi..na baadaye mikwara ikawa kibao.