PDA

View Full Version : Mengi atoa tuhuma dhidi ya Waziri

mwanakijiji
12-03-2008, 11:43 PM
Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi amekutana na waandishi wa habari na kusema mambo mengi na baadaye kutoa tamko lifuatalo.

TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI

Hivi karibuni waziri mmoja kijana anayeongoza wizara nyeti alipendekeza nibambikiziwe kodi bandia ya kiasi kikubwa nitakachoshindwa kulipa na hatimaye nifilisiwe kama njia pekee ya kuninyamazisha kabisa eti kama alivyofilisiwa tajiri mmoja mkubwa huko Urusi.

Alidai kwamba vyombo vyangu vya habari vimekuwa mno mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, jambo ambalo kwa maoni yake siyo zuri kwa sababu linawanyanyasa baadhi ya watu.

Nilitegemea waziri huyo msomi sana angefahamu jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi. Angalao angefahamu kwamba anayeamua nini kiandikwe na nini kisiandikwe ni mhariri wa gazeti ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari na siyo mmiliki wa vyombo vya habari.

Kama mkiristo na kama alivyoagiza Bwana Yesu namsamehe kwa vile hajui atendalo. Baada ya kumsamehe ningetaka ajue yafuatayo.

Asiyekemea maovu katika jamii, yeye ni sehemu ya maovu hayo. Waziri huyu na wale wote ambao wamekwishanitumia vitisho wakumbuke kwamba hata kama watafanikiwa kuvinyamazisha kwa hujuma zozote zile, vyombo vyangu vya habari, na hata kama mimi sitakuwepo tena, moto wa kupiga vita ufisadi uliokwishawashwa katika akili za wanajamii hauwezi kuzimika kamwe.

Ieleweke pia kwamba sauti za maskini na wanyonge katika jamii hazisikiki kwa urahisi. Vyombo vya habari husaidia kupaaza sauti na vilio vyao katika vita dhidi ya maovu. Ni wajibu wa kila mtu aliye na uwezo kusema kwa sauti kubwa kwa niaba ya wanyonge na maskini ili kutokomeza ufisadi.

Nachukua fursa hii kumpongeza sana Rais wetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuguswa na sauti na vilio vya wanyonge na maskini wa Tanzania kuhusu ufisadi na hatua za kijasiri zinazochukuliwa na Serikali yake dhidi ya ufisadi. Sisi sote ni lazima tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azidi kumpa ujasiri, nguvu na hekima nyingi wakati huu wa majaribio makubwa.

____________________
Reginald A. Mengi
Mwenyekiti Mtendaji
IPP Limited
3 Desemba,2008

NB: Vyanzo mbalimbali vimeihakikishia KLHN kuwa Waziri huyo ni yule mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani ya nchi. Vyanzo hivyo toka kwenye Jumba letu Kuu vimeihakikishia KLHN kuwa siku za hivi karibuni Waziri huyo amekuwa akijikuta akitajwa na vyombo mbalimbali vya habari na vile vya udaku wa mtandaoni akihusishwa na tabia mbalimbali ambazo kwa mujibu wa Jumba hilo vinaiweka vibaya sura ya uongozi wa Taifa.

Kuna uwezekano mkubwa katika mabadiliko madogo ya Mawaziri ambayo yanatarajiwa wakati wowote Waziri huyo akatemwa.

Kepa
12-04-2008, 12:31 AM
Waziri gani huyo msomi [B]hajui kazi, wajibu na umuhimu wa vyombo vya habari? [/B

]Ninawasiwasi na wale wasomi sana ambao hata majengo ya chuo anachosoma hajawahi kuyaona kwa macho wala kwa picha achilia mbali walimu wake. Hivyo vyuo ukimaliza kulipa ada tu unasubiria kutumiwa degree yako.

Sasa wakiipata hiyo bahasha pale posta mpya wanasumbuaaaaaa!!! :mad::mad:

omondi
12-04-2008, 09:49 AM
Sounds desperate. Mengi ni miongoni mwa wahasibu waliobobea Tanzania. Na kwa upepo ulivyokuwa ukimuendea tangu utawala wa Mwinyi, sidhani kuwa angefanya biashara yake kihuni. TRA wanafahamu uwezo wa Mengi kitaaluma hivyo mtu anayefikiria kumbambikizia kodi Mengi ameishiwa kabisa.

mwanakijiji
12-04-2008, 04:37 PM
Lakini kuna faida gani kwa serikali au baadhi ya watu serikalini kumdhibiti Mengi? Hawaoni kwamba ni wao watakaoharibu mbele ya jamii?

Kepa
12-05-2008, 05:23 PM
Lakini kuna faida gani kwa serikali au baadhi ya watu serikalini kumdhibiti Mengi? Hawaoni kwamba ni wao watakaoharibu mbele ya jamii?

Mwenyekiti mimi napata taabu sana kutofautisha kati ya malengo au maamuzi serikali na malengo au maamuzi ya watumishi wa serikali. Labda ndio maana naona wakati mwingine serikali inakuwa na double standards. Sijui hili limekaaje?

mwanakijiji
12-05-2008, 10:18 PM
wenye mgongano kati ya watu wenye madaraka na wale wenye pesa mara nyingi (kama siyo zote) wale wenye madaraka hushinda, kwa kadiri ya kwamba bado wana madaraka yale. Wakati huo huo hakuna watu ambao hawawaamini watawala kama watu wenye pesa. Hata hivyo ni wenye pesa kutokana na kutowaamini wenye madaraka hujikuta wakijiweka karibu na wenye madaraka ili angalau kuwa katika mazingira ya "kujua" nini wenye madaraka wanapanga dhidi ya wenye pesa.

Hata hivyo wenye madaraka mara zote wana hofu na wenye fedha kwa sababu wanajua kabisa kama wenye fedha wakitaka madaraka wanaweza zaidi kuliko wao (watawala) kutaka kuwa wenye fedha. Kutokana na mkinzano huo basi wenye madaraka mara zote wanawaangalia wenye fedha kwa shuku na wale wenye fedha wanawaangalia wenye madaraka kwa shuku.

Mgongano unatokea siku watawala wanapoamua kufanya kitu kinachowatishia wenye fedha au wenye fedha kufanya kitu kinachowatishia watawala; pande hizo mbili zinajiandaa kugongana na mgongano huo hauepukiki; ni mgongano wa lazima. Mgongano huu ni wa lazima ili kuweza hatimaye kuamua ni nani kati ya pande hizi mbili ndiyo mwenye nguvu zaidi (the most powerful).

Katika kuamua hili aidha mwenye madaraka anajitahidi ili na yeye awe na fedha nyingi au yule mwenye fedha nyingi naye apate madaraka. Ukimkuta mtu mwenye fedha pia ndiye mwenye madaraka basi utaiona nchi ambayo hakuna kinachofanyika zaidi ya kurushiana vijembe, migongano, chuki n.k lakini pia utaiona nchi ambayo watawala wake wanatawala kiimla zaidi na jamii inakuwa kama kiunga chao cha mpunga ambapo wanaweza kuamua kuvuna wapendapo au kuacha ndege wajilie.

Katika sakata tunalolishuhudia Masha ataweza kushinda tu endapo ataendelea kuwa na madaraka na Mengi ataendelea kuwa tishio kwa kadiri ya kwamba yeye ni tajiri. So one of them has to give in; mmoja asiwe na madaraka au mwingine asiwe tajiri! Kwa vile vyote viwili vina mvuto tofauti, ni rahisi kwa tajiri kuwa maskini (kwani anaweza kuanza upya kutengeneza biashara yake) kuliko kwa mwenye madaraka kuachia (kwani ni vigumu kuyapata tena).

Kwa vile mwenye madaraka anauwezo mkubwa wa kushiinda katika sakata hili, lakini kwenye kushinda mioyo ya wananchi, ushindi utakuwa kwa Mengi (yawezekana ndicho alichochezea kamari?), kwani at the end, watu watalign up na mtu mwenye fedha kuliko mtu mwenye madaraka! Don't ask me why!
__________________

Advocate Jasha
12-07-2008, 09:59 PM
Haya tena jamani CCM kuna mambo Huyu Mengi wakati wote alikua mfadhili wa CCM magazeti yake na vyombo vyake vya habari havikua vikitofautiana na magazeti ya chama na serikali.Namsifu kwa kitu kimoja KUSOMA MISHARE YA WAKATI kwani kuendelea kuisifu au kuunga mkono CCM na serikali iliyopo ni matusi kwa WATANZANIA .n CCM katika uchaguzi ujao uwezo wa kubaki madarakani ni mfinyu na kama upo ni kwa njia ambazo viongozi wa Zimbabwe na Kenya walivyobaki madarakani watu wenye akili timamu wameishaliona hilo wafanyabihashara na matajiri sitashangaa kama katika uchaguzi ujao watamwaga pesa zao kuipinga CCM na uongozi uliopo kwani uongozi uliopo ni mali isiuzika hata wakichota pesa zote za BOT na kutoka makampuni ya madini n.k bado hauziki ni bidhaa chafu ambayo hat kipofu anajua.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Ach-F
12-07-2008, 10:55 PM

Usiwa-underetimate CCM ni wezi mashuhuri wana uwezo mkubwa sana. Hivi sasa tayari wako kwenye kampeni ya kujisafisha si unaona akina Mramba na wenzake wako huru na hakuna tuhuma zozote nzito za Uhujumu wa Uchumi? Angalia akina Lowasa wanapeta tu , Karamagi pamoja na kulidanganya bunge kwa kusaini mkataba wa Buzwagi n.k.

Mazingaombwe ya CCM bado kabisa enjoy the movie. Angalia vibaraka waliopandikizwa kila kona.

Kepa
12-08-2008, 12:14 AM
'........Kwa vile mwenye madaraka anauwezo mkubwa wa kushiinda katika sakata hili, lakini kwenye kushinda mioyo ya wananchi, ushindi utakuwa kwa Mengi (yawezekana ndicho alichochezea kamari?), kwani at the end, watu watalign up na mtu mwenye fedha kuliko mtu mwenye madaraka! Don't ask me why!
__________________

Somo linakolea, Please do the needful

mwanakijiji
12-08-2008, 04:53 PM
Haya tena jamani CCM kuna mambo Huyu Mengi wakati wote alikua mfadhili wa CCM magazeti yake na vyombo vyake vya habari havikua vikitofautiana na magazeti ya chama na serikali.Namsifu kwa kitu kimoja KUSOMA MISHARE YA WAKATI kwani kuendelea kuisifu au kuunga mkono CCM na serikali iliyopo ni matusi kwa WATANZANIA .n CCM katika uchaguzi ujao uwezo wa kubaki madarakani ni mfinyu na kama upo ni kwa njia ambazo viongozi wa Zimbabwe na Kenya walivyobaki madarakani watu wenye akili timamu wameishaliona hilo wafanyabihashara na matajiri sitashangaa kama katika uchaguzi ujao watamwaga pesa zao kuipinga CCM na uongozi uliopo kwani uongozi uliopo ni mali isiuzika hata wakichota pesa zote za BOT na kutoka makampuni ya madini n.k bado hauziki ni bidhaa chafu ambayo hat kipofu anajua.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Advocate karibu tena!!

Kepa
12-12-2008, 03:16 AM
Mwenyekiti , baada ya kukisoma kijarida cha Cheche nimekupata vizuri zaidi.!!