PDA

View Full Version : Ndizi za Kichagga a.k.a Mtori

mwanakijiji
12-03-2008, 11:54 PM
Mapishi ya Bi Aziza yanaendelea...

VIPIMO

Ndizi mbichi 10
Nyama kilo 1
Nazi ya kopo 1
Chumvi Kijiko 1 cha chakula
Ndimu 1
Bizari ya manjano Kijiko 1 cha chai
Pili pili mbichi 3
Nyanya (tomatoes 2
Kitunguu maji 1
Thomu na Tangawizi ya kusaga Kijiko 1 cha chakula

.NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Kata nyama vipande vipande na uisafishe.
2. Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive.
3. Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi.
4. Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi.
5. Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria.
6. Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo.
7. Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi.
8. Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda.
9. Weka pembeni zipoe.
10. Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.

Kepa
12-04-2008, 12:00 AM
Leo umetupeleka kwetu kabisa mmhhhh hapa udenda nusu umwagikie juu ya lap top.

mwanakijiji
12-06-2008, 07:12 AM
sasa hata karibu?

Kepa
12-07-2008, 11:47 PM
sasa hata karibu?

Hata nilikuwa siijui taste yako, siku nyingine nitakukumbuka:D:D

MissiE
05-27-2009, 11:22 PM
Mapishi ya Bi Aziza yanaendelea...

VIPIMO

Ndizi mbichi 10
Nyama kilo 1
Nazi ya kopo 1
Chumvi Kijiko 1 cha chakula
Ndimu 1
Bizari ya manjano Kijiko 1 cha chai
Pili pili mbichi 3
Nyanya (tomatoes 2
Kitunguu maji 1
Thomu na Tangawizi ya kusaga Kijiko 1 cha chakula

.NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Kata nyama vipande vipande na uisafishe.
2. Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive.
3. Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi.
4. Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi.
5. Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria.
6. Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo.
7. Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi.
8. Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda.
9. Weka pembeni zipoe.
10. Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.

ahhhhh bwana wee....huo sio mtori...mtori unapondwa na hautiwi nyanya wala binzari!!hizo ni ndizi za kupikwa 2 basi kwa lugha ya kiswahili!majina ya kinyumbani yapo mengi!

mwanakijiji
05-29-2009, 09:28 PM
ahhhhh bwana wee....huo sio mtori...mtori unapondwa na hautiwi nyanya wala binzari!!hizo ni ndizi za kupikwa 2 basi kwa lugha ya kiswahili!majina ya kinyumbani yapo mengi!

unataka kusema kuna "mtori original"? Haya tupatie basi jinsi ya kuupika maana miye nilidhani ndiyo nimepatia hapo..LOL

mwanakijiji
05-29-2009, 09:30 PM
Hata nilikuwa siijui taste yako, siku nyingine nitakukumbuka:D:D

ndugu yangu mimi na uchaggani ni kama sumaku na chuma..!

MissiE
05-30-2009, 01:54 AM
unataka kusema kuna "mtori original"? Haya tupatie basi jinsi ya kuupika maana miye nilidhani ndiyo nimepatia hapo..LOL

upo sana 2

Mahitaji.....
Ndizi kiasi chako
Viazi kidogo-vinaongeza testy
Nyama na ukipata utumbo ule wa maziwa wanaita wenyewe ni mzuri kama unapenda
Vitunguu-kidogo ila sio lazima
Mafuta yakutosha
Chumvi ofcoz

Maandalizi...
Chemsha nyama
Menya ndizi na viazi alafu ukate vipande vidogo vidogo kiasi
Tia nusu ya ndizi na viazi kwenye sufuria,alafu tia nyama bila supu lakini,vitunguu kama unataka,chumvi, zile ndizi zilizobaki na maji kiasi....usiweke mengi mpaka uone yanatokezea....kiasi 2 chakutosha kuivisha na yakipungua unaweza kuongeza ila usizidishe...mafuta unaweza kuweka baada ya muda kidogo.
Acha mpaka ndizi na viazi vilainike kabisa, hakikisha hazina mchuzi mchuzi.Ziipue kisha uziponde ponde kama mash potatoes then weka ile supu ya nyama na uchanganye pamoja,kama bado ni nzito sana ongeza maji kidogo kidogo mpaka upate uzito uupendao.Ukimaliza hivyo rudisha kwenye moto kwa kama dkk kama 10...moto wa chini na mtori wako utakua tayari.