mwanakijiji
12-04-2008, 04:47 PM
(Toka Tanzania Daima, Jumatano Disemba 3, 2008)
Na. M. M. Mwanakijiji
TUTAKUWA ni waongo na wanafiki endapo tutabeza hatua tunazozishuhudia mbele ya macho yetu leo hii na kwa hakika tutakuwa wakanao historia kama hatutakubali uhistoria wa kile kinachotokea mbele yetu.
Macho yetu yanashuhudia kitu ambacho tafsiri yake yaweza kuwa ngumu kueleweka hadi pale kitakapochambuliwa vizuri. Aidha tunashuhudia mazingaombwe ya daraja la kwanza au mbele yetu tunachoona ni ndiyo “kitu chenyewe”.
Haya ni mazingaombwe?
Kati ya vitu ambavyo vinazungumzwa sana mitaani kufuatia hatua za serikali kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa vitendo mbalimbali vya kifisadi ni kama kweli tunachokiona ni ukweli au uzugaji tu.
Nimejiuliza kwa muda kwa nini watu hawajarukaruka kama kulungu kwa furaha kuona watuhumiwa wa ufisadi wakifikishwa mahakamani? Kwa nini kuna watu wanaona kinachoendelea ni mazingaombwe? Je tuna sababu ya kuona fahari au kujisikia kuwa tumepiga hatua kwenye vita vya ufisadi au matumizi mabaya ya madaraka? Fuatana nami.
Siyo mara ya kwanza kwa vigogo kufikishwa mahakamani.
Kuna kizazi cha Watanzania ambacho hakijawahi kushuhudia kesi nzito zinazowahusu watu waliowahi kuwa na nafasi serikalini au wale ambao kwa namna fulani wanaaminika kuwa wana ujiko wa aina fulani katika siasa za nchi yetu. Kizazi hiki bila ya shaka kinashangazwa na kutiwa moyo na hatua hizi za kufikishwa mahakamani wale wafanyabiashara ambao wanatuhumiwa wizi wa mabilioni, watumishi wa umma waliowezesha wizi huo na wale viongozi wa kisiasa ambao kutokana na nafasi zao wanadaiwa kuzembea na kulisababishia taifa hasara kubwa.
Hapa tunawategemea wataalamu wetu wa sheria na historia watatusaidia kuweka kesi hizi katika maudhui yake yanayostahili. Mwalimu Nyerere aliwahi kushtakiwa mahakamani na serikali ya kikoloni kwa makosa ambayo wakati ule yalionekana kuwa yana msingi.
Baada ya Uasi wa Kijeshi mwaka 1964 ambao ulisababisha uundwaji wa JWTZ tunavyoliona leo kulikuwa na msukosuko serikalini kitu ambacho baadaye kilisababisha mashtaka ya uhaini kuletwa katika kundi la watu ambao walikuwa ni wasaidizi wa karibu wa Nyerere na watendaji wa serikali.
Mionongoni mwao ni Oscar Kambona na Bibi Titi Mohammed. Ninawataja hao ili kuonesha kuwa kesi dhidi ya kiongozi au mtu aliyewahi kuwa kiongozi katika serikali au chama siyo ngeni nchini.
Siyo lengo langu kuangalia kesi hizo bali kuonyesha tu kuwa kama taifa tumeshawahi kuwa hapa. Kesi za kina Kambona na wenzake zilipaswa kuitikisa nchi, lakini kama taifa tuliweza kuhimili na kuendelea kuwepo.
Kesi nyingine ambayo naweza kuiweka hapa kuonyesha kuwa Tanzania imeshawahi kupitia msukosuko wa kesi kubwa na taifa likaendelea kuwepo ni kesi ya uhaini ya miaka ya themanini. Ni moja ya kesi zilizokuwa wazi na watu waliweza kuifuatilia kwa karibu sana; mwishoni mwa kesi ile kuna watu walipata kifungo na wale walioachiliwa. Pamoja na uzito wa kesi hizo mbili za uhaini, kosa kubwa zaidi dhidi ya jamhuri yetu, taifa bado lipo na limeendelea kuwepo.
Kwa upande wa biashara kuna kesi za uhujumu uchumi za miaka ya themanini. Kesi zile zilitufundisha mambo mengi sana na kutoa mafunzo makubwa juu ya utawala wa sheria.
Bahati mbaya sana baadhi ya kesi zile za uhujumu uchumi ushahidi wake ulikuwa mbovu na uendeshaji wake ulikuwa mbaya ambao baadaye ulisababisha rufaa zake kushinda na hatimaye walioshtakiwa kujikuta wakilipwa fidia kubwa kabisa. Ulimwengu wa biashara ulitikisika nchini na hofu iliwajaa watu.
Wakati ule hatukuwa na “mafisadi” tulikuwa na “Wahujumu Uchumi” watu waliotumia hali mbaya ya uchumi kuficha mali na kusababisha upungufu wa bidhaa katika jamii na kusababisha bei kupanda (bei ya kuruka). Kipindi hili biashara ya magendo ilitamalaki.
Baadhi ya mambo tunayoyafanya leo katika biashara msingi wake ni wakati wa uhujumu uchumi. Leo hii hata baadhi ya watu wanavyokwepa kodi, kuficha mali misituni, au kutumia “njia za panya” kuingiza mali nchini ni kutokana na mawazo ya “kilanguzi”. Tulikuwa huko, tukayaona na kama taifa tumesalimika.
Kwa upande wa madaraka kesi nzuri ambayo inaweza kutajwa hapa ni pamoja na kesi ya aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Nalaila Kiula, ambaye Serikali ya Mkapa ilimfikisha mahakamani na hatimaye baada ya mchakato akaachiwa jina lake likiwa limechafuliwa sana.
Leo hii serikali ile iliyomfikisha mahakamani imeshindwa kumpa nafasi ya kuitumikia nchi yake tena! Pamoja naye tunakumbuka alifikishwa katibu wa Wizara yake George Mlingwa ambaye alikutwa na hatia Mahakama Kuu, katumikia kifungo kwa muda hadi aliposhinda katika Mahakama ya Rufaa. Taifa liliyaona, likaendelea kuwepo.
Lakini kama kuna wakati ambapo tungeshtuka zaidi ni pale Rais Mkapa alipowastaafisha kwa manufaa ya umma maafisa wa ngazi za juu wa polisi ambao walituhumiwa kujihusisha na vitendo vya kifisadi.
Kustaafishwa kwao kulisikika radioni na wananchi wakaamini, kama si wote, kuwa ni mapambano dhidi ya ufisadi. Bahati mbaya au kutokana na uzembe wa Mwanasheria Mkuu maafisa wale hawakupiga magoti na kusalimu amri kwani baadhi yao walikuwa ni wanasheria na wote walijua haki yao kwa mujibu wa sheria ya polisi. Wakakata rufaa, wakaweza kuthibitisha katika mahakama zetu kuwa Rais hakufuata sheria kuwastaafisha na hivyo kudai mamilioni ya shilingi. Wakashinda! Taifa likaona, na likaendelea kuwepo.
Leo hii kuna kesi inaendelea ya aliyekuwa balozi wetu kule Italia ambaye anashtakiwa mfano wa makosa wanayoshtakiwa leo kina Mramba na watendaji wengine. Kesi inaendelea lakini hakuna la kushtua kwani tumewahi kufika hapa kama Taifa.
Hivyo mifano hiyo michache ya kesi kubwa kubwa ni ushahidi tosha kuwa Tanzania haiwezi kutikisika au kushangazwa kwa kushtakiwa viongozi au mtumishi wa juu wa umma. Tumeshayaona haya! Taifa letu haliwezi kushtushwa kusikia mfanyabiashara mkubwa ametinga kizimbani kwa tuhuma za ufisadi; tumeyaona hatuwezi kushtuka ati aliyekuwa waziri kafikishwa mahakamani! Hatuwezi kushtuka kusikia afisa usalama amekamatwa kwa kutumia madaraka yake vibaya, tumeyaona; hatuwezi kusikia kuna watu wamejaribu uhaini dhidi ya jamhuri yetu au kutishia usalama wa uwepo wetu kama Taifa, tumeyaona haya (mara mbili na ya tatu kule Zanzibar ilipanguliwa!).
Hapana, wananchi wasishtuke wala kutetemeshwa na haya. Tumeyaona na kwa kadiri tunavyoendelea kukua kama taifa tutayaona mengi na siku moja tusije kushangaa aliyekuwa Rais anafikishwa mahakamani au Rais aliye madarakani kaondolewa madarakani kwa mashtaka ya Bunge (impeachment). Hata hayo yote yatokee Tanzania itaendelea kuwepo!
Hivyo, kitendo cha kuwapelekea watu mahakamani peke yake hakitoshi kabisa kutufanya tuamini kuwa tunachoshuhudia siyo mazingaombwe. Niliandika karibu miaka miwili iliyopita kuelezea sanaa ya mazingaombwe ilivyo. Tutakuwa watu wa ajabu sana kama tutashangilia majigambo ya mwanamazingaombwe au mbwembwe za kuvutia onyesho.
Je ni kitu halisi?
Kuna mambo kadhaa ambayo yananitatiza kuhusu hatua hizi ambazo wengi tumelilia zichukuliwe na sasa zimeanza kuchukuliwa hatujui kama ni mazingaombwe au ndiyo “mchezo wenyewe”.
1. Mashtaka dhidi ya watuhumiwa wa EPA
Kesi yoyote ile inapoandaliwa kuna mambo kadhaa yanayoangaliwa. La kwanza na la msingi ni ushahidi uliopo na uzito wa ushahidi huo (preponderous of evidence). Ni ushahidi pekee ndio unatakiwa kuongoza msingi wa mashtaka yaliyopo lakini katika kuweza kuelewa uzito wa ushahidi huo na mashtaka gani yaletwe kinachoangaliwa ni sheria. Ni sheria ipi inayoweza kutumika kwenye ushahidi upi ili kuleta mashtaka yapi ndilo swali la msingi.
Lakini msingi wa kwanza katika mashtaka yoyote yale ni ushahidi kwani sheria zipo wakati wote mpaka pale kunapokuwepo na ushahidi wa kuvunja sheria hizo ndipo mashtaka yanapoweza kuletwa. Mwendesha mashtaka mzuri ni yule ambaye anaweza kuangalia ushahidi kwa upana wake na kuamua ni mashtaka gani ayalete dhidi ya mtuhumiwa.
Hivyo katika kesi hizi za EPA, tatizo langu la mashtaka nikisoma jinsi yalivyotolewa najikuta nahoji kama ushahidi uliopo hautoshi kuongeza mashtaka yaliyo makubwa zaidi kuliko yale ya “kula njama, kughushi, wizi na kujipatia fedha kwa udanganyifu”.
Kwa kadri mashtaka yalivyosomwa, naamini kesi hizi za EPA, haziwezi kabisa kuwa kamili bila kuongeza mashtaka ya kuhujumu uchumi (kwa mujibu wa sheria ya Kuhujumu Uchumi ya 1984) na pia mashtaka ya kufaidika kutokana na uhalifu kwa mujibu wa sheria ya “Kunufaika kutokana na Uhalifu” ya mwaka 1991. Sheria zote mbili pamoja na mabadiliko yake.
(Inaendelea Chini)