PDA

View Full Version : Aibu ya Taifa letu (Picha)



mwanakijiji
12-04-2008, 07:29 PM
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/gallery/mariam.jpg

Bi. Mariam, mwenye ujauzito aliponyoka na kunusu maisha yake mwezi wa kumi baada ya kuvamiwa na watu waliotaka kumuua na kuchukua viungo vyake kutokana na imani za kishirikina. Je, Masha anaona kuwa jambo hilo ni "dogo" na ambalo halistahili full exposure ya vyombo vya habari?

Je ingekuwa kwenye nchi iliyoendelea mauaji ya kulenga watu si yangezua sokomoko? Je tunakumbuka jinsi "DC Sniper" alivyoterrorize Wamarekani? au kisa cha Boston Strangler au yule Railroad Killer?

mfanyakazibora
12-05-2008, 05:42 PM
Waziri Masha anayaona haya?

mwanakijiji
12-05-2008, 06:12 PM
Waziri Masha anayaona haya?

Mwenye kazungumza na kusema siyo mambo makubwa; Hebu angalia habari hii inayoingia mida hii:


Albino auawa kwa kupigwa risasi na kunyofolewa mkono

2008-12-05 14:23:00
Na ITV Habari

Watu wenye silaha wamevamia nyumba ya mwenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino huko Kasulu mkoani kigoma na kumpiga risasi kisha wakanyofoa mkono wake na kuondoka nao.

Ndugu wa karibu wamemtaja albino aliyeuwawa kisha kukatwa mkono kuwa ni Bw. Zacharia John mwenye umri wa miaka 40.

Wamesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana wakati wauaji hao walipovamia nyumba ya albino huyo katika kijiji cha Kasumo.

kamanda wa polisi mkoani Kigoma kamishna msaidizi Abihaji Rashid amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia leo ambapo shughuli za mazishi zimezuiliwa hadi kukamilika uchunguzi.

Kamanda Abihaji amesema jeshi la polisi limetoa timu mbili za kutoka makao makuu ya polisi Kigoma, kikosi cha mbwa na ofisi ya mkuu wa polisi wilaya ya Kasulu kufuatilia na kuchunguza tukio hilo ili kuwanasa wahusika.

My more
12-06-2008, 04:23 AM
Naona watu ofisi zinawashinda, si wanyooshe mikono juu kiustaarabu wapokelewe? kweli haya mauaji ya kila siku ni mambo madogo???

mwanakijiji
12-06-2008, 08:11 AM
sijui na sisi tumpe siku saba?

My more
12-11-2008, 12:50 PM
sijui na sisi tumpe siku saba?

Yaani imebidi nicheke tu!!..... Lakini anastahili kushauriwa aipitie tena job description ya position yake. Then A...... kwa manufaa ya umma.

Shahada
12-11-2008, 03:03 PM
Kwa kweli ni aibu sana hivi ulimwengu unatuonaje wakati ulishatubatiza kisiwa cha amani?.... hivi kuna watanzaniawenye roho za kikatili namna hii?

Masha hebu wajibika achana na kupigizana kelele na Mengi

bulesi
01-12-2009, 02:15 PM
Sisi kama taifa tutakuwa mgeni wa nani katika karne hii ya Scince na teknolojia wakati watu wetu bado wanaamini ushirikina kama njia ya kupata utajiri kwa kuwaua binadamu wenzeo badala ya kufanya kazi kwa bidii !! Serkali isifanye mchezo na tatizo hili kama anavyoonesha Masha; waliokamatwa kwa kuhusika na mauaji ya albino kesi zao ziendeswe haraka as a matter of urgency na hukumu kali zitolewe kwa watakaopatikana na hatia ili liwe fundisho kwa wengine. Nadhani ni kwa njia hiyo tunaweza kukomesha aibu hii kwa nchi yetu.

Akajase
01-12-2009, 04:19 PM
Tatizo si kwa Wizara ya Mambo ya Ndani tu, pia hata kwa Wizara ya Sheria na Katiba. Kesi zimefunguliwa nyingi zinazohusu mazeruzeru waliojeruhiwa ama kuuawa lakini mwendo wa kesi hizo ni wakinyonga hivyo kuendelea kutengeneza mazingira ya washirikina, watafuta viungo vya wanadamu,kuzidi kuleta madhara kabla ya kuona nguvu ya sheria.
Upolepole huu wa mahakama unachangia kuuwa ndugu zetu. Sijui,kasi yaweza ongezeka pale atakapokufa ndugu wa Hakimu,Wakili au Jaji.Maana hawa jamaa hawataki kuguswa hata kama madhara yanazidi kutokea.wanatumia kigezo "Mahakama ni chombo huru hivyo kisiingiliwe na mtu,watu au taasisi yoyote".
Tanzania!! Tutafika tukiwa tumechoka sana.

mwanakijiji
01-12-2009, 04:51 PM
Akajase, umesema kweli kabisa kwa sababu licha ya matukio haya kuendelea sasa katika mwaka wa pili, hakuna hata mtu mmoja aliyekutwa na hatia ya mauaji ya Albino. Naamini tuna tatizo kubwa katika kupeleleza na kukusanya ushahidi au kwa namna moja au nyingine hatujaona uzito wa tukio hili bado.