mwanakijiji
12-05-2008, 09:10 AM
Tahariri
Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa makampuni ya IPP Bw. Reginal Mengi kufuatia habari zilizoandikwa zikimnukuu Bw. Mengi akimtuhumu "Waziri" mmoja kijana kuwa amemkusudia mambo mabaya. Bw. Masha akizungumza na chombo kimoja cha habari asubuhi hii amemtaka Bw. Mengi kutoa ushahidi wa madai yake hayo. Habari mbalimbali zimekuwa zikisema kuwa Waziri aliyekusudiwa na Bw. Mengi ni Waziri Masha ingawa yeye mwenye (Mengi) hakumtaja kwa jina waziri huyo.
Katika mazungumzo yake katika televisheni ya Taifa Waziri Masha kimsingi amejaribu kuzungumza kwa niaba ya serikali kuhusu tuhuma za Mengi kuhusu Waziri. Amefanya hivyo akiamini kabisa kuwa yeye ndiye mwenye nafasi na jukumu la kuitetea serikali. Amefanya hivyo akiamini kuwa kwa vile anayetuhumiwa ni Waziri basi Waziri mwngine aje kumtetea. Kumbe kwa kufanya hivyo amethibitisha kabisa kuwa hakuzingatia suala zima la impartiality (kutokuwa na upande). Wakati yeye ni mmoja wa mawaziri basi atakuwa vipi huru kudai Mengi amtaje "Waziri" huyo?
Tunaamini kama kuna chombo chochote cha serikali ambacho kilitakiwa kuzungumzia suala hili au kudai ushahidi zaidi ni aidha Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake au IGP au kwa upande mwingine Mwanasheria Mkuu. Na mtu wa tatu ambaye angeweza kabisa kudai ushahidi ili kuona kama sheria zimevunjwa ni Mkurugenzi wa Mashtaka kwani ni yeye pekee kisheria anayeweza kuingilia kati uchunguzi na kufuatilia ushahidi akiridhika kuna jambo au sababu ya kufanya hivyo. Hatujaona sababu yeyote ya Bw. Masha kulizungumzia au kulitolea kauli jambo hili.
Hoja yetu ni kuwa kama Masha anataka kuwa fair katika hizo siku saba basi kutokana na wadhifa wake (anasimamia Magereza na Jeshi la Polisi) hana budi kukaa pembeni ili asije kuonekana anataka au ametumia madaraka yake vibaya. Wito wangu kwa Waziri Masha ni kuwa kutokana na nafasi aliyonayo na kama kweli yeye ni mmoja au ndiye aliyekusudiwa na Mzee Mengi basi kitu cha kwanza cha kufanya ni kujiuzulu Uwaziri ili kupisha mchakato wa haki kuanza. Vinginevyo, yatakayosemwa na Polisi au vyombo vya Usalama tunayatalia mashaka makubwa kwani kutokana na nafasi yake ana uwezo mkubwa sana wa kushawishi mwelekeo wa kupatikana haki.
Tunakumbuka vizuri jinsi alivyojipeleka gereza la Keko ambapo marafiki zake wa familia ambao waliwahi kuwa mawaziri walikuwa wametupwa siku moja kabla na alikataa katakata kuelezea kilichompeleka huko au kiini cha mazungumzo yake na kina Mramba na Yona. Wakati huo huo tumefuatilia kwa makini jinsi kauli yake juu ya mauaji ya Albino ilivyozua songombingo na vyama vya walemevau kwani alionekana kupuuzia mauaji hayo kana kwamba ni jambo dogo tu na ni wazi chini ya uongozi wake mauaji haya yameendelea kana kwamba hatuna vyombo vya usalama.
Kutokana na nafasi yake hiyo basi tunaamini kuwa haiwezekani kabisa kuwa na "fair fight" endapo yeye Bw. Masha ataendelea kushika wadhifa wake huo na wakati huo huo kutoa masharti ya "siku saba" kwa mtu ambaye amelalamika kuonewa au kutishiwa maisha. Hofu yetu ni kuwa siku hizo "saba" zimetolewa kama mlio wa panda ya mwisho yenye kutuma ujumbe kuwa kile kilichokusudiwa kitatimia.
Amri yoyote itakayotekelezwa na Polisi au Magereza kwa ushauri, amri, au hoja za Bw. Masha dhidi ya Bw. Mengi au taasisi zake tutachukulia kama jaribio la kwanza na la makusudi dhidi ya vyombo vya habari na haki za Raia. Kama kweli Bw. Masha hana cha kuficha na hategemei cheo chake kuwa ni kinga tunamtaka ajiuzulu mara moja ili kupisha mchakato wa haki na afute kauli yake ya siku saba kwani chombo pekee chenye haki ya kutaka ushahidi kwa muda wa kisheria ni Mahakama.
Zaidi ya yote tunashangazwa kwanini hakutaka Spika Sitta aliyedai kutishiwa maisha huko nyuma atoe siku saba au kumtaka Mbunge wa Igunga Bw. Rostam Aziz ataje "wafanyabiashara" alioashiria wanamtafuta pale alipozungumza na waandishi wa habari. Zaidi ya yote hatujamsikia Bw. Masha akitaka siku saba za ushahidi kwa watu mbalimbali ambao wanaripoti taarifa Polisi na badala yake kama ilivyokawaida Polisi wanaachwa kufanya kazi zao kama kawaida.
Waziri Masha aache kazi za Polisi zifanywe na Polisi vingijnevyo kutokana na nafasi yake ana uwezo wa kuharibu ushahidi au kuharibu kabisa mwelekeo wa ushahidi. Tunatoa wito kwa wakuu wa Polisi ambao wana taarifa za Mengi kuzingatia sheria na kutotoa unfair advantage kwa Waziri wao ili kuminya au kunyima haki ili wasionekane wabaya kwa bosi wao.
Haki siyo tu itendeke, lazima pia ionakane inatendeka.