PDA

View Full Version : Elimu ya Tanzania

Matigari
12-06-2008, 07:55 AM
Nashukuru bwana Mwanakijiji kwa kutoa hii hoja, nimekuwa nikichungulia hapa kuona kama kuna mawazo lakini hakukua na lolote. Yafuatayo ni machache amabyo nadhani yatasaidia kuchokoza gumzo.

Elimu ya Tanzania ilivyo sasa hivi imetilia sana mkazo nadharia kuliko vitendo, ningekuwa narudi shule sasa hivi au ningekuwa mpangaji wa taaluma , ningeshauri wanafunzi wafunze elimu ya vitendo na ufundi. Ninapozungumzia ufundi si tu useremala na ujenzi na vitu kama hivyo, ningeshauri vijana wawe na ujuzi wa kufanya vitu ambavyo vitawaletea kipato hata kama hawajaajiriwa, kwa kupitia mabo kama kilimo, mapishi kusuka mikeka nk.

Vile vile niliposoma mimi hatukufundidhwa kwa kirefu mauaji ya wayahudi ( holocast) na African American civil rights movoment, hivyo tunakuwa ignorant wa the plight of African Americans na tunashindwa kulifahamu vizuru tatizio la mashariki ya kati na vipengele vyake vyote, amabvyo ni muhi,u katika kupanga mikakati ya siasa na masuala ya ushirikiano wa kimataifa. Nadhani an Avarage Tanzanian needs to be equiped with thisa information.

Vile vile tutafute jinsi ya kuwafundisha watoto wetu wae ba uzalendo, huwezi kujenga nchi yako kama unaidharau. Vinginevyo caruculum kitaaluma ilichanganywa vizuri at least mpaka kidato cha nne.

Naamimi kuwa wanaukumbi watachangia mengineyo. Tafadhali tuzungumze kuhusu hili, ni muhimu sana kwa vizazi vijavyo.

mwanakijiji
12-10-2008, 04:53 PM
Umekumbusha jambo moja muhimu sana; hivi vitabu vyetu na mitaala yetu ya historia imebadilika kwa kiasi gani? Sijui ni kwa kiasi gani tunajifunza historia mpya..

magoma
12-10-2008, 07:16 PM
Sasa mi nashindwa kuelewa mwanakijij, sasa tukisoma wote history hiyo nchi itakuwaje ina maana kila mtu atataka kuwa Kiongozi na wataalamu tutawapata wapi, na kwa upande wa tanzania kielimu mi naona kama mitaara ya cku hizi imejikita sana kwenye Technologia lakini hatuna vifaa vya kujifunzia ila inasomwa nadharia tu na sielewi tunakoelekea kwa sasa, vitabu kama JUMA NA ROZA vimepotea kabisa katika anga ya ulimwengu wa mtotto wa kitanzania sijui vilikuwa na kosa gani hadi kuondolewa kabisa katika elimu ya msingi.

Matigari
12-10-2008, 07:23 PM
Shukurani kwa kuichangia hii hoja. Naona haijawahasanisha wengi.

Sijafuatilia kwa kweli jinsi taaluma ilivyopangwa hasa katika somo la historia. Sijui hata kama huwa kuna kuirudia na kuibadilisha kutokana na wakati au la. Wenzetu mnaofahamu mpangilio wa wizara ya Elimu na vyombo husika tafadhalini tuelewesheni.

Jambo lingine ambalo nilisahau kulizungumzia awali ni kujaribu kuwafundisha watoto wetu wa kike na wa kiume masuala ya self esteem. kuwa na strong self esteem na confidence kutapunguza sana mabo yatokanayo; kama unwanted pregnacies, kutegemea kusaidiwa, na magonjwa na mengineyo. Je tunaweza kusema kuwa elimu ya jadi ilijaribu ( underline kujaribu) kupitia jando na unyago?

Shukrani kwa yote.

magoma
12-11-2008, 07:10 PM

watoto wenyewe hawa wanafundishika kweli mwanakijiji Mtigari!! kwanza huo unyago utaufundishia wapi watoto wengi wanajua picha za vita na kungfuu tu na Nigeria moves na michezo ya TVS especiaaly the Ze Commedy.

Matigari
12-12-2008, 04:18 AM
watoto wenyewe hawa wanafundishika kweli mwanakijiji Mtigari!! kwanza huo unyago utaufundishia wapi watoto wengi wanajua picha za vita na kungfuu tu na Nigeria moves na michezo ya TVS especiaaly the Ze Commedy.

Ndugu magoma, siyo kuwafundisha unyago waziwazi, hawawezi kabisa kukubali, ila mara moja moja unawaambia fact of life, tena ikitoka kwa mzazi ina nguvu za pekee. Kwa mfano tukiacha mambo mengine labda ambayo ni magumu kwetu kimila kuwaambia watoto ingefaa kuwakumbusha tu kuwa you will not be twenty years old for ever, time to grow up and be responsible, think where you would like to be in ten years from now etc., na kuwakumbusha kuwa mtoto siyo doll ambalo ukichoka kuchezea walibwaga. Tukiacha utani ninaumia sana nikiona vijana wanahangaika bila ya kazi simply because they were not focused when they were young.

Kuhusu suala la historia,nakumbuka nilipokuwa secondary school vijana wa sayansi walikuwa wanadharau historia, sidhani kama hoja ni kuwa sisi wote tuwe wataalamu wa historia hasha, lakini kabla hujatengeneza huo mtambo wa nuklia na vitu vingine vya kitechnologia unapaswa kujua matokeo yake, hense, try to understand Nagasaki, Hiroshima,uvutano uliopo kati ya North Korea na mataifa mengine, what is going on in Iran etc.