PDA

View Full Version : Kikwete akandia siasa za Nyerere

mwanakijiji
11-06-2008, 11:35 PM
Habari Leo

?Sote tumeishi katika mfumo ule wa kiuchumi na tunajua ni kiasi gani tuliteseka. Upinzani huu dhidi ya mageuzi ya sasa ya kiuchumi, ni kelele za kisiasa tu kutoka kwa watu wanaojifanya wamesahau hali ilivyokuwa wakati huo,? amesema Rais leo, Alhamisi, Novemba 6, 2008, mjini Arusha.

Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na kwamba upinzani huo wa kisiasa utaendelea kujitokeza hapa na hapa na kila baada ya muda, Tanzania kamwe haitarudi nyuma wala kuacha mageuzi yake ya sasa ya kiuchumi ambayo yameleta manufaa makubwa kwa wananchi.

?Kamwe hatutarudi nyuma, katika uchumi unaodhibitiwa na dola, ? amesisitiza Rais Kikwete wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) Mama Antoinette Sayeh kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC mjini Arusha.

Rais amekutana na Mkurugenzi huyo baada ya kuwa amefungua Mkutano wa 14 wa Vyombo vya Fedha katika Tanzania unaohudhuriwa na watalaam mbali mbali wa masuala ya fedha kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mikutano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka huandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Mama Sayeh yuko nchini kuhudhuria mkutano huo.

Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi, Mustafa Mkullo; Katibu Mkuu wa Wizara iyo, Gray Mgonja; Gavana wa BOT, Profesa Benno Ndullu na gavana wasaidizi ? Dk Enos Bukuku, Juma Reli na Lilla Mkila wamehudhuria mazungumzo hayo kati ya Rais Kikwete na Mama Sayeh.

Rais Kikwete amesema kuwa baadhi ya wanasiasa, kwa sababu zao tu za kisiasa, wamekuwa wakiibuka na upinzani dhidi ya mageuzi hayo muhimu, lakini akaongeza kusema kuwa tatizo la wanasiasa hao ni kwamba wamesahau hali ya uchumi na maisha ya wananchi yalivyokuwa wakati uchumi ukimilikiwa na dola.

?Mara watataka Serikali kuyafukuza makampuni ya madini, mara watasema kuwa nchi haihitaji wawekezaji. Uzuri ni kwamba haya hayatoki kwa wananchi. Ni ya sisi wanasiasa. Na unajua tena mwenendo wetu wanasiasa, kwa kadri unavyopigiwa makofi?Wakati mwingine baadhi yetu tunasahau haraka,? amesema Rais na kusisitiza:

?Lakini napenda kukuhakishia kuwa hakuna kurudi nyuma. Tumefanya maamuzi, tumeona faida ya maamuzi hayo. Mageuzi yamesaidia sana nchi yetu. Tutaendelea, na maneno haya ya wanasiasa yatafikia siku yataisha tu.?

Rais Kikwete pia amemweleza Mkurugenzi huyo kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa mpaka na Serikali katika kumaliza tatizo la Malipo ya Madeni katika Akaunti ya Nje (EPA) katika BOT.

?Tumefanya kila linalowezekana kuhusu EPA. Kumbuka haya ni madeni ya karibu miaka 30 iliyopita. Lakini sasa tumefikia kwenye hatua za kisheria. Tumeanza mchakakato wa kisheria. Tumejifunza mengi kuhusu mifumo yetu ya udhibiti na muhimu hapa ni kuhakikisha kuwa jambo kama hili halirudiwi tena,? amesema Rais na kuongeza:

?Dhamira yetu sasa ni kuongozwa na utawala wa kisheria, na siyo kuruhusu wanasiasa kutumia EPA kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe. Sasa kila kila kitu kiko mikononi mwa DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka wa Serikali).
Mwisho wa siku yeye ndiye mwenye madaraka na mamlaka ya mwisho kisheria. Mamlaka yake ni ya kikatiba, na wala haliwezi kuwa suala la uamuzi wa kisiasa.
Kamwe hata mimi siwezi kumwingilia.?

Mpita Njia
11-09-2008, 11:42 AM
Nadhani Rais amemiss some points. Kwanza, siamini kuwa madai haya anayoyazungumzia ni kilio cha wanasiasa pekee, ni kilio cha wananchi wengi ambao wameachwa nje katika mfumo wa uchumi anoutetea.
Pili, si kama watu wanataka mfumo uloiopo ufute na kurejea kwenye mfumo wa zamani. Wengi wangependa kuyaona manufaa ya mfumo unaotetewa na rais yakiwafikia watu wote, si wateule wachache kama ilivyo sasa. Ni kweli kuwa mfumo anaoutetea Rais una manufaa lakini hadi sasa manufaa yake hayajaonekana kwa watu wengi.

mchukia fisadi
11-09-2008, 01:56 PM
?Sote tumeishi katika mfumo ule wa kiuchumi na tunajua ni kiasi gani tuliteseka. Upinzani huu dhidi ya mageuzi ya sasa ya kiuchumi, ni kelele za kisiasa tu kutoka kwa watu wanaojifanya wamesahau hali ilivyokuwa wakati huo,? amesema Rais leo, Alhamisi, Novemba 6, 2008, mjini Arusha.

Ni wakati upi anaozungumzia Kikwete? mbona hasemi wazi wakati huo jamani? Je ni wakati wa sera za chama chake hiki hiki? Je leo anazikana sera zake?

Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na kwamba upinzani huo wa kisiasa utaendelea kujitokeza hapa na hapa na kila baada ya muda, Tanzania kamwe haitarudi nyuma wala kuacha mageuzi yake ya sasa ya kiuchumi ambayo yameleta manufaa makubwa kwa wananchi.

Kwa hiyo anawashitaki wapinzani kwa mabwana zake hao wa IMF? kwamba hawakubaliani na sera za hao mabwana wa dunia hii yetu sisi sote?

?Kamwe hatutarudi nyuma, katika uchumi unaodhibitiwa na dola, ? amesisitiza Rais Kikwete wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) Mama Antoinette Sayeh kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC mjini Arusha.

Na je uchumi unaomilikiwa na viongozi wetu na sio dola huo anasemaje? si ni sawa na uchumi unaomilikiwa na dola?

Rais amekutana na Mkurugenzi huyo baada ya kuwa amefungua Mkutano wa 14 wa Vyombo vya Fedha katika Tanzania unaohudhuriwa na watalaam mbali mbali wa masuala ya fedha kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mikutano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka huandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Mama Sayeh yuko nchini kuhudhuria mkutano huo.

Rais Kikwete amesema kuwa baadhi ya wanasiasa, kwa sababu zao tu za kisiasa, wamekuwa wakiibuka na upinzani dhidi ya mageuzi hayo muhimu, lakini akaongeza kusema kuwa tatizo la wanasiasa hao ni kwamba wamesahau hali ya uchumi na maisha ya wananchi yalivyokuwa wakati uchumi ukimilikiwa na dola.

Hili ni la wanasiasa au ni la wananchi wa Tanzania wasioona hayo mabadiliko anayosema Kikwete? Hivi kumbe wananchi tukiona mambo sivyo tunaitwa wanasiasa? ni lini wananchi tutatenganishwa na wanasiasa?

?Mara watataka Serikali kuyafukuza makampuni ya madini, mara watasema kuwa nchi haihitaji wawekezaji. Uzuri ni kwamba haya hayatoki kwa wananchi. Ni ya sisi wanasiasa. Na unajua tena mwenendo wetu wanasiasa, kwa kadri unavyopigiwa makofi?Wakati mwingine baadhi yetu tunasahau haraka,? amesema Rais na kusisitiza:

Nani aliyasema haya Bwana Kikwete? Si tunataka uyafukuze makampuni yasiyotaka kutulipa bali kuchimba na kuondoka huku madini yetu yakiwa yamekwisha kama walivyofanya Buhemba. Je ulimweleza huyo bwana mkubwa wako hivyo? Kumbe mara nyingine hata nyinyi waheshimiwa tena waheshimiwa sana mnasema uongo mnapokutana na wakubwa wenu?!:confused:?

Lakini napenda kukuhakishia kuwa hakuna kurudi nyuma. Tumefanya maamuzi, tumeona faida ya maamuzi hayo. Mageuzi yamesaidia sana nchi yetu. Tutaendelea, na maneno haya ya wanasiasa yatafikia siku yataisha tu.?

Maamuzi mengi yamefanywa na chama chako na wezi wenzio maana iko siku tutayakataa baada ya kuwakataa nyinyi wezi kwa njia ya kura . Hao IMF hawaji kupiga kura hapa. Sisi wadanganyika ndio tutakaopiga kura ya kuwakataa. Usidhani dhambi hii itawaponyoka. Hapana. Uko wakati wa kuwatia hatiani nyinyi au watoto wenu kama watafuata njia hii yenu.

Rais Kikwete pia amemweleza Mkurugenzi huyo kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa mpaka na Serikali katika kumaliza tatizo la Malipo ya Madeni katika Akaunti ya Nje (EPA) katika BOT.

?Tumefanya kila linalowezekana kuhusu EPA. Kumbuka haya ni madeni ya karibu miaka 30 iliyopita. Lakini sasa tumefikia kwenye hatua za kisheria. Tumeanza mchakakato wa kisheria. Tumejifunza mengi kuhusu mifumo yetu ya udhibiti na muhimu hapa ni kuhakikisha kuwa jambo kama hili halirudiwi tena,? amesema Rais na kuongeza:

?Dhamira yetu sasa ni kuongozwa na utawala wa kisheria, na siyo kuruhusu wanasiasa kutumia EPA kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe. Sasa kila kila kitu kiko mikononi mwa DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka wa Serikali).
Mwisho wa siku yeye ndiye mwenye madaraka na mamlaka ya mwisho kisheria. Mamlaka yake ni ya kikatiba, na wala haliwezi kuwa suala la uamuzi wa kisiasa.
Kamwe hata mimi siwezi kumwingilia.?

Kwa hili umejitahidi lakini ukweli ni kwamba bado tunakufuatilia kuona mwisho wa sakata hili usidhani tumekuacha. Kama na wewe ulichotewa ili upigie kampeni tutajua la kukufanya. Na ikiwa hutawakamata na rafiki zako tunaojua kuwa wanahusika kwa namna moja au nyingine katika wizi huo, tutajua la kufanya!