PDA

View Full Version : Chombo cha kuzama hakina usukani



dRU
12-07-2008, 10:11 AM
Mengi yamejiri katika kipindi cha Siasa za mpito ndani ya nchi nyingi za dunia na kuleta mabadiliko makubwa kisiasa na hata kiuchumi. Kuna pahala mpito huu haukuwa na muafaka na kusababisha machungu na maafa mengi kwa jamii. Tukienda na mtazamo huu inaweza kutuchua muda mwingi ndani ya Forum hii kufuatilia na kuchambua matukio ya nchi mbali mbali. Sasa huko si kwetu, letu hapa ni kuchambua japo kwa uchache yaliojiri hapa kwetu mpaka kufikia hapa tulipo hivi kweli tumekuwa "Chombo cha kuzama hakina usukani".!!!????

Mashaka yanakuwa mengi na wasiwasi unakuwa mkubwa kwamba nini hatma ya Chombo (Serikali) yetu miaka michache ijayo??

Kumekuwa na panga pangua ya serikali hasa Baraza la Mawaziri kwa kutafsiri kwamba labda panga pangua hii ingeleta nafuu kila panapopanguliwa na kuwekwa upya uongozi. Kama wanavyosema wenyewe "wanajipanga upya" - si kwa mantiki waonekane wapya bali wafanye mambo mapya ya maendeleo kwa jamii.

Mara nyingi panapotokea panga pangua kama hii huwa panatokea minon'gono kwamba pana uwezekano mkuu wa nchi kachangua watu eti kwa kulipa fadhila na si baada ay muda mrefu hutokea ule "u-Fadhila ya punda ni mateke". Na ndipo anajikuta katika hali ngumu ya kupambana na hao waliyopewa jina jipya la ubadhilifu na ufujaji mali ya umma "Ma-FISADI":confused::mad:

Sasa hivi jamii ya kitanzania imepevuka na imekuwa na uelewa mkubwa wa mambo mengi tu na huwezi kuwafanya tena kama usemavyo ule usemi wa "Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno" SI TANZANIA YA LEO na TANZANIA YA KESHO ndiyo itakuwa mahiri maradufu.

Hapana marefu yasio na mwisho, hivyo tuna hakika kwamba haya yote yanayojiri kwenye jamii yetu na serikali yetu yana mwisho wake lau kwa urefu wake hapanshaka tutauona mwishowe!! Tunasema "Kichango kuchangizana" hivyo wote pamoja na wanakijiji shime tuchangie hoja za kuondoa haya matatizo ya "UFISADI" ndani ya Siasa na Uchumi wa nchi yetu.. ieleweke UFISADI haukomi pale tuu walipomega EPA bali UFISADI ni ile tabia ya UBINAFSI ambayo wengi wetu wakipata nyadhifa za umma hujipendelea wenyewe na kusahau kwamba pale walipo ni "Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua":D