PDA

View Full Version : Tetesi za Mabalozi wapya



mwanakijiji
12-08-2008, 07:23 PM
Kuna dalili kuwa katika mabalozi wapya watakaotangazwa muda si mrefu watakuwemo vijana ambao wengine ndio itakuwa mara ya kwanza kushika nafasi ya Ubalozi. Sasa hivi jina mojawapo linalotajwa sana katika kuta za kidiplomasia ni Bi. Jairo ambaye yawezekana akaukwaa Ubalozi na kuiwakilisha Tanzania katika nchi moja ya Kiafrika ambayo inadaiwa ana "ujuzi wa kutosha"..

Tunaendelea kufuatilia balozi mpya wa TZ huko UN..

Mr. XXX
12-09-2008, 06:06 PM
Mabalozi wapya wanaweza kutangazwa wakati wowote kabla ya Krismasi au mapema baada ya mwaka mpya. Vijana na watumishi ambao wamefanya kazi yao vyema na wana utaalamu wa maeneo yao ndio wataangaliwa na kupewa nafasi hizo. Yote ni katika lengo la kuingiza kundi jipya la wanadiplomasia katika utumishi wa serikali yetu.

Tusiwaonee wivu au kufikiri wanapendelewa!

Kepa
12-12-2008, 03:11 AM
Tusiwaonee wivu au kufikiri wanapendelewa!

Sasa haya ya kuwa wivu tumeanza lini tena hapa kijijini?

bulesi
01-18-2009, 02:50 PM
Huyo mnaesema anatajwatajwa kuwa anaweza kuukwaa ubalozi wa nchi moja ya kiafrika ni Bi. Jairo au huyo Jairo msaidizi wa muungwana? Tafadhali tufafanulieni.

Mpita Njia
01-31-2009, 11:12 AM
Mabalozi wapya wanaweza kutangazwa wakati wowote kabla ya Krismasi au mapema baada ya mwaka mpya.

tarehe zinakwnda mkuu, na hatujasikia tangazo. Inakuwaje au imeahirishwa?

mwanakijiji
01-31-2009, 07:16 PM
tarehe zinakwnda mkuu, na hatujasikia tangazo. Inakuwaje au imeahirishwa?

tusubiri vitu tu.. si unajua kila kitu na timing yao. Kuna teuzi kadhaa za ubalozi zinazokuja. Kwanza kwa sababu kuna kundi jingine la mabalozi wanaostaafu so nadhani wakubwa wanaangalia "wakati muafaka". Upande mwingine kimbelembele chetu chaweza kumgharimu huyo dada..

Japhet
02-05-2009, 11:07 PM
Try to give us reliable news please!!! it is waste of time to keep commenting on tetesis!!!!

Angeris
02-06-2009, 01:36 AM
Mwanakijiji katika hii tetesi, je umemaanisha Bw.Jairo msaidizi wa raisi au Bi.Jairo? ni nani kikazi huyu bi. Jairo?