PDA

View Full Version : Masha ataka atumiwe maswali kwanza...

mwanakijiji
12-08-2008, 10:06 PM
TUmepata nafasi ya kuzungumza kidogo na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Lawrence Masha lakini tulipofikia cha kuzungumzia alikataa na badala yale alitaka atumiwe maswali ofisini kwanza ili ayapitie. Licha ya kumhakikishia kuwa maswali tuliyonayo hayahusiani na mambo ya kitaalamu au takwimu, yaani maswali yanahusu jambo/mambo anayoyajua tayari Bw. Masha alikataa kuzungumza na kuamua kukata simu...

Hii ina maana habari yetu ya kesho kwenye "Cheche" itaruka kama ilivvyo!!!

My more
12-08-2008, 11:05 PM
Kweli mheshimiwa waziri kaniacha hoi, yaani alikata simu kabla ya muafaka?? hii ina maanisha nini? uwoga au ubabe? lol
Ipaishe hivyo hivyo tu mkuu. nasafisha miwani yangu ili kesho nisipata taabu. :):)

mwanakijiji
12-09-2008, 12:10 AM
Jinsi alivyozungumza inaonesha alikuwa anasubiri simu yangu kwani majibu yake yalikuwa well crafted and prepared. Alipokata simu alikuwa anaonesha tu kuwa yeye ana madaraka; nimepata hilo na kina Msolla, Lowassa, n.k It is extremely rude and almost tyrannical..

dRU
12-09-2008, 12:41 AM

Wala usikate tamaa maaana "Atangaye na jua hujuwa". Kasahau kwamba "Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia" ... si kaanza!!:p:D

mwanakijiji
12-09-2008, 12:54 AM
Wala usikate tamaa maaana "Atangaye na jua hujuwa". Kasahau kwamba "Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia" ... si kaanza!!:p:D

dRU, misemo yako kwa kweli inanikosha haswa!

Ach-F
12-09-2008, 12:57 AM
Masha hafai kuwa waziri ni dizaini ile ile ya wezi kama kina Karamagi na Lowasa yaani kati ya watu millioni 40 tunapata wendawazimu kama huyu. MSISHANGAE KUONA HATA huko mambo ya ndani kinachoendelea hakionekani. He should be fired with immediate effect.

magoma
12-09-2008, 03:15 PM
Huyu bwana masha ana matatizo tena makubwa tu, huyu mtu anaonekana kama MAFIA FLANI aliyejimbia kwenye serikali yetu, huyu ni tatizo kubwa

Mr. XXX
12-09-2008, 05:59 PM
Mengi safari hii amejitakia. Huyu bwana mdogo Masha amekulia majuu na anajua kuwashughulikia watu wenye hela kama Mengi. Hili litakuwa fundisho kwa wafanyabiashara wengine wanaopenda kuchezea viongozi wa nchi yetu.

Mengi ni nani hata atoe tuhuma dhidi ya Waziri? Hajui kuwa Waziri ana uwezo mkubwa hata wa kumfunga? Subirini jumatano muone na hakuna mtu atakayeleta fyoko.

dRU
12-11-2008, 12:19 AM

Fika ninafahamu hapa kijijini si pahala pa malumbano, sawia kutoa hoja kwa uhuru wako wa habari, pamoja na ufahamu huu nimekuwa sina budi kulumbana japo kiduuchu na Mr XXX. -- Ni wengi wamekulia majuu na huko majuu hakuna mafundisho ama sera za kuwashughulikia wakubwa si wadogo --- yamejiri mambo kadha wa kadha toka kwa Mheshimiwa nasi ndani ya kiswahili husema "Heri kujikwa kidole kuliko ulimi" -- maana hili linapotokea huwa kama moto ndani ya majani makavu. Hatutaki kuona ubabe wa kuonyeshana nani zaidi ila tunachotaka kuona ni kwamba haki inatendeka bila ya kujali madaraka ama nyadhifa za mtu. Mr. XXX kumbuka kwamba "Mwenye kuchinja hachelei kuchuna":confused::confused::D:D

Advocate Jasha
12-13-2008, 01:15 AM
Hao wakina Masha,Makamba,Hosea,Mchikali na viongozi wengi katika serikali yetu na taasisi mbalimbali za Umma kwa kauli zao zisizo na kichwa wala miguu zimekua kichefuchefu kwa wengi kwa sababu hawajui nini wanachokisema na wapi wanapotoa kauli zao.Katika kipindi hiki tumeshuhudia kauli za ajabu ajabu nyingi za viongozi wetu CCM naona kunamkakati wa kujaribu kupunguza vituko hivyo hivyo wanadai maswali kabla ili watu wengine wawaandalie majibu.NI HATARI KUA NA RAIS ASIETOA MAAMUZI YOYOTE YALE KATIKA MASWALA MUHIMU YA NCHI LAKINI NI HATARI ZAIDI KAMA RAIS HUYO AMEZUNGUKWA NA VIONGOZI NA WASHAURI WASIOJUA WALIFANYALO!!!MUNGU IBARIKI TANZANIA