mwanakijiji
12-10-2008, 08:54 AM
http://mwanakijiji.podomatic.com/mymedia/thumb/13384/460%3E_1426122.jpeg
Sijafanya onesho jipya kwa muda sasa; hivyo leo nimefanya onesho jipya kufuatia tafakari yangu ya miaka 47 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Unaweza kusikiliza onesho hilo ukurasa wa mbele wa tovuti upande wa kulia mahali panaposema "Podcast" (pana alama ya "M")
Tulipodai haki yetu ya kuwa watu huru tulidai ili baadaye kiwe nini? Tulipoona fahari bendera ya Ufalme wa Uingereza ikiteremka taratibu usiku ule wa kukumbukwa na ya Tanganyika huru ikapindishwa tulikuwa tuna njozi ya aina gani ya Taifa? Siku ile wazee wetu walipocheza kwa furaha na kushangilia kuwa "na sisi ni huru" walikuwa wanafurahia uhuru hasa kutoka kitu nani na kwa nini? Je yawezekana kile tulichoshangilia wakati ule, miaka 47 iliyopita sicho ambacho tunacho leo hii?
Je njozi zile za wazee wetu ndizo zimetimia leo hii? Je watawala tulionao leo ndio viongozi tuliowatamani watutawale baada ya kumuondoa Mwingireza? Hoja yangu leo ni nyepesi kuwa tunachoshuhudia leo hii kutoka kwa watawala wetu ni dalili za kuonesha tu kuwa kuna mahali tumeenda kombo tangu wakati ule. Kuna kitu tulikiacha, kanuni tuliyoivunja, au njozi tuliyoificha ambayo ndani ya mioyo yetu bado tunaiwazia.
Karibu katika mfululizo wa maonesho yetu ya "funga mwaka" ambayo tunatumaini yataamsha fikra zao na kuchochea mwamko mpya wa kiraia ndani ya moyo wako na kukufanya nawe usiridhikie na hali iliyopo (status quo) na uwe tayari kushirikia katika mabadiliko tunayoyataka. Pamoja na Sisi tunaweza, mmoja mmoja tutabakia kubezwa! (Pichani vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Rais Kikwete na kutoa heshima siku ya Uhuru jana - Picha kwa hisani ya Issamichuzi.blogspot.com)