PDA

View Full Version : Kamusi

dRU
12-11-2008, 12:49 AM
Ninatoa changamoto ya kamusi mpya ambayo labda itatusaidia katika harakati zetu za ujenzi wa nchi yetu.. tafadhalini wana kijiji ongezeni uga wa kamusi hii na hata kurekebisha yaliyopo humu :

Kiongozi muadilifu awamu ya tatu = Mtu mwenye hisa katika kampuni binafsi ama mshiriki kuisaidia kampuni binafsi “ku-EPA”

EPA = Mahala maalum ndani ya benki kuu pa kujichotea mapesa kwa kiongozi muadilifu awamu ya tatu

Fisadi = Kiongozi muadilifu awamu ya tatu ambaye ana “vijisenti” vya mabilioni ya shilingi za kitanzania benki za ughaibuni

mwanakijiji
12-11-2008, 07:52 AM
Nimependa hiyo ya "EPA" kuwa mahali penye fedha za umma ambapo watu wanajichotea kinyume cha sheria!

Kepa
12-12-2008, 03:01 AM
Nimependa hiyo ya "EPA" kuwa mahali penye fedha za umma ambapo watu wanajichotea kinyume cha sheria!

Nafikiri hicho kisima baadae itabidi kibatizwe jina maalumu kwa kumbukumbu. Yaani mtu aliyekivumbua hicho kisima basi jina lake ndo lingetumika badala ya EPA. Mfano kama ni mimi KEPA ndio nilikuwa master mind wa EPA , then kisima kile cha Benk kuu kingeitwa ki-KEPA :D

mwanakijiji
12-12-2008, 03:10 AM
Nafikiri hicho kisima baadae itabidi kibatizwe jina maalumu kwa kumbukumbu. Yaani mtu aliyekivumbua hicho kisima basi jina lake ndo lingetumika badala ya EPA. Mfano kama ni mimi KEPA ndio nilikuwa master mind wa EPA , then kisima kile cha Benk kuu kingeitwa ki-KEPA :D

tayari kuna neno "kuepa" kwa maana ya kuepuka kitu ; tunaweza kutumia epa katika namna tofauti pia lakini kuitofautisha na ile nyingine napendekeza kuongeza "y" mbele yake

a. nahau - yepa (mahali ambapo fedha za umma zimeibwa) - hiyo ndiyo ilikuwa yepa yao wizara ya mambo ya Nchi za Nje!

b. kitenzi - epa - waliamua kuyepa mabilioni ya shilingi toka mfuko wa maendeleo wa Kijiji!