PDA

View Full Version : Lowassa kurudishwa kwenye uongozi?



mwanakijiji
12-14-2008, 02:38 AM
Kuna kila dalili ya kumrudisha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alijiuzulu kufuatia kuhusishwa na kashfa ya Richmond Mhe. Edward Lowassa kwenye nafasi ya uongozi wa juu wa serikali au ndani ya chama.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya kuaminika Mhe. Lowassa anaangaliwa kurudisha kwenye nafasi "yenye nguvu" ili kuhakikisha kuwa wakati CCM inaelekea kwenye uchaguzi mkuu 2010 basi Lowassa ahakikishwe amerudi kwenye upande wa Rais Kikwete baada ya kujikuta amewekwa nje kufuatia kujiuzulu kwake Uwaziri Mkuu mapema mwaka huu.

Inasadikiwa kuwa kurudishwa kwa Lowassa kwenye nafasi ya juu ndiyo njia pekee ya yeye kutokugombea 2010 dhidi ya Rais Kikwete na hivyo kuepusha mgongano kama ule wa Afrika ya Kusini katika ya aliyekuwa Rais Bw. Thabo Mbeki na aliyewahi kuwa Makamu wake Bw. Jacob Zuma.

Tunazo taarifa za uhakika mkubwa ni nafasi gani inaandaliwa kwa ajili ya Lowassa na itatengenezwa vipi.

Fuatilia kijarida cha Cheche ambacho kinaendelea kufuatilia suala hili taratibu.

Ach-F
12-14-2008, 06:02 PM
Mfa maji heshi kutapatapa. Serikali ya Mrisho ipo kwenye dhoruba kali sana na hivi sasa mipango ndiyo hiyo. Hata siku moja fisi aliyewekwa ngozi ya kondoo hawezi kubadilika na kuwa kondoo.

Waacheni wazame peke yao.

Mpita Njia
12-15-2008, 03:09 PM
Hivi kweli Lowassa ana nguvu kiasi hicho?!?

dickabudi
03-24-2009, 12:49 PM
Awamu ya tatu ilipoanza Mh Lowasa hakuwemo kwenye Baraza la Mawaziri hii pengine ilinatokana na Marehemu Baba wa Taifa kuwa hai na kuwaeleza CCM ukweli kwamba Lowassa hafai uongozi.

Hata Rais wetu alipomteua lowassa kuwa Waziri Mkuu wapo waandishi wa habari jasiri walimueleza bayana Mh Kikwete kuwa ameteua Waziri Mkuu kwa kujali urafiki si ufanisi wa kuendesha serikali nae akaahidi akikosea atamtoa...........yametimia kumrudisha kwa wadhifa wowote itakuwa sasa uongozi ni urafiki si ufanisi na umahiri wa kuendeleza nchi na wananchi wake

Mantaleka
03-27-2009, 06:56 PM
Kama hivyo ni kweli basi , punguwani si lazima aseme seme hovyo barabarani, hivi sikio la kufa kweli halisikii dawa.

mugagagigikoko
05-30-2009, 06:09 PM
Guys, let's be realistic:
Lowassa is young enough to need something meaningful to do with his life.
A snap shot at his CV, utaona kuwa maisha yake yote amekuwa kada wa CCM.
Kazi pekee ambayo amefanya ktk maisha yake yote kama raia huria, nina maana bila kuomba ujiko na kwa kutumia akili na ujuzi alionao, na si kwa kadi ya chama, ni kuwa meneja wa ukumbi arusha (AICC)
Tusishangae kuwa inabidi kwa nguvu zote atafutiwe nafasi naye aweze kuwa na lengo anapoamka asubuhi kutoka kitandani!
Ndivyo nchi inavyoendeshwa, na ndivyo CHAMA kinavyowatumia na kuwaangalia makada wake. Nothing new!