PDA

View Full Version : "Mramba bado Mbunge" - Spika Sitta



mwanakijiji
12-16-2008, 11:15 PM
Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa Mbunge wa Rombo ambaye hivi sasa anatuhumiwa na kesi ya jinai kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Bw. Basil Mramba anaendelea kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano mpaka pale kesi yake itakapomalizika na hatima yake kujulikana.

Spika Sitta akizungumza na chombo kimoja cha habari amesema kuwa mtuhumiwa anabakia kuwa hana hatia hadi pale atakapokutwa na hatia kwenye Mahakama. "Bila ya shaka mipango itafanyika kuona jinsi gani ataweza kufuatiia kesi yake na wakati huo huo kutimiza majukumuu yake ya Kibunge"

Spika Sitta ametoa ufafanuzi huo baada ya watu mbalimbali kuanza kuhoji juu ya kuendelea kwa Bw. Mramba kuwa Mbunge wakati akikabiliwa na tuhuma nzito Mahakamani.

Swali:
Kwanini kwenye nchi za wenzetu tuhuma tu zinatosha kabisa kumfanya mtu apoteze kazi yake?