mwanakijiji
12-18-2008, 05:15 PM
Hadi hivi sasa upinzani bado haujapata jaribio la kweli ambalo tunaweza kusema linapima jinsi unavyokubalika kufuatia juhudi zake za kufunua ufisadi nchini na kujenga hoja za kuhitajika uongozi mpya. Hapa nazungumzia kukubalika zaidi kwa upinzani baada ya uchaguzi wa 2005 na hasa kutokana na hali ya kisiasa kuonekana kuupendelea upinzani.
Katika chaguzi tatu ndogo zilizopita hakuna chama kilichokiondoa chama kingine kutoka jimbo walilokuwa wakishikilia. Mwanzoni ilikuwa ni Jimbo la Tunduru kufuatia kifo cha Mhe. Akukweti (CCM) aliyefariki baada ya kujeruhiwa katika ajali ya ndege. Uchaguzi ule ulitarajiwa kuonesha jinsi gani upinzani unakubalika na matokeo yake yalisababisha maswali zaidi kama kweli upinzani unaweza kukubalika. Wapinzani waligaragazwa Tunduru. Kiti kikabakia CCM
Ukaja uchaguzi mdogo wa Kiteto kufuatia kifo cha mbunge wake Mhe. Benedict Losurutia, huko nako wapinzani walipiga kambi na kufanya mikakati ya kila aina kuweza kuchukua kiti hicho lakini kutokana na sababu mbalimbali (wenyewe wanaweza kudai kuwa walionewa na dola) upinzani ulijikuta ukishindwa. Kiti kikabakia CCM
Katika uchaguzi wa Tarime, upinzani ulikuwa unatetea kiti cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime. Mhe. Chacha Wangwe. Licha ya jaribio zito la CCM kukitwaa kiti hicho matokeo yakaonesha kuwa upinzani bado unakubalika Tarime na hivyo kiti cha Tarime kikaendelea kubakia Upinzani.
Sasa uchaguzi wa Mbeya vijijini unaweza kuwa ni kipimo kizuri cha kukubalika kwa upinzani nchini. Kutokana na mazingira ya Mbeya vijijini kuwa karibu sana na ya miji mikubwa na watu wake kuwa katika eneo linalofikika kirahisi ni wazi kuwa kampeni zitakuwa ni motomoto na vyama vitapigana vikumbo. Zaidi ni utulivu wa kisiasa wa watu wa Mbeya vijijini kulinganisha na sehemu kama Tarime ambapo kulikuwa na mlundikano wa mambo mengi katika fikra za wapiga kura.
Kitu ambacho kitakuwa kinaangaliwa Mbeya vijijini ni jinsi gani wapinzani watajenga hoja ya kwanini wao waaminiwe kuchukua jimbo hilo badala ya kuiachia CCM. Yaani kwanini watu walioipigia kura CCM mwaka 2005 kwa kumchagua Marehemu Richard Nyaulawa waamue ndani ya miaka mitatu kubadili mwelekeo wao na kumchagua mbunge wa upinzani. Kikubwa ni uamuzi wa kupigia kura mtu au chama.
Mwaka 2005 yawezekana Mbeya vijijini walimpigia kura Mtu (Nyaulawa hata angekuwa upinzani angeweza kushinda); je wakati huu kitakachopigiwa kura ni chama au mtu? Je wapinzani ili waweze kushinda hawana budi kushirikiana au kila mtu aende kivyake vyake. Baada ya walivyotendeana kule Tarime, kweli wapinzani wanaweza kuaminiana tena?