PDA

View Full Version : Hii ndiyo Kagoda Agriculture ya EPA



mwanakijiji
11-07-2008, 04:12 PM
Mojawapo ya makampuni yanayotuhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na ambayo watendaji wake hawajafikishwa mahakamani na kundi hili la kwanza ni hii ya Kagora Agriculture. Kampuni hii peke yake ililipwa dola milioni 40 (zaidi ya Shilingi bilioni 42). Lakini hadi hivi sasa kuna utata wa kujua hii hasa ilikuwa ni kampuni ya nani? Kama vile RIchmond inaonekana kuna ugumu kweli wa kujua ni nani hasa mwenye hii kampuni.