View Full Version : "Bila CCM Tanzania haitawaliki" ...
mwanakijiji
12-19-2008, 05:40 PM
Nimepata kuzungumza "privately" na kiongozi mmoja wa CCM ambaye katika kubadilishana mawazo na mjadala motomoto alisema kitu ambacho bado kichwani na ni kitu ambacho akili zangu hazitaki kuamini lakini instincts zangu zinanidokeza kuwa chaweza kuwa kweli.. kuwa "bila CCM Tanzania haittawaliki"..
Sasa sielewi kama ni sentiments za kweli na sijui kama ana maana ya "CCM Madarakani" au "CCM kama chama cha kisiasa".. Inavyoonekana ni kuwa CCM imejikita katika fikra na mawazo ya watu wengi kiasi kwamba hawawezi kuiona Tanzania bila CCM!
Je ni kweli?
Matigari
12-19-2008, 06:27 PM
Greetings mzee Mwanakijiji. Je ulimuuliza kwa nini anafikiria hivyo? Kwani yeye anadhani CCM ni nini? Ni jina au ni watu? Anajua kuwa kuna watu hata humo humo CCm ambao wana uchungu na Tanzania, na wanaipenda nchi kuliko wanavyoipenda CCM, na hivyo wanaweza akatoka kwenda kuviunga mkono vyama vingine? Au anadhani kwa sababu vyama vingine viko vingi hivyo hakuna kimoja kitakachopata mandate?
NNionavyo mimi huo usemi una ukweli pale tu kama vyama vingine havitaungana, ingawaje hapo napo kutatokea tatizo kama hivyo vyama vitaanza kugombania madaraka.
Ach-F
12-20-2008, 11:48 PM

TANU na ASP ziliishia wapi? Mafisadi siku zote wanahitaji kuwashurutisha wananchi waamini kwamba bila CCM (magababacholi) hakuna Tanzania. Waacheni CCM waendelee na ndoto zao hata Obama aliposhinda hadi leo wengi hawajaamini kama kashinda. Wenye fikra kama hizo hawawezi kubadilika ni sawa na Robert Mugabe.
mwanakijiji
12-21-2008, 10:14 PM
Greetings mzee Mwanakijiji. Je ulimuuliza kwa nini anafikiria hivyo? Kwani yeye anadhani CCM ni nini? Ni jina au ni watu? Anajua kuwa kuna watu hata humo humo CCm ambao wana uchungu na Tanzania, na wanaipenda nchi kuliko wanavyoipenda CCM, na hivyo wanaweza akatoka kwenda kuviunga mkono vyama vingine? Au anadhani kwa sababu vyama vingine viko vingi hivyo hakuna kimoja kitakachopata mandate?
NNionavyo mimi huo usemi una ukweli pale tu kama vyama vingine havitaungana, ingawaje hapo napo kutatokea tatizo kama hivyo vyama vitaanza kugombania madaraka.
hilo wazo limenifanya mimi nifkirie pia kama lina ukweli wa aina fulani Lakini ukweli huo unanipa taabu kwa sababu yeyote mwenye mawazo ya namna hiyo anaaminii kuwa CCM inahodhi Tanzania na ya kuwa CCM ni kubwa zaidi kuliko nchi. Cha kusikitisha ni kuwa kweli wapo watu wanaoamini kabisa kuwa bila CCM Tanzania kutakuwa na vurugu au itakuwa vigumu sana kutawalika.
Swali kubwa kwetu ni je watu wenye mawazo ya namna hii tutaweza vipi kuwabidili?
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.