View Full Version : Sheria ya Usalama wa Taifa 1996
mwanakijiji
11-07-2008, 04:09 PM
Hii ni sheria iliyounda Idara ya Usalama wa Taifa (Idara ya Ujasusi) ya TISS. Ni sheria iliyoifanya idara hiyo kuwa butu kwa kuigeuza kuwa chombo cha kukusanya na kuchambua habari za kijasusi tu bila nguvu za kipolisi.
Daywell
02-04-2009, 10:59 PM
Nashukuru mwanakijiji kwa kuwa mstari wa mbele kutujuza baadhi ya sheria mbalimbali za nchi yetu, lakini naomba kujua kama sheria hizi zinapatikana kwa lugha yetu adhimu ya kiswahili kama ujuavyo watanzania tulio wengi hatuimudu vizuri lugha hii ya wenzetu ,na je hakuna mipango ya baadaye ya kuweza kutuwekea hapa matandaoni hizi sheria kwa lugha hii ya taifa?!
mwanakijiji
02-05-2009, 03:54 PM

Daywell, baadhi ya sheria utaona zimeanza kwa kiingereza lakini mwishoni ziko katika Kiswahili. Hata hivyo mojawapo ya mapungufu ya mfumo wetu wa sheria ni hilo. Sheria karibu zote zinaandikwa kwanza kwa Kiingereza halafu ndiyo zinatafsiriwa kwa Kiswahili. Hata hivyo sheria nyingi bado hazijatafsiriwa katika Kiswahili.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.