My more
12-23-2008, 07:09 AM
Majambazi yateka mwanamke
na Ahmed Makongo, Bunda
WATU watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi, wamemteka mfanyabiashara Specioza Nestory wa mjini Bunda, mkoani Mara na kumficha mlimani kwa zaidi ya saa tatu na kisha kumwamuru awapeleke dukani kwake ili awapatie fedha zote za mauzo ya siku hiyo.
Tukio hilo lililothibitishwa na polisi, lilitokea juzi majira ya saa 1:30 jioni ambapo mfanyabiashara huyo wa kike, alitekwa na watu watatu waliokuwa na bunduki na mapanga.
Akisimulia tukio hilo mwanamke huyo alisema baada ya kufunga duka lake majira ya jioni, aliondoka kwenda nyumbani kwake, lakini njiani alikutana na watu watatu waliomteka na kumpeleka mlimani na kukaa naye huko kwa zaidi ya saa tatu.
?Baada ya kuniteka walisema nisijaribu kupiga kelele, waliniambia hawataniua ila wanataka pesa tu na mimi nikawambia kwamba hapa nilipo sina pesa kwani ziko dukani, tukienda dukani nikifungua nitawapa peza zote za mauzo walizotaka,? alisema Specioza.
Alisema mumewe alipoona mkewe harudi kutoka dukani, aliamua kwenda dukani na kuweka makufuri mengine katika milango ya duka hilo na kisha alienda kutoa taarifa polisi za kutoonekana kwa mkewe katika mazingira tatanishi.
Mwanamke huyo alisema walikaa mlimani huko hadi ilipofika majira ya saa 4:30 usiku, ndipo watu hao walimwamuru awapeleke dukani kwake na kuwapatia pesa pamoja na vocha za simu za mkononi.
?Pamoja na mume wangu kutoa taarifa polisi juu ya kupotea kwangu kwa sababu haikuwa kawaida yangu, polisi hawakuja kufanya doria sehemu ya duka letu mapema na kama wangewahi, wangewakamata,? alisema.
Alisema baada ya kufika dukani hapo, alijaribu kufungua lakini alishindwa, ndipo walijitokeza walinzi wawili akiwemo mlinzi wao aitwaye Mwita Marwa (35), aliyekuwa amejibanza pembeni.
Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, majambazi hayo yalipobaini kwamba kuna walinzi wanawanyatia, waliamua kufyatua risasi hewani na kumkata kwa mapanga mlinzi wao.
Baada ya kushindwa kuiba katika duka hilo, waliamua kuondoka na kuambulia sh 1,500 tu, pamoja na simu ya mkononi iliyokuwa ndani ya mkoba wa mwanamke huyo.
Muuguzi wa zamu katika Hospitali teule ya Wilaya ya Bunda, (DDH) alikolazwa mlinzi aliyejeruhiwa katika tukio hilo, Benjamin Masatu, alisema hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri, baada ya kushonwa nyuzi sita.
Matukio ya ujambazi wa kutumia silaha kwa siku za hivi karibuni, yamekuwa yakitokea mara kwa mara mjini Bunda, ambapo watu wawili wamekwisha uawa na majambazi hao na wengine wanne kujeruhiwa katika matukio tofauti.