PDA

View Full Version : Yaani ziara ya Pinda kwao izuie mikutano ya kisiasa?



mwanakijiji
12-23-2008, 04:50 PM
Polisi wamtumia Pinda kuzuia mkutano wa Zitto

2008-12-23 12:25:59
Na Muhibu Said


Jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda, mkoani Rukwa, limezuia mkutano wa hadhara uliokuwa uhutubiwe na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe kwa madai ya kupisha ugeni wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyeko wilayani humo.

Habari kutoka Mpanda zilizolifikia Nipashe jijini Dar es Salaam jana, zinaeleza kuwa mkutano huo, ambao awali ulikuwa ufanyike jana katika viwanja vya Muleba, Kata ya Kawajense, wilayani humo, uliandaliwa rasmi na uongozi wa Chadema Jimbo la Mpanda-Kati kwa ajili ya kuhutubiwa na Zitto.

Kwa mujibu wa habari hizo, Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alifika Rukwa juzi akitokea mkoani Mbeya kutekeleza operesheni ya Chadema, maarufu kama ``Operesheni Sangara`` kwenda mkoani Kigoma.

Hatua hiyo, ambayo imechukuliwa na polisi kupitia barua yao yenye Kumbukumbu namba MPA/B.3/24/VOL.I/316, ya Desemba 22, inafuatia uongozi wa Chadema katika jimbo hilo, kuliandikia jeshi hilo barua Desemba 19 na 22, mwaka huu kuliarifu kuhusu kusudio lao la kutaka kufanya mkutano huo.

Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) ya Mpanda, ambayo Nipashe inayo nakala yake, polisi wanaeleza kuwa, hatua hiyo inatokana na askari kuweka ulinzi kwenye mkutano huo hawatoshi kufuatia ugeni wa Pinda.

``Kwa niaba ya jeshi la polisi, ofisi yangu inawajulisha kuwa hamjaruhusiwa kufanya mkutano wowote wa hadhara mpaka hapo baadaye mtakapojulishwa.

Hii kutokana na askari wa kufanya ulinzi kwenye mkutano huo wa hadhara hawatoshi kufuatia ugeni wa Mheshimiwa Waziri Mkuu tulionao hapa wilayani,`` ilieleza sehemu ya barua hiyo ya polisi.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu kutoka Mpanda jana, Zitto alisema sababu zilizotolewa na polisi hazina msingi kwani anaamini wamezuia mkutano huo makusudi kwa vile ulitaka kuhutubiwa naye.

Zitto alisema anaamini hivyo kwa vile taarifa za kufanyika mkutano huo, zilipelekwa polisi mapema tangu Desemba 19, mwaka huu, baada ya uongozi wa Chadema katika jimbo hilo kumuomba afanye japo mkutano mmoja, lakini siku zote hizo polisi hawakutoa taarifa zozote za kuzuia.

Alisema kwa vile viwanja vya Muleba, ambako mkutano wake ulipangwa ufanyike viko jirani na Ikulu, jana waliamua kuwaandikia polisi barua kuomba wahamishie mkutano huo katika viwanja vya Sikonge ili kuepuka kumsumbua Waziri Mkuu.

``Hata hivyo, busara yetu ya kuepuka kumsumbua Waziri Mkuu polisi wameipuuza, wameamua kuzuia mkutano wangu,`` alilalamika Zitto.

Alisema kabla ya mkutano wake kuandaliwa, uongozi wa Chadema jimboni humo, ulifanya mkutano wa hadhara jana yake bila wasiwasi wowote.

My Take:
Haya ndiyo mambo ya watu waliolewa madaraka! Sasa kama kina Zitto wangetaka kuandamana hadi Ikulu kuna ubaya gani? Yaani tumefikia mahali kuwa alipokuwa kiongozi wa kitaifa mawazo mbadala yasitolewe kwa sababu "tunamsumbua". Kama angekuwa hapendi kusumbuliwa asingeingia kwenye siasa!

Ach-F
12-24-2008, 02:51 AM
Pinda anatamani kuwa kama Robert Mugabe.