PDA

View Full Version : Wadhamini CCM: Lowassa na wenzake washitakiwa!

mwanakijiji
12-23-2008, 06:13 PM
Mwandishi Wetu

Mfanyabiashara wa Jijini Dar-es-Salaam Bw. Ibrahim Gulam Alibhai ameiomba Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi kuwakamata na kuwatia kifungoni maofisa kadhaa wa Chama cha Mapinduzi kwa kukiuka amri ya mahakama. Miongoni mwa maafisa hao ni waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu Bw. Rashid Kawasa, Bw. Edward Lowassa,na Jaji Joseph Sinde Warioba.

Viongozi wengine ambao wanahusishwa katika ombi hilo ni pamoja na Pius Msekwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara). Wadhamini wengine wa CCM wanaohusishwa katika kesi hiyo ni pamoja na Bw. Peter Kisumo, Job Lusinde, Khamis Mkandara, na Juma Ame.

Viongozi wa tawi la Gerezani wanaohusishwa katika kesi hiyo ni Bw. Ismail Idris (Mwenyekiti), Bi. Fatuma Abubakar (Katibu), Ahmed Ally na Bi. Khadija Jabir.

Bw. Alibhai amedai kwenye mahakama hiyo kuwa wadhamini hao wa Chama pamoja na uongozi wa tawi la CCM Gerezani mjini Dar wamekiuka amri iliyotolewa na Mahakama hiyo kuzuia (injunction order) kwa uongozi huo wa CCM kuendelea na ujenzi wa jengo kwenye kitalu namba 11, kiwanja namba namba 53 nyumba na. 107 ambacho kinabishaniwa katika kesi ya msingi.

Katika kiapo chake Bw. Gulam amedai kuwa tarehe 8 Mei mwaka huu Mahakama hiyo chini ya Jaji Alice Chinguwile ilizuia wahusika hao, mawakala wao, wafanyakazi na watumishi mbalimbali kufanya shughuli yoyote ya kukiendeleza kiwanja hicho kilichoko katika Mtaa wa Sikukuu eneo la Kariakoo wakati kesi ya msingi bado inaendelea.

Mfanyabiashara huyo amedai kuwa alipotembelea eneo hilo tarehe 12 mwezi huu alikuta eneo hilo likiendelea na ujenzi kinyume na amri ya Mahakama Kuu. Mmoja wa mawakili wanaomuwakilisha mfanyabiashara huyo alimshauri Bw. Gulam kuwa kitendo kinachofanywa kwenye kiwanja hicho ni kinyume na amri ya mahakama. Wakili huyo Bw. Mabere Marando ndiye anafuatilia shauri hili jipya.

Kwa mujibu wa Bw. Gulam, yeye ndiye mmiliki halali wa kitalu hicho na anayo hati na. 2635 ya kumiliki kiwanja hicho. Bw. Gulam anadai kuwa mwaka 1980 alikubaliana na CCM kuwa watumie nyumba iliyopo hapo ila yeye wampatie eneo jingine. Hata hivyo aligundua baadaye kuwa eneo alilopewa na CCM halikuwa mali yake bali ilikuwa ni mali ya wamiliki wengine halali.

Shauri hilo limeandikishwa na kupewa namba 81/2008 na bado halijapangiwa jaji wa kulisikiliza.

Mapambano
12-24-2008, 01:48 PM

this a good sign..watu wanaanza kusimama..ccm wameburza wengi sana kibiashara sema kwakuwa wao ni serikali wengi waliogopa kuwashtaki!!