mwanakijiji
12-25-2008, 11:19 PM
Watoto wanne wa Kimasai wafa kwa kulipukiwa na bomu
2008-12-23 22:46:57
Na Radio One Habari
Watoto wanne wa Kimasai wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu katika kijiji cha Embukoi karibu na eneo la kambi ya mafunzo ya Jeshi la polisi Kilelepori wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro.
Wakizungumza na Radio One Stereo katika eneo la tukio wanachi wa kijiji hicho wamelaani kitendo kilichotokea kwa madai kuwa wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu katika serikali ya mkoa bila mafanikio.
Wamesema kuwa wameshapeleka malalamiko yao Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bwana Mohamed Babu kuhusu madhara yanayowapata.
Madhara hayo ni pamoja na mifugo yao kuuwawa pamoja na wanawake wajawazito kuharibika mimba na wazee kupata mishtuko na kufariki dunia kutokana na mabomu na silaha za moto zinazopigwa katika kambi hiyo ambayo iko katika makazi ya watu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Bwana Lucas Ng`hoboko amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewataja watoto hao kuwa ni Larta Lota, Samweli Julius, Liyomomo Olikirima na Rose Saningo na majeruhi ni Isaya Ndiogi ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu.
Watoto hawa walilipuliwa na mabomu mwanzoni mwa wiki hii huko Siha, Kilimanjaro (Habari zaidi na MROKI MROKI (http://mrokim.blogspot.com))
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/watotonabomu1.jpg
Askari polisi wa kituo cha Siha wakiichukua miili ya watoto waliofariki baada ya kulipukiwa na bomu kwa ajili ya kuihifadhi katika hospitali ya Kibong’oto iliyopo wilayani humo kwa uchunguzi zaidi
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/watotowaliolipuliwa.jpg
Miili ya maiti za watoto waliofariki ikiwa katika bonde la kijiji cha Embukoi mara baada ya kulipukiwa na bomu katika bonde la mlima Embukoi uliopo wilayani Siha mkoani Kilimanjaro. Bomu hilo lilikuwa likitumiwa na askari polisi wakati wa mazoezi ya shabaha katika mlima huo.