PDA

View Full Version : JWTZ na Ufisadi - Nchi iko salama?

mwanakijiji
12-26-2008, 08:42 AM
Katika utawala wa kidemokrasia na katika nchi ambayo inaongozwa na katiba, hakuna chombo muhimu na chenye uzito mkubwa katika kulinda Katiba hiyo kama Jeshi. Mahali popote duniani, Jeshi ndicho chombo cha mwisho kabisa chenye kuweza kulinda Taifa na ndio pekee ambao kwa maisha yao wanaapa kulinda mipaka ya Taifa hilo.

Maana yake, jeshi ndicho chombo pekee chenye uwezo, jukumu, na kuhakikisha Taifa linakuwepo. Polisi wakishindwa, Usalama wa Taifa wakishindwa, Magereza wakishindwa, Wanasiasa wakishindwa, viongozi wa kidini wakishindwa; Jeshi linatakiwa kuweza. Ndiyo ngao yetu pekee ya kuhakikisha kuwa tunaendelea kubakia kuwa huru na kuwa Taifa.

Ninapofikiria kifo cha Brig. Nyirenda ambaye leo watu wanamtaja kama shujaa, ninapowafikiria kina Mwita Kyaro, Walden, Musuguri, Tumainieli Kiwelu na wengine waliopitia jeshi letu na nikiwafikiria hawa kina Mboma na wenzake na sakata zima la Meremeta na dhahabu, ninabakia na swali moja tu:

Jeshi linapohusishwa na ufisadi, na uongozi wake ukakaa kimya, je linaweza kweli kulinda uhuru wetu? Je tuko salama mikononi mwao kama wao wenyewe ndiyo wanatajwa katika ufisadi?

elien
12-27-2008, 11:42 PM
Mwanakijiji, I personally support most of your posts, however some goes beyond your understanding as journalist & .... This post reminds all of us that sometimes we should stop pretending we know everything in every field !!!

Vita halisi popote duniani haipiganwi kwa silaha. Vita vya silaha ni LAST MILE SOLUTION kwa utatuzi wa migororo. Kunapokuwa hakuna vita ujue vita halisi zinapiganwa vizuri na kwa namna isiyoamsha migongano ya wazi.

Najaribu kukuonyesha kuwa tafsiri yako juu ya jambo hilo haikuwa sahihi.

mwanakijiji
12-28-2008, 12:53 AM

Elien.. una maana Meremeta na JKT kuanzisha kampuni ya ulinzi ni sehemu ya "vita".. ?