PDA

View Full Version : Mzazi: Pombe si chai?



mwanakijiji
12-26-2008, 08:58 AM
Haya yanasimuliwa na Mroki kuwa yameonekana Coco Beach katika kusherehekea Xmass!

Huyu ni mzazi?

http://3.bp.blogspot.com/_mqjENGefutg/SVO034Qux4I/AAAAAAAABUE/rrMrMIeEtS0/s1600-h/Mama.JPG


Na huyu ni mtoto

http://2.bp.blogspot.com/_mqjENGefutg/SVO04Zvb0GI/AAAAAAAABUM/uUWGQUEWQjM/s400/Laga.JPG

wapi na wapi?

My more
12-27-2008, 05:59 AM
Sijui na hii tuusingizie utandawazi???

duru langu
12-27-2008, 06:25 PM
yawezekana ukosefu wa maji bomba eneo hilo hivyo
maji yamehifadhiwa kwenye hiyo chupa ya larger

mwanakijiji
12-27-2008, 07:22 PM
Mtoto afa kwa kunyweshwa gongo na mama yake mzazi

2008-12-27 15:02:29
Na Charles Masayanyika, Manyara

Mwanafunzi wa darasa la kwanza, mkazi wa kijiji cha Komolo, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, amekufa kwa madai ya kunyweshwa na mama yake pombe haramu aina ya gongo.

Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Luther Mbutu, alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Fausta Hango (50) anayedaiwa kujishughulisha na biashara ya pombe ya gongo.

Aidha, Kamanda Mbutu alimtaja mtoto anayedaiwa kufa kwa kunyweshwa pombe hiyo kuwa ni Sifael Raphael (6) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Komolo.
Alisema tukio hilo lilitokea Desemba 23, mwaka huu saa 12:00 jioni kijijini hapo.

Kamanda huyo alisema uchunguzi wa tukio hilo umebainika baada ya mwili wa mtoto huyo kufanyiwa uchunguzi na daktari na kuonyesha kuwa kifo chake kilisababishwa na ulevi wa pombe hiyo haramu.

Kamanda Mbutu alisema mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji ya mtoto wake na kuuza pombe haramu kinyume cha sheria.

Na katika tukio lingine, mkulima wa kijiji cha Ibwaga, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, anadaiwa kuuawa na mkulima mwenzake kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika ugomvi unaodaiwa kutokana na wivu wa mapenzi.

Tukio hilo lilitokea katika kijiji hicho kilichopo mkoani Dodoma lakini kutokana na umbali wa kituo cha polisi wilayani Kongwa, Kamanda Mbutu alisema liliripotiwa katika kituo cha polisi kilichopo karibu katika mji wa Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Alimtaja mkulima aliyeuawa kuwa ni Ndogo Mkivila (40) ambaye anaelezwa kuwa kabla ya kifo chake, alikuwa akifanya kibarua cha kulima katika shamba la Mfalme Mwinila, mkazi wa wilayani Kongwa wakiwa pamoja na mkulima mwenzake ambaye bado hajajulikana jina lake.

duru langu
12-29-2008, 03:12 AM
Huko Manyara/Arusha kuna kazi kweli kweli. Nakumbuka kwenye miaka ya mwanzoni
1980s kuna mwanamama aliyefikishwa kwa pilato kwa sababu ya kuuwa
bila kukusudia. Huyo mama alimpa mwanaye dozi ya gongo
ili mtoto alale usingizi mzito ili mama apate nafasi ya kuvinjari na njemba
lililo-impotiwa usiku huo :mad:

My more
12-29-2008, 03:38 AM
Huko Manyara/Arusha kuna kazi kweli kweli. Nakumbuka kwenye miaka ya mwanzoni
1980s kuna mwanamama aliyefikishwa kwa pilato kwa sababu ya kuuwa
bila kukusudia. Huyo mama alimpa mwanaye dozi ya gongo
ili mtoto alale usingizi mzito ili mama apate nafasi ya kuvinjari na njemba
lililo-impotiwa usiku huo :mad:

Duu hiyo nayo ilikuwa kali!!

duru langu
01-01-2009, 02:45 AM
Kali kwelix2

Max Shimba
09-01-2009, 09:08 PM
Sasa hako kadogo kamenza na umri huo, si itakuwa taaabu katapo kuwa la saba?

The Great Cardinal
09-03-2009, 04:21 PM
Ni vizuri kameanza mapema maana kakikuwa hakatapata shida ya kuwa na kiu au kufundishwa. Na pengine kanaweza kakaacha kabisa.

mkumeni
03-12-2011, 04:28 PM
:confused::confused::confused
Haya yanasimuliwa na Mroki kuwa yameonekana Coco Beach katika kusherehekea Xmass!

Huyu ni mzazi?

http://3.bp.blogspot.com/_mqjENGefutg/SVO034Qux4I/AAAAAAAABUE/rrMrMIeEtS0/s1600-h/Mama.JPG


Na huyu ni mtoto

http://2.bp.blogspot.com/_mqjENGefutg/SVO04Zvb0GI/AAAAAAAABUM/uUWGQUEWQjM/s400/Laga.JPG

wapi na wapi?