mwanakijiji
12-28-2008, 09:52 PM
Bakwata yataka mapumuziko mwaka mpya wa Kiislamu
Kuruthum Ahmed na Salim Said (mwananchi)
BARAZA Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) limepeleka maombi serikalini kutaka siku ya mwaka mpya wa Kiislaam iwe sikukuu ya kitaifa.
Sambamba na hilo Bakwata imeomba siku hiyo iwekwe katika kalenda ya serikali na iwe ya mapumziko na kufahamika katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Suleiman Gorogosi alisema maombi hayo walishayapeleka serikalini tangu mwaka jana.
"Maombi yetu tumeshayapeleka kwa serikali tangu mwaka jana kupitia kwa waziri mkuu aliyepita Edward Lowassa ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mwaka jana, tunachotaka ni kupata kibali cha kupata mapumziko ya sikukuu hiyo ili iwe kama sikukuu nyingine na kufahamika katika jamii,"alisema Sheikh Gorogosi.
Gorogosi alisema kuwa mwaka 1429 ambao (leo) jana ni tarehe 28/12 Hijjiria (sawa na Desemba 27 mwaka huu, hivyo wanatarajia kuingia mwaka mpya wa Kiislam 1430 ambayo Jumatatu Desemba 29, 2008.
"Kiislaam mwezi wa kwanza unajulikana kwa jina la Muharramu au Mfunguo nne kama tulivyozoea kwa tarehe Mosi ya mwezi huo ambayo itakuwa sawa na Januari Mosi, tutafanya maadhimisho hayo," alisema Sheikh Gorogosi.
Alisema maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika mkoani Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na mgeni rasmi katika shughuli hiyo atakuwa Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein.
Aliwataka, waislamu na wanazuoni wote nchini kukutana saa 8:00 katika Msikiti wa Al-Farouq uliopo Kinondoni, Bakwata Makao Makuu kujiunga na maandamano kuelekea Mnazi Mmoja kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Gorogosi alisema waislamu wanatakiwa kuifanya sherehe kwa ajili ya ibada na sio kwenda kwenye mambo ambayo hayampendezi Mungu.
"Tusherehekee sikukuu hii kwa kwenda kufanya ibada na sio kwenda kwenye kumbi za starehe, kwenda kwenye fukwe za bahari kwa kuvaa vitu visivyo kuwa na maadili ya kidini,"alisema Gorogosi.
Aliwataka Waislaam wote ambao wamefunga ndoa za bomani au mahakamani kuwa hazitambuliki katika Uislaam, hivyo akawataka kuzirekebisha na kuondokana na 'uzinzi' huo.
"Sisi binadamu tutawalaumu sana, lakini kwa Mwenyezi Mungu watakwenda kuulizwa na kuhukumiwa kwa zinaa waliyokuwa wakiifanya," alisema Sheikh Gorogosi.
Aliwataka Waislaam nchini kujiepusha na ndoa za namna hiyo au kuchukua kesi za ndoa kuzipeleka mahakamani kwa kuwa zinawachanganya mahakimu.
Wakati huo huo baraza hilo limepuuza malalamiko ya muda mrefu ya baadhi ya Waislaam kuwa wanakandamizwa na kubaguliwa katika sekta ya elimu na utawala kwa maelezo kuwa "hakuna Muislaam anayekandamizwa na wanaosema hivyo ni waongo".
Kwa miaka mingi Waislaam wamekuwa wakilalamika kuwa wanakandamizwa kwa kutoa hoja ya idadi ndogo ya wanafunzi wa Kiislaam wanaochaguliwa katika vyuo vikuu vya umma, kukatazwa kwa somo la maarifa ya Kiislaam katika baadhi ya shule za umma, kucheleweshwa na kunyimwa usajili kwa baadhi ya shule za Kiislaam.
Gorogosi alisema kuwa suala la elimu si suala la kukandamizwa bali ni suala la mtu kushughulika na kusoma kwa bidii.
"Elimu na ibada si suala la kukandamizwa ni la mtu binafsi kushughulika, hata Mtume Muhammad (S.A.W.) aliwambia wanae kuwa utume wake hautawasaidia kuwaepusha na adhabu ya Mwenyezi Mungu iwapo hawatamuabudu," alisema Sheikh Gorogosi.
Sheikh Gorogosi alisema kuna baadhi ya waislaam wamekuwa wakitoa lawama kuwa wananyanyaswa, kubaguliwa na kukandamizwa katika sekta ya elimu na utawala jambo ambalo alidai kuwa ni uongo.
"Kwa upande mmoja zamani ilikuwa kweli, lakini si kosa la mtu wala dini nyingine bali ni kosa la Waislaam wenyewe kwa kuwa awali walikataa kuwapeleka watoto wao shule kwa madai kuwa watakuwa makafiri na hivyo kuwafanya wenzetu watutangulie katika elimu," alisema Sheikh Gorogosi.
Alisema kutokana na maboresho mbalimbali yanayofanywa na serikali katika sekta hiyo, suala hilo kwa sasa halipo na kuwataka wanaotoa malalamiko hayo waache kwa kuwa si ya kweli.
Akifafanua kuhusu uamuzi wa kamisheni ya Kusimamia vyuo Vikuu (TCU) kutaka kujiingiza katika udahili wa wanafunzi jambo ambalo limepingwa na Waislaam nchini kwa madai kuwa uamuzi huo ni kwa lengo la kuwakandamiza, Gorogosi alisema hiyo ni dhana tu na halina ukweli.
Aidha, alifafanua kuwa, kwa upande wa utawala wanaolalamika hawana hoja kwa kuwa Waislaam wamewahi kushika nafasi za juu serikalini kuanzia urais hadi ngazi za chini.
"Ooh! hatuna nafasi kubwa serikalini wanachukuwa wakristo. Nafasi gani unayotaka wew? Rais Muislaam, makamu muislaam, Waziri wa Fedha muislaam, Mkuu wa Jeshi la Polisi Muislaam na hata Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Muislaam na wengine katika chama na wakuu wa mikoa.
Nafasi gani kubwa unayotaka zaidi ya urais na makamu wake?" alihoji Sheikh Gorogosi. Alieleza kuwa nafasi serikalini zinapatikana, lakini sio bure bali ni kwa kushughulika kutafuta elimu, kuwa mwaminifu na mkweli katika kazi.
"Ubaguzi hamna na wanaosema kuna ubaguzi wa kidini nchini katika utawala na elimu wanasema tu kwa sababu wamezoea kusema lakini hawana hoja," alituhumu Sheikh Gorogosi.