mwanakijiji
12-29-2008, 06:42 PM
Wizi wa kutisha wagundulika NDC
2008-12-29 13:31:15
Na Mwandishi Wetu
Ufisadi mkubwa umetokea katika benki ya Barclays London ambapo dola za Kimarekani milioni 1.5 zilizokuwa zitumike kwa ajili ya upembuzi wa miradi ya makaa ya mawe Mchuchuma na chuma Liganga, hazijulikani matumizi yake.
Kufuatia hali hiyo, Serikali imeliagiza Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), kuchunguza jinsi amana ya kiasi hicho cha fedha ambazo ni karibu sawa na Shilingi bilioni mbili zilizowekwa katika benki ya Barclays London, Uingereza zilivyotumika.
Ufisadi mwingine, uligundulika mapema mwaka huu, baada ya uchunguzi wa kampuni ya Ernst & Young kugundua kuwa zaidi ya Sh. bilioni 133 za Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zimechotwa na makampuni kadhaa kwa matumizi binafsi.
Baadhi ya watuhumiwa hao wa EPA tayari wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na menejimenti ya NDC jijini Dar es Salaam jana, maagizo hayo yanafuatia taarifa za ukaguzi wa ndani ya NDC.
Taarifa hiyo inaonyesha kuwa mnamo mwaka 2000, Shirika lilipata mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 1.5 kutoka Benki ya Barclays na kuziweka katika tawi la London, Uingereza.
``Fedha hiyo ilikuwa itumike kwa ajili ya upembuzi wa Miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma na chuma Liganga,`` ilisema taarifa hiyo.
Menejimenti hiyo ilisema nyaraka ambazo shirika limezipata zimebainisha kuwa fedha hiyo ilitumika mwaka 2002 kudhamini mkopo uliotolewa na Benki ya Investec Mauritius kwa kampuni moja ya Singapore iitwayo Uhuru Capital Management PTE Ltd.
``Kwa vile Bodi ya Shirika haijawahi kuruhusu dhamana hiyo, Serikali imeona ipo haja ya kuchunguza kwa kina matumizi ya fedha hiyo na iwapo umetokea uvunjaji wowote wa sheria, hatua mwafaka zichukuliwe haraka kwa watakaobainika kuhusika,`` ilisema.
Ilianisha kuwa uchunguzi huo unalenga katika kubaini walioidhinisha kutolewa kwa dhamana hiyo, kubaini wamiliki wa kampuni iliyodhaminiwa, kubaini uhusiano wa kampuni iliyodhaminiwa na NDC na kwamba uchunguzi utakapokamilika utawezesha mamlaka husika kuamua hatua zifaazo kuchukuliwa.
My Take:
Hivi kati ya 2000-2005 kulikuwa na viumbe gani kwenye serikali yetu?