PDA

View Full Version : Hivi Polisi wanajifunza mbinu za Upelelezi?

mwanakijiji
12-30-2008, 10:09 AM
Mama mbaroni kwa kutaka kumuuza mwanawe albino
? Bei yake ilikuwa milioni 15/-

na Julieth Mkireri, Pwani

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani limewakamata Mwajabu Said (66) na mama na mtoto wake, Said Omary (40), kwa tuhuma za kula njama za kutaka kumuuza binti wa mama huyo aliyetajwa kwa jina la Kabuyu Dalili (22), mwenye ulemavu wa ngozi (albino ) kwa sh milioni 15.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Absalom Mwakyoma, jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa, mama na mtoto wake wanadaiwa kula njama za kuandaa mpango huo na mtu ambaye aliahidi kuwalipa kiasi hicho cha fedha.

Alisema, uchunguzi wa polisi umebaini kuwa biashara hiyo ilipangwa kufanyika Desemba 26, siku moja baada ya Sikukuu ya Krismasi.

Kamanda huyo alisema binti huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kwamba anakusudia kuuzwa kwa kitita hicho cha fedha alikimbilia katika kituo cha polisi kwa ajili ya usalama wake.

Kwamba baada ya polisi kupewa taarifa hizo, walimtaka binti huyo kubaki kituoni hapo na wao walikwenda kijijini Fukayosi alikokuwa akiishi na kuwakamata watuhumiwa.

Alisema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kuwatia mbaroni wahusika waliotaka kumnunua albino huyo.

My Take:
Mbona naona kama ni Polisi walioboronga kuwakamata wahusika?

dRU
01-05-2009, 03:33 PM

Pole mwanakijiji elewa kwamba "Kumwashia taa kipofu ni kuharibu mafuta.":mad::mad:

mwanakijiji
01-05-2009, 04:55 PM
Pole mwanakijiji elewa kwamba "Kumwashia taa kipofu ni kuharibu mafuta.":mad::mad:

sasa tufanyeje wakati tunaona kipofu anaelekea shimoni; tumpige konzi?

Dua
01-08-2009, 02:09 AM
Hivi kile kituo cha Polisi ambacho huwa wanachukua mafunzo kina vifaa vya kutosha katika mafunzo yao? Au pesa yote inakwenda kwa wawekezaji na kuwapa peremende wahusika?

Mwanakijiji mafunzo lazima wanapata swala ni Je, yanaendana na wakati tulionao?

QUTE
01-08-2009, 02:49 AM
Hivi kile kituo cha Polisi ambacho huwa wanachukua mafunzo kina vifaa vya kutosha katika mafunzo yao? Au pesa yote inakwenda kwa wawekezaji na kuwapa peremende wahusika?

Huenda mafunzo wanapewa lakini wakishatoka depo wanawaachia maofisa mafunzo yao halafu wao wanaondoka na akili ya kuja kufanya biashara ya police. hapo walijua tayari wamepata dili na hivo walivosikia million tano wakachanganyikiwa

RITCHIEB
01-28-2009, 03:12 PM
Jamani nyinyi mnasumbuka na kuumiza vichwa bure kuhusu hawa askari POLISI wa Tanzania hawa sio Polisi ni POLISH kama ile dawa za kung.arishia kitu chochote kile kama viatu , Askari POLISI wetu sisi ni magwanda na kwa siku hizi hizo Defender zao ! POLISI AKIKUKAMATA ATAKUIBIA SIMU NA PESA ZAKO ! Polisi hajui maana ya upelezi ni nini au kwa makusudi kabisa huyo huyo Polisi ndio wa kwanza anakimbilia kuvuruga ushahidi (Rushwa) Mwanakijiji mbona hilo liko wazi majambazi ni jina tu , majambazi wenyewe ni hao hao POLISI ukienda kutoa taarifa POLISI basi ujue polisi hao hao wataambia wahusika kuwa ni fulani katoa siri wanachukua pesa yao uhasama na kuuawa wanakuachia wewe !
Kitu kiko very clear Hao POLISI walitakiwa waweke mtego trh 26/12/ yule Albino angeendelea na mambo yake wakati huo huo analindwa na askari waliovalia kiraia wangeacha biashara ifanyike then watu wangekamatwa na ushahidi , kwa jinsi walivyofanya sasa ni upuuzi mtupu Afande mwema uongozi mzuri lakini wanakuharibia darasa bado halijafika huku chini wengi wana njaa sana hwa askari wako wa Doria ni wezi mkuu