PDA

View Full Version : Ruhinda: The Man behind Mkapa?



mwanakijiji
12-30-2008, 06:14 PM
Jamani tunajua nini kuhusu huyu bwana na yale yaliyotokea Benki Kuu...

Dua
12-31-2008, 12:38 AM
Mwanakijiji labda umwage kidogo kwani Gilman alikuwa anakula wakati Ben alikuwa bado yuko NY tena wakati wa Mwalimu ingawa ilikuwa bado peremende njaa sasa Ben aliporudi huenda walikuwa pete na kidole.

dRU
01-05-2009, 02:44 PM
Jamani tunajua nini kuhusu huyu bwana na yale yaliyotokea Benki Kuu...
Mwanakijiji fafanua ni Ruhinda gani!! Maana yupo ambaye ni shwahiba mkubwa wa Mkapa huyu ni Balozi Ruhinda... Kampeni zote za Mkapa ndiye alikuwa msitari wa mbele na aliogopewa sana na hata mawaziri... Licha ya ubalozi ni mwandishi wa siku nyingi tuu...

lemunyake
01-05-2009, 03:28 PM
Balozi Ruhinda ndo alikiwa mmiliki wa Weekly ya Wiki HII ambayo baadaye ikazaa Mwananchi Communications. Lakini nasikia kauza hisa zake pale.

mwanakijiji
01-05-2009, 04:54 PM
Kuna mtandao ambao ulishughulikia wizi wa mabilioni 2005; watu hawa walikuwa na nafasi ya kujua kuhusu EPA, na walikuwa na nguvu ya kuweka watu wao na kufanikisha the biggest heist katika historia ya benki zetu. Ballali, Mkapa, Rostam, Ruhinda, Chande na Jeetu pamoja na Apson na wanawe bila ya shaka walikuwa katika nafasi fulani hivi ambayo naamini inabidi uchunguzi yakinifu kuweza kuelewa ilikuwaje.