PDA

View Full Version : Leo wamegungua menejimenti TRL bomu!



mwanakijiji
01-04-2009, 05:57 AM
Serikali: Menejimenti TRL wababaishaji

2009-01-03 11:59:07
Na Joseph Mwendapole (Nipashe)

Serikali imekiri kuwa kuna ubabaishaji unaofanywa na mwekezaji wa reli ya kati (TRL). Kampuni ya Rites ya India ina asilimia 51 ya hisa kwenye shirika hilo wakati serikali imebakia na asilimia 49.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema kuna mambo mengi kwenye mkataba ambayo hayajatekelezwa na mwekezaji huyo.

Alisema uwekezaji mkubwa ulioahidiwa na mwekezaji huyo wakati wa kusaini mkataba huo haujatekelezwa ipasavyo.

Dk. Kawambwa alisema serikali tayari imeunda kamati ambayo imepitia upya mkataba baina yake na mwekezaji huyo ili kuangalia makubaliano yanayokiukwa.

Alisema kamati hiyo imeainisha maeneo yenye mapungufu na kwamba itakuwa ikikaa na kuzungumza nao ili watekeleze mapungufu yanayojitokeza katika mkataba wao.

Dk. Kawambwa alisema walishakaa na mwekezaji huyo Novemba mwaka jana na kumweleza anachotakiwa kufanya na kwamba mwaka huu pia watamweleza mapungufu yake.

Alisema mwekezaji huyo aliahidi maboresho mengi ya usafiri huo wa reli ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya safari, lakini ameshindwa kufanya hivyo.

Waziri alisema ingawa serikali nayo inahisa kwenye TRL, lakini menejimenti ni ya Rites, na kwamba sasa watakaa pamoja kuangalia namna ya kugawana madaraka.

Alisema anaamini kuwa suala hilo litajadiliwa kwa busara ili hatimaye kufikia muafaka na kumaliza malalamiko ya mara kwa mara kwa kuweka Watanzania kwenye menejimenti hiyo.

Kuhusu serikali kuipa fedha za kujiendesha TRL, Waziri Kawambwa alisema inafanya hivyo kwa kuwa na yenyewe ni sehemu ya umiliki wa kampuni hiyo.

``Lazima tufahamu kuwa TRL si ya Rites peke yake, sisi tuna hisa asilimia 49 kwa hiyo kunapotokea matatizo na sisi tunahusika, ndiyo maana tunatoa fedha kuweka mambo sawa,`` alisema.

Mwishoni mwa mwaka jana serikali iliamua kubeba tena mzigo kuilipia Kampuni ya Reli nchini (TRL) mishahara ya Oktoba na Novemba kwa sababu kampuni hiyo ilishindwa kulipa mishahara hiyo kama ilivyokubaliana na serikali miezi michache iliyopita.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyasema hayo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mamuya kuhusu tatizo la malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa TRL.

Pamoja na kuahidi kulimaliza tatizo hilo, Pinda alisema lazima ifikie mahali kampuni hiyo iendelee kuwalipa wafanyakazi wake yenyewe.

Kati kati ya mwaka jana wafanyakazi wa (TRL) waliishauri serikali kuuangalia upya mkataba wa uendeshaji shirika hilo na serikali wakidai unaonyesha kufanana na ule wa Richmond. Kampuni ya Richmond ilipewa mkataba na serikali wa kufua umeme wa dharura wakati haikuwa na uwezo wa kazi hiyo.

Swali:
Nani aliyependekeza Rites Consortium wachukue TRL?