PDA

View Full Version : Mbatia naye vipi? tuwaachie mafisadi...



mwanakijiji
01-05-2009, 04:58 PM
Mbatia ataka mafisadi waachwe (Nipashe)

2009-01-05 14:24:34
Na Muhibu Said

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amewataka Watanzania kuachana na mtindo wa sasa wa kundi moja kulinyooshea kidole lingine kuhusu kashfa za ufisadi na kutumia madaraka vibaya akisema kwamba kitendo hicho kinaigawa nchi.

Sanjari na kuigawa nchi, Mbatia, ambaye muda wa uongozi wake katika chama hicho ulifikia tamati jana, aliuambia Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa chama hicho kuwa kitendo hicho pia kinakwamisha uzalishaji kwa vile hakuna aliyemsafi katika kashfa hiyo tangu enzi za utawala wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Badala yake, amewataka Watanzania wakae chini na kujadiliana kuhusiana na suala la ubinafsishaji, ambalo alisema ndio chanzo kikubwa cha kuibuka kwa kashfa hiyo.

Mbatia alisema hayo alipokuwa akitoa nasaha katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa chama hicho, uliofanyika katika ukumbi wa kituo cha Msimbazi, jijini Dar es Salaam.

Alisema suala la kutumia madaraka vibaya, ni la muda mrefu kwa Watanzania nchini na kwamba hakuna asiyeguswa kwa namna yo yote na kashfa hiyo.

``Kwa mfano, jana (juzi) alikuja mtu ofisini kwangu kutoka Mtwara, akaniambia kuwa usikanyage Mtwara na hoja yako ya kutaka Mkapa aondolewe kinga ili ashtakiwe, akaniambia kama unataka Mkapa aondolewe kinga, basi aondolewe na Mzee Mwinyi pia, kwa kubariki ubadhirifu wa IPTL (mradi wa kuzalisha umeme) wakati wa utawala wake.

Hata leo Nyerere akifufuka ataambiwa alitumia madaraka yake vibaya, hivyo naye ashtakiwe. Kila mtu anamnyooshea mwingine kidole,`` alisema Mbatia.

Alisema nchi hivi sasa imefikia pabaya, ambapo Watanzania wameanza kuitana mafisadi, baada ya kuacha kuitana ndugu na mheshimiwa, kama walivyokuwa wakifanya hivyo huko nyuma.

``Tumetoka kwenye kuitana ndugu, tukaenda kwenye kuitana mheshimiwa sasa tumekwenda kwenye kuitana mafisadi.

Kama hujatoa kibanzi katika jicho lako, ona boriti la jicho lako,`` alisema Mbatia, ambaye kauli zake zilionekana kupingana na juhudi za makundi mbalimbali ya jamii nchini kupinga vitendo vya ufisadi.

Alisema amesikitishwa na gazeti moja nchini, ambalo lilimkariri wakati akiwa masomoni nje ya nchi akishauri Rais Mstaafu Benjamin Mkapa aondolewe kinga ili ashtakiwe mahakamani kwa tuhuma za ufisadi zinazomkabili, wakati hakuwahi kusema kitu kama hicho.

``Naviomba vyombo vya habari vinitendee haki,`` alisema Mbatia akimaanisha kuwa haungi mkono hoja zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa Mkapa anapaswa kushitakiwa kutokana na kutumia vibaya madaraka yake katika mchakato wa ubinafsishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.

Mkapa na wenzake wanadaiwa kujimilikisha hisa asilimia 80 kupitia Kampuni ya Tan Power Resources Limited kwa Sh. milioni 700 badala ya thamani halisi Sh. bilioni nne. Pia wanadaiwa kulipa Sh. milioni 70 tu.

Kutokana na hali hiyo, Mbatia, aliyekuwa akigombea uenyekiti wa chama hicho, aliwataka Watanzania kutoa hoja zenye kujenga ustawi kwao badala ya kuendelea na mjadala unaozua mgogoro miongoni mwao, ambao alidai kuwa unaigawa nchi na kukwamisha uzalishaji.
``Hakuna uzalishaji, ni mjadala tu wa mgogoro,? alisema Mbatia.

Naye Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu huo, alivitaka vyama vya siasa kutekeleza yale wanayosema.
``Ninavitaka vyama vya siasa, wazingatie wanayosema.

Wamekuwa wakisema kuwe na mshikamano na tuwe na utaifa. Watekeleze kwa vitendo. Siyo baada ya hapo kila chama kinafuata yake,`` alisema Tendwa.

Pia, alisisitiza mahitaji ya mabadiliko ya sheria ya ruzuku na kuvitaka vyama vya siasa kuwafikia wananchi na pia serikali ibadilike na kudhibiti rushwa katika vyama vya siasa.

Wazo:
Kimemkuta nini Mbatia?

Ach-F
01-06-2009, 01:51 AM
Mbatia na kundi lake ndio wanaofaidika na pesa ya walipa kodi kwa kutanua bila kufanya kazi yoyote, hivyo Ufisadi ukiisha watakula wapi? Ni wajibu wao kuona hii vita haifanikiwi. NCCR mwelekeo umekwisha ni kusubiri hizo pesa za ufisadi hadi kiama chao futi 6.

mwanakijiji
01-06-2009, 06:01 PM
sasa ona haya:

Mbatia remarks on corruption provoke storm (Guardian)

2009-01-06 11:41:30
By Correspondent Felister Peter


Politicians have challenged a statement given by NCCR-Mageuzi Chairman James Mbatia on people suspected of corruption, with MP Anne Kilango saying Mbatia is now speaking like a priest.

Mbatia was quoted on Sunday as saying that public leaders who are currently facing charges of abuse of office, tax exemption and occasionally loss to the government should be freed because there is no single honest and clean person in Tanzania.

The Member of Parliament for Same East Ane-Kilango Malecela told ‘The Guardian’ in a telephone interview yesterday that with all the efforts that President Jakaya Kikwete has made to fight corruption, there was no way someone could emerge and demand that people accused of corruption should be freed.

She said that Mbatia had to make his statement clear and manifest his stance on whether he supported or fought corruption so that he could be challenged.

``I don`t understand what Mbatia is talking about because everyone has his own capacity of thinking and analysing issues.

I want to exactly know whether he is supporting or fighting corruption``, said Kilango.

Dr Wilbroad Slaa, Member of Parliament for Karatu, said he has been shocked by Mbatia`s statement and that his argument could not change the attitude of other people.

He said if Mbatia was coward, then he did not have the confidence to fight corruption. ``He better stays away and leaves other people who are committed to continue with the struggle.``

Dr Slaa said Mbatia\'s statement would not demoralise them as they would continue fighting for the country`s resources not to be exploited by few people.

``If Mbatia is not clean, then it is okay. He should not try to convince other people to believe that all Tanzanians are corrupt,`` he said.

The Member of Parliament -Bariadi East, John Cheyo said there was no way dishonest people should be left free. Any person who commits an offence must face the law, Cheyo said.

Mbatia was quoted yesterday saying there is no honest person in this country and so he doesn`t see the reason why few people should be taken to court.

He said if properly investigated, every one would be found with faults. He said Tanzanians must now think of privatisation which is the main source of all the current problems.

He went further saying that if it was a matter of taking to court every corrupt person, then former presidents Ali Hassan Mwinyi and Benjamin Mkapa should be charged because there were so many corrupt incidences during their reigns.

Mbatia was also quoted as saying that if Mwalimu Julius Nyerere was still alive, once investigated, he would also have been found with corruption scandals.

More than 20 people have also been arraigned in court allegedly for stealing from the Bank of Tanzania`s External Payment Arrears (EPA) account.