PDA

View Full Version : Mahakimu wastaafu kuajiriwa tena..



mwanakijiji
11-07-2008, 06:40 PM
Mahakimu wastaafu kurejeshwa kazini kukabili upungufu

Na Habel Chidawali, Dodoma (Mwananchi)

SERIKALI imesema imejipanga kuwaajiri kwa wingi mahakimu wa mahakama za mwanzo na kuwatafuta wale waliostaafu ambao bado wanaonekana kuwa na nguvu ili waweze kuajiriwa kwa mkataba maalumu ili kukabiliana na upungufu mkubwa wa mahakimu nchini.

Mwanansheria Mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika aliyasema hayo jana bunge wakati akijibu swali lililoelekezwa katika wizara ya katiba na sheria ambapo muuliza swali alihoji juu ya mikakati iliyowekwa na serikali katika kuondoa kero hiyo.

Mbunge wa Mfenesini Mossy Mussa (CCM) alitaka kujua kuhusu mikakati ya serikali juu ya upatikanaji wa mahakimu nchini kutokana na ukweli kuwa wananchi wengi wamekuwa wakikosa haki zao za msingi tatizo linalosababishwa na upungufu wa mahakimu.

Mussa alisema kuwa imedhihirika wazi kuwa kuna upungufu mkubwa wa kada hiyo ya watenda haki katika sheria jambo linalofanya haki za watu kupotea bure bila ya za kujua ni wapi watazipata tena kwa wakati.

Awali pia Mwanasheria huyo alisema serikali inaangalia uwezekano wa kuongeza udhamini kwa mahakimu wanaosoma katika chuo cha Lushoto ili iwe ni rahisi kuwaajili kwani alisema kuwa wale wanaojidhamini wenyewe huwa ni kazi sana katika kuwalazimisha kupata ajira.

Alisema kuwa serikali ina mpango wa kuboresha mahakama zake na kisha kuwaajiri wahitimu wa stashahada kutoka chuo cha Lushoto hasa wale wanaojisomesha na wanaomaliza katika vyuo vingine hapa nchini ambao wataonekana kuwa na sifa.

Jambo lingine mwanansheria huyo alisema kuwa serikali inaangalia uwezekano wa kuongeza udhamini wa serikali kwa wanafunzi wa sheria ili watakapomaliza iwe ni rahisi kuajiriwa moja kwa moja na mahakama kuliko ilivyo hivi sasa ambapo wale wanaojisomesha hawalazimishwi kuajiriwa na mahakama.

Alisema kuwa serikali itaendelea kuajiri mahakimu wakazi kulingana na mahitaji kwa kuwa kada ya mahakimu wa wilaya haipo tena katika muundo wa utumishi hivyo akasema kuwa serikali inapeleka mahakimu wa wakazi katika ngazi ya wilaya.

Kuhusu mawakili wanaosomeshwa na serikali na kisha kukimbia kufanya kazi serikali na badala yake kuamua kujiajiri, mwanansheria huyo alisema kuwa tatizo hilo linatokana na mishahara na marupurupu kidogo wanayopata serikalini kuwa hayakidhi haja ikiwemo mazingira magumu wanakoapngiwa kufanya kazi.

Hata hivyo alikiri kuwa kuwa kuna upungufu mkubwa wa mahakimu nchini unaosababisha hakimu mmoja kuhudumia zaidi ya mahakama moja na hivyo kusababisha baadhi ya watu kutopata haki yao ipasavyo.