PDA

View Full Version : Kupunguza msongamano wa usafiri Dar: Pendekezo



mwanakijiji
01-05-2009, 07:46 PM
Mojawapo ya mapungufu makubwa ya tawala za nchi yetu ni kutokuweza kusoma nyakati. Jiji la Dar-es-Salaam lilitakiwa liwe na miundo mbinu ya kutosha kuweza kusafirisha na kuhudumia wakati wake wanaoelekea kufika milioni 4 muda si mrefu ujayo.

Habari zilizoripotiwa kwenye gazeti moja leo (http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2009/01/05/129184.html) kuwa serikali imetenga Tsh bilioni 20 kufanyia mabadiliko na matengenezo barabara kadhaa za Dar zenye jumla ya urefu wa kilimoita 85 ni za kusikitisha. Inaonesha ni jinsi gani serikali haijanuia na kukusudia kwa dhati kupunguza msongamano wa usafiri jijini Dar.

Bila ya kuingia mradi wa makusudi, mkubwa na wa haraka wa kujenga barabara kubwa mpya jijini Dar, bado matengenezo haya hayawezi kupunguza msongamano wa usafiri zaidi ya kuongeza mahali pa kusongamana.

Naamini,

a. jiji la Dar linahitaji barabara za magari yaendayo kasi (express way) ambapo magari hayasimami (hakuna exit hadi kila baada ya kama kilomita kumi hivi) kuliko sasa ambapo kuna njia za kutokea kila urefu wa karibu mita chache.

b. Jiji la Dar linahitaji ongezeko la haraka la taa za kuongezea magari ambapo makutano yote katikati ya jiji na ndani ya mduara wa kilimoita 15 za jiji yanakuwa na taa za kuongezea magari.

c. Picha hizi mbili zinaonesha mgawanyo wa barabara uliopo sasa (picha ya rangi ya njano) na jinsi ambavyo ningefikiria ujenzi wa express ways.

http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/darroads.bmp

na picha ya pili:

http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/darroads2.jpg

d. Ipo haja ya ya haraka ya kusambaza shughuli za kibiashara kwa mkoa mwingine zaidi ya Dar. Mji kama wa Tanga ni mji ambao unaweza kabisa kuchukua nafasi kubwa ya Dar kwani miundo mbinu yako bado ina uwezo mkubwa wa kuchukua watu wengi sana. Kwa upande wa kati, Dodoma bado libakia kuwa chagua zuri la kupunguza shughuli za kiserikali zinazofanyika Dar. Dodoma inaweza kumeza watendaji na wafanyakazi wengi wa serikali walioko Dar; hakuna sababu ya msingi kwa nini bado serikali inafanya kazi toka Dar.


Swali:

Unafikiri ni kwa jinsi gani majiji yetu yanaweza kupunguza msongamano wa magari (kama Dar) na kujiandaa kwa msongamano kwa kadiri nchi inaendelea na uchumi unakua?

zhukovski, Odessa
01-07-2009, 03:21 PM
Mimi naona mipango ya kupunguza msongamano wa usafiri Dar ndio uwezo wa serikali yetu. Kama tungelikuwa na uwezo mbona hata ma-fly overs tungekuwa nayo? Angalia jiji la Nairobi, idadi tuu ya taa za kuongozea magari ni nyingi sana kuliko Dar! wanazo fly overs katika baadhi ya barabara kuu. Kujenga express way inayozunguka jiji ni gharama sana na ni mradi wa "long term". Hata hivyo huu mpango wa kujenga baadhi ya feeder roads kama ile ya Ubungo Maziwa kupitia Kigogo sio wazo baya. Hata ile ya Mbezi Beach hadi Mbezi mwisho/Morogoro Road ni mpango mzuri sana.

mwanakijiji
01-07-2009, 06:26 PM
Nadhani, kama Taifa lazima tuwe tayari kulipa gharama ya maendeleo!

Ach-F
01-11-2009, 01:02 AM
Kupamga ni kuchagua. kwa sababu Dodoma ndio makao makuu shughuli nyingi zihamishiwe kule. Ofisi nyingi za kitaifa ziondoke Dar. Huwezi kuendelea na uozo wa Dar kuanzia usafiri na kuwa kituo kikuu cha mafisadi. Katika karne hii ya techologia unaweza kuweka kwa mfano TRA mkoa wowote ule. Nairobi sio mfano mzuri.

hhm
05-03-2010, 01:10 PM
Mimi naona mipango ya kupunguza msongamano wa usafiri Dar ndio uwezo wa serikali yetu. Kama tungelikuwa na uwezo mbona hata ma-fly overs tungekuwa nayo? Angalia jiji la Nairobi, idadi tuu ya taa za kuongozea magari ni nyingi sana kuliko Dar! wanazo fly overs katika baadhi ya barabara kuu. Kujenga express way inayozunguka jiji ni gharama sana na ni mradi wa "long term". Hata hivyo huu mpango wa kujenga baadhi ya feeder roads kama ile ya Ubungo Maziwa kupitia Kigogo sio wazo baya. Hata ile ya Mbezi Beach hadi Mbezi mwisho/Morogoro Road ni mpango mzuri sana.

Ndugu yangu Upo wapi?????....Hivi tujiulize jamani Juzi tuu Chama Tawala CCM kimetuhakikishia kuwa kina uwezo wa ku-raise 40Billions kwa Muda wa miezi hii michache kwa lengo la kufanyia Campaign pesa hizo na Wanaharakati hawa walitueleza mbinu mbali mbali watakazozitumia kupata fedha hizo ...Kumbuka mbinu zote walizotupa jinsi yakupata pesa hizo ni kutoka ndani ya mifuko ya wananchi ......nilijiuliza sana kama CCM ina watu wabunifu kiasi hiki kwanini kama Chama kilichoshika na kuongoza nchi kwa muda wa miaka karibu hamsini sasa wasilete wazo lifananalo na hilo kwa wananchi wa Dar es salamu na Tanzania kwa ujumla kwa kauli mbiu TUJENGE FLY OVERS na SPEED WAYS????... Hii inaonyesha kuwa kodi tunazokatwa wafanyakazi zinatosha kabisa kufanya hayo yote na ndiyo sababu serikali hiyo haiwezi kuja tena kuomba pesa kwa wananchi kwa style hiyo!!!!!...Sana sana tunapata Machungu tu kila kukicha.....mara ooh Tirion ngapi sijui zimepotea kinyemela mara Epa nyingine hiyo Mara mkataba feki....Dah!! Jamani