mwanakijiji
01-06-2009, 09:20 AM
USHIRIKIANO WA UPINZANI UMEKUFA – Dr. Slaa
Mwandishi Wetu
Uliokuwa ushirika wa vyama vya upinzani vya TLP, CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi umekufa tangu wakati wa uchaguzi mdogo wa Tarime. Hilo ni kwa mujibu wa Dr. Wilbroad Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipozungumza na tovuti yetu ya mwanakijiji.com hapo jana siku ya Jumatatu.
Katika mahojiano hayo marefu ambayo yalizungumzia kwa undani kile kilichotokea Mbeya hadi kusababisha Chadema kukosa mgombea kwenye uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini Dr. Slaa alizungumzia pia masuala ya kufikishwa watuhumiwa ufisadi mahakamani, uchaguzi wa Chadema, na masuala mengine ya kitaifa.
Akijibu swali kwanini Chadema baada ya mgombea wao kuenguliwa huko Mbeya Vijijini isimuunge mkono mgombea yeyote wa upinzani Dr. Slaa alisema kuwa ushirikiano unaohusisha vyama vyenye unafiki hauwezekani. “Sisi tutashirikiana na watu wasio wanafiki, wa wazi na ambao tunaaminiana” alisema Dr. Slaa katika mahojiano hayo ambayo yataandikwa kwa kirefu kwenye gazeti la Raia Mwema kesho siku ya Jumatano.
“Mmojawapo wa watu waliotuwekea pingamizi kule Mbeya vijijini ni CUF watu tuliokuwa na ushirikiano nao, sasa tutaweza vipi kuwaunga mkono watu tusioaminiana nao?” alihoji Dr. Slaa katika mahojiano marefu ya kufungulia mwaka kufanywa na KLHN.
Hata hivyo Dr. Slaa amesema kuwa huko mbeleni Chadema itashirikiana na vyama vingine kimkakati tu akiashiria kwamba ule uhusiano wa karibu kati ya vyama hivyo vikubwa vya upinzani umefikia tamati kama ilivyokuwa ikihofiwa na wachunguzi wengi wa kisiasa nchini.
Tamko hilo la Chadema limekuja masaa machache baada ya gazeti moja kuripoti kuwa chama cha CUF kimewakebehi Chadema kwa kuvurunda mchakato wa uapishwaji mgombea wao kwani “hata mama Ntilie wa SAU aliweza kufuata taratibu iweje chama chenye uzoefu kama Chadema”.
Mahojiano hayo na Dr. Slaa yataweza kusikika kwenye tovuti yetu ya mwanakijiji.com kuanzia mapema kesho (Jumatano)