View Full Version : Mashindano ya Urembo kila siku?
mwanakijiji
11-07-2008, 09:47 PM
Yawezekana kabisa kuwa Tanzania ndiyo nchi yenye mashindano mengi zaidi ya "umodo" kuliko nchi nyingine duniani. Yaani kuna mashindano ya kila aina na hata pale ambapo hakuna basi kuna mtu anafikiria jinsi ya kuanzisha.
Mabinti zetu wanakuwa bombarded na haya mambo ya umodo kana kwamba umodo kweli unalipa. Ukiondoa ushindi wa magari na nyumba ni kwa kiasi gani wale "MaMiss" wanafanikiwa katika fani ya "umodo"?
Tusipoangalia tutajikuta tumejaza ma "modo" wenye madoido lakini hawana lolote la kuelezea hiyo "fani yao".
Napinga kweli kuenea na kuenezwa kwa mashindano haya ya urembo, isije kutoka mwisho ndani ya familia kunaanza kuwa na mashindano ya urembo!
Napinga kweli kuenea na kuenezwa kwa mashindano haya ya urembo, isije kutoka mwisho ndani ya familia kunaanza kuwa na mashindano ya urembo![/B]
Mzee umekuwa mkali kweli, Nakuelewa una maana gani... Hata hivyo naomba simile kidogo maana sijui itakuwaje hapa chakula ya watoto. Si unajua tena fani?? Natamani kukuunga mkono ila mmmhhh naona inakuwa ngumu:mad::mad:
Mpenda amani
11-10-2008, 01:32 AM
Nakuunga mkono Mkjj, kwakweli imefikia wakati sasa imekuwa too much. Urembo umegeuka biashara kuu sikuhizi bila kuangalia madhara yake kwa jamii, Mabinti hawasomi, au kuwa na moyo wa kujiendeleza hasa pale akishajiona ameanza kurefuka refuka kidogo tu anajua ahh kusoma kitu gani bwana miss nahii mbona ipo. Ningeshauri mamlaka husika watupie macho hii kitu vinginevyo huko tunakoelekea wala siko.
mwanakijiji
11-10-2008, 07:15 AM
Napinga kweli kuenea na kuenezwa kwa mashindano haya ya urembo, isije kutoka mwisho ndani ya familia kunaanza kuwa na mashindano ya urembo![/B]
Mzee umekuwa mkali kweli, Nakuelewa una maana gani... Hata hivyo naomba simile kidogo maana sijui itakuwaje hapa chakula ya watoto. Si unajua tena fani?? Natamani kukuunga mkono ila mmmhhh naona inakuwa ngumu:mad::mad:
Kepa, siyo kwamba napinga mashindano yote ya urembo lakini kwangu ni jinsi gani hasa yanafanywa.
Kwa mfano kungekuwa na "Miss Scientist" ambaye ni binti mrembo lakini amebobea katika sayansi pia! Kama hilo haliwezekani basi hata viwango vya "Umiss" viinuliwe na kuhakikisha kuwa ma Miss wote ni lazima wawe na elimu ya Chuo Kikuu au wako tayari Chuo Kikuu au Chuo cha elimu ya juu. KUsiwe na ma Model wa kidato cha nne au cha sita tu.
My more
11-30-2008, 12:57 AM

Wenyewe wanadai eti mtu akienda shule sana. (akiwa na kichwa) anafikiri sana na hivyo hata kama mdogo uso unakomaa. Hapo maswala ya urembo inakuwa not reachable kidogo:):)
Sijawahi kufanya hako kautafiti, labda sio kweli.
duru langu
11-30-2008, 02:14 AM
Mimi naona haya mashindano ya "umodo" ni nyavu tuu za
kuwanasa warembo. Si unajua tena sikuizi ukiitwa "selebreti"
jamaa wanamiminika kukufuata na "kukuombaa"!
magoma
12-02-2008, 07:00 PM
Mamlaka husika iangalie kwa umakini swala hili, maana naona kama umekuwa ugonjwa flani kwa watoto wa kike wembamba, maana hata kutilia maanani masomo hakuna tena na hawa wazazi wao sijui kama wanafikiria mara mbili, naona kama wana utindio wa fikra na macho
My more
12-12-2008, 06:25 PM
Mzee umekuwa mkali kweli, Nakuelewa una maana gani... Hata hivyo naomba simile kidogo maana sijui itakuwaje hapa chakula ya watoto. Si unajua tena fani?? Natamani kukuunga mkono ila mmmhhh naona inakuwa ngumu:mad::mad:
Hii ya Kepa nilikuwa sijaiona:)
MAHESABU
09-22-2010, 10:31 PM
watu walipiga kelele mashindano haya yaruhusiwe yakaruhusiwa.....sasa wanahamia UKAHABA uruhusiwe(nna mashaka kama si hawa hawa ) baadaye watataka USHOGA URUHUSIWE....na watapitiliza NDOA NA WANYAMA IRUHUSIWE.......! AM PROUD TO BE BLACK......WITH HUMAN DIGNITY.....AND MENTAL CAPABILITY....ambapo naweza pembua baya na zuri
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.