PDA

View Full Version : Janeti na Sofia - Wote wawili hawakustahili!



mwanakijiji
01-08-2009, 08:41 AM
Mmoja wa hawa atatangazwa mshindi (dalili zinaonesha ni Sofia; usishange Kahama akiibua upset ya mwaka). Lakini kwa kuangalia tangu mwanzo wa mchakato wa kugombea kiti cha Uenyekiti wa UW-CCM hawa kina mama wawili wamejiabisha; wameibisha majina yao, na wamewaibisha wanawake wa CCM na kwa urefu wake wanawake wa Tanzania.

Kiu yao ya madaraka na mbinu walizotumia kufika walipofika ningekuwa nina uwezo ningewatimua na kuwatupa kwenye kisiwa cha waliosahauliwa!

Lakini kwa vile CCM imewataka na kuwapa nafasi; basi ni CCM inayowastahili na siyo Taifa letu kwani ni fedheha kuwa na Waziri anayesimamia usalama wa Taifa kufanya mambo aliyoyafanya! Nitafafanua kwa uzito siku ya Ijumaa baada ya kumjua mshindi!

Ach-F
01-08-2009, 09:58 AM
Chama kilichooza hakiwezi kuwa kisafi kitaendelea kuoza tu. Ngoja tusubiri tai waanze kula uozo.

mwanakijiji
01-08-2009, 05:54 PM
Sophia ashinda!

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. Sophia Simba ndiye mwenyekiti mpya wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania. Bi. Simba amewashindwa wapinzani wake kwa kupata kura 470 ambayo ni sawa na asilimia ya 54.5 ya kura zote zilizopigwa. Mshindani wake mkubwa Bi. Janeti Kahama (MB-Viti Maalum) amepata 383 sawa na asilimia 44.4 na Bi. Joyce Masunga amepata kura 10 sawa na asilimia 1.1 ya kura 872. (Taarifa kamili yaja)
Ukumbi wa Mkutano ulilipuka kwa furaha baada ya Mhe. Simba kutangazwa mshindi huku muziki wa taarabu ukirindima kukoleza furaha ya ushindi huo. Ngoma za watu wa mwambao ikiwemo segere zilisindikiza tangazo hilo la ushindi. Wimbo ulioonekana kuzikosha nyoyo za wajumbe zaidi ni pamoja na ule wa "Msumari umechoma kotekote". Ushindi wa Bi. Simba umekuja baada ya mchakato uliojaa vijembe, malumbano, na tuhuma za kila aina na ambao kwa watu wengine ulionekana kutishia hatima ya jumuiya hiyo hasa katika suala la uongozi wake.

Ka "nzi" ka KLHN ambako kalikuwemo ndani ya mkutano huo wa uchaguzi na hivyo kutupasha kwa uhakika kanadokeza kuwa hata kabla ya kupigwa kura wapambe wa Bi. Sophia walionekana kuwa na uhakika wa matokeo ya ushindi wakiamini kuwa mgombea wao ndiye anakubalika zaidi hasa na viongozi wa Taifa akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

"Unajua Bi.Sophia ndiye Waziri anashughulikia utawala bora, na utawala bora umeonekana ukifanya kazi katika masuala ya mafisadi hivyo ni wazi aliingia kwenye kinyang'anyiro hicho akiwa na ujiko mkubwa" amesema mjumbe mmoja kutoka mojawapo ya mikoa ya pwani na ambaye alikuwa karibu na kampeni ya Bi. Simba.

Akizungumza na tovuti hii kwa masharti ya kutotajwa jina lake kwani siyo msemaji wa UW-CCM, mjumbe huyo amesema kuwa Bi. Sophia asingeweza kushindwa uchaguzi huo ukizingatia nafasi yake.

"Kwanza yeye ni Mbunge wa kuteuliwa na Rais, na hivyo hajapigiwa kura mahali popote wakati wenzake Janeti na Joyce ni Wabunge wa Viti Maalum ambao nafasi zao zinatokana na mfumo wa uchaguzi ndani ya Chama." Amefafanua mjumbe huyo aliyezungumza kwa kujiamini.

"Pili, akiwa mbunge wa kuteuliwa na Rais amepewa Uwaziri wa Wizara nyeti nchini inayosimamia pia taasisi muhimu kama TAKUKURU na Usalama wa Taifa, hivyo anapoingia kwenye kinyang'anyiro ni vigumu kumuona kama mgombea mwingine," Amesema mjumbe huyo.

Naye mjumbe mwingine toka Songea ambaye alikuwa kambi ya Bi. Kahama ameonesha kusikitishwa na mchakato mzima wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa TAifa akidai kuwa kilichotokea ni "Aibu". Alipobanwa na mwandishi wetu afafanue kwa nini anatumia neno hilo moja kuelezea kilichojiri Dodoma, mjumbe huyo amesema kuwa "Huwezi kuwa na wagombea watatu ambapo mmoja wao anapigiwa debe na Rais wa nchi".

Akifafanua zaidi mjumbe huyo amehoji mambo kadhaa. "Kwanza, pale Sophia Simba alipopitishwa kugombea Uenyekiti ingempasa amuombe Rais kupumzika kwa muda shughuli za Uwaziri wake na hivyo kutokuwa na access na vyombo nyeti kama TAKUKURU na Usalama wa Taifa". Kwa maelezo ya mjumbe huyo tuhuma za rushwa katika uchaguzi huo zisingeweza kuchunguzwa kwa uhuru zaidi wakati mmoja wa mawaziri wenye nguvu sana ni mmoja wa wagombea. "Pili" aliendelea mjumbe huyo, "Wakati Rais anatangaza vigezo vya nani achaguliwe, alitangaza kuwa mojawapo ni kuwa 'msomi', sasa ukiangalia kati ya wagombea wote hao ni Bi. Sophia ndiye anaonekana msomi zaidi.".

Pamoja na hayo inaonekana kwa namna au nyingine "damu mbaya" kati ya wagombea wakubwa wawili (Bi. Kahama na Simba) yaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi licha ya baadhi ya wapambe wao kuonekana wakiserebuka pamoja. Kwa mujibu wa watu mbalimbali wanasubiri kuona ni jinsi gani Bi. Simba ataiongoza jumuiya hiyo na hivyo kujijengea imani kwa karibu nusu ya wajumbe ambao walionekana kumuunga mkono Bi. Kahama.

"Hapa bwana kuna dalili za kambi hizi mbili kuendelea hadi 2010" amesikika mjumbe mmoja.

Sasa hivi wajumbe na viongozi mbalimbali wanaendelea kutoa shukrani zao na pongezi pamoja na nasaha katika kuelekea kuhitimisha mkutano huo.

hofstede
01-09-2009, 06:38 PM
Hii ndiyo Tanzania yetu. Kwa staili hii ni ufisadi ndiyo unaonekana kushinda. Kwa nini mtu anunue uongozi kama "share" vile ni lazima anataji gawio ambalo ni ufujaji na rushwa. nafasi za uobgozi zinageuza investments Tanzania, hii ni aibu kubwa

mwanakijiji
01-09-2009, 07:36 PM
Hii ndiyo Tanzania yetu. Kwa staili hii ni ufisadi ndiyo unaonekana kushinda. Kwa nini mtu anunue uongozi kama "share" vile ni lazima anataji gawio ambalo ni ufujaji na rushwa. nafasi za uobgozi zinageuza investments Tanzania, hii ni aibu kubwa

swali kubwa ni kwanini wanautaka uongozi kwa nguvu zao zote?

Ndahani
01-10-2009, 12:01 AM
Nahisi ni kendeleza hoja za makundi...kila kundi linataka kulinda interest zake

mwanakijiji
01-10-2009, 12:17 AM
Ndahani tatizo linakuja ni katika kufahamu hizo "interests" zao hasa ni nini? Mimi nimejiuliza, kwanini wamejitahidi sana kugombania hii nafasi?

duru langu
01-10-2009, 02:44 AM
Ndahani tatizo linakuja ni katika kufahamu hizo "interests" zao hasa ni nini? Mimi nimejiuliza, kwanini wamejitahidi sana kugombania hii nafasi?

Aidha hao waliowasaidia/waunga mkono (kwani mapesa yaliyomwagwa hayawezekani ni yao peke yao) wana interest gani?

dude
01-11-2009, 09:44 PM
hapa kikubwa ni makundi tu hakuna jingine,kama ulichunguza kikwete alikuwa hana mtu katika waliongombea uvv-ccm na ndio maana akaamua mtu wa zanzibar achukue uongozi,ukija kwenye uwt sophia ndo aliyekuwa kwenye mtandao wa kikwete hilo halina ubishi na ndio maana ni waziri kwahiyo anachofanya kikwete ni kuhakikisha kila sehemu anaweka mtu wake ili kusiwe na wa kumpindua

mwanakijiji
01-11-2009, 10:02 PM
hapa kikubwa ni makundi tu hakuna jingine,kama ulichunguza kikwete alikuwa hana mtu katika waliongombea uvv-ccm na ndio maana akaamua mtu wa zanzibar achukue uongozi,ukija kwenye uwt sophia ndo aliyekuwa kwenye mtandao wa kikwete hilo halina ubishi na ndio maana ni waziri kwahiyo anachofanya kikwete ni kuhakikisha kila sehemu anaweka mtu wake ili kusiwe na wa kumpindua

Najaribu kuona kama tutaweza kuwapata wote wawili kwenye mtandao... kwa ajili ya toleo la Cheche wiki hii.