mwanakijiji
01-09-2009, 04:50 PM
JK aitaka Israel isimamishe mashambulizi Gaza
na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete ameitaka Serikali ya Israel kusitisha haraka matumizi ya nguvu za kijeshi kwenye Ukanda wa Gaza na badala yake itumie njia ya kidiplomasia ili kutafuta ufumbuzi wa amani na Palestina.
Kwa mujibu taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa vyombo vya habari jana, ilisema wito huo aliutoa juzi alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na Balozi wa Palestina, Dk. Nasri Khalli Abu Jaish na Balozi wa Israel nchini, Jacob Kdeidar.
Katika mazungumzo hayo Rais Kikwete aliwaeleza kuwa Tanzania inasikitishwa na machafuko yanayoendelea Palestina, ambako Jumanne wiki hii walishambulia moja ya shule 23 za Umoja wa Mataifa na kuua Wapalestina 50 huku wakiwajeruhi 100.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa kutokana na mashambulizi hayo, vifo vya Wapalestina waliopoteza maisha vinazidi kuongezeka ambapo hadi sasa zaidi ya Wapalestina 700 wamefariki dunia na 3,000 wamejeruhiwa tangu Israel ilipoivamia Gaza.
Rais Kikwete aliwaeleza mabalozi hao kuwa serikali yake inapinga matumizi ya kijeshi katika mgogoro wa Palestina na Israel, kwani njia hiyo si suluhisho la vurugu bali ni kichocheo cha machafuko.
Alisema Tanzania imekata rufaa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na wanachama wa Quartet kwa ajili ya kupinga mauaji ya Gaza, ambayo yanaendelea kushamiri kwa kasi na kuomba mashirika ya kimataifa kujitokeza kupinga mauaji hayo.
Swali:
Kwanini JK hakumtafuta mwakilishi wa Hamas ili kumpatia ushauri wa kusitisha makombora? kama alivyomuita Balozi wa Israeli na kuitaka nchi yake isitishe vita huko Gaza? Kwanini hajawaita Morgan na Mugabe; au Bashir na viongozi wa Janjaweed na wengine kule Darfur? Vipi kuhusu viongozi wa Somalia? Vita ni vita, na vifo vya raia vyote vinauma!