PDA

View Full Version : Quemu ndani ya kijiji

Quemu
01-10-2009, 07:15 PM
Jamani naombeni mnikatie angalau robo heka katika shamba hili la kijiji.

mwanakijiji
01-10-2009, 07:49 PM
Jamani naombeni mnikatie angalau robo heka katika shamba hili la kijiji.

quemu.. karibu.. wewe njoo na jembe lako tu.. ukikuta kuna mahali kuna msitu.. safisha anza kujilimia, kijiji kikubwa hiki

karibu !!!!

My more
01-10-2009, 10:38 PM
Jamani naombeni mnikatie angalau robo heka katika shamba hili la kijiji.

Una familia? robo itakutosha? Karibu sana Quemu.

Kaswali kadogo (eti Quem vipi una undugu wowote na akina Qute na cute??)

duru langu
01-11-2009, 08:57 PM
Karibu kijijini Quem

Ach-F
01-12-2009, 12:54 AM
Sasa hapa kijijini kila uchwao tunapata wageni lakini wengine michango yao wanabania Oooops fweza za Cafe siku hizi ni tabu si unajua kuna Crunch iliyoanzia Northern Rock ooops ilianza kwenye sub-prime morgages kule USA. Leteni sasa hayo mazingaombwe yanayochezwa na mafisadi. Mie naona mwanakijij bora aweke zawadi ya michango bora kutoka Bongo maana Cafe zinakomba bila kurudisha gharama bora tutoe tuzo kwa wachangiaji wetu wafaidike na kupunguza makali ya CRUNCH.

Quemu
01-13-2009, 08:57 PM
Una familia? robo itakutosha? Karibu sana Quemu.

Kaswali kadogo (eti Quem vipi una undugu wowote na akina Qute na cute??)

Aisee nina familia kubwa kweli. mke, watoto , pamoja na watoto wa dada na kaka yangu.

Kusema ukweli robo haitoshi. Lakini sikuwa najua utaratibu wa ugawaji wa ardhi katika kijiji hiki. Kwa hiyo nikaona bora kuomba kidogo, halafu ukapewa kikubwa. Kuliko kuomba kikubwa, halafu ukaishia kupata kiduchu.

Nafikiri majina yamegongana tu. Kama Qute na Cute nao ni wanakijiji hapa, basi bila ya shaka tutatunga undugu.

Quemu
01-13-2009, 09:00 PM
Sasa hapa kijijini kila uchwao tunapata wageni lakini wengine michango yao wanabania Oooops fweza za Cafe siku hizi ni tabu si unajua kuna Crunch iliyoanzia Northern Rock ooops ilianza kwenye sub-prime morgages kule USA. Leteni sasa hayo mazingaombwe yanayochezwa na mafisadi. Mie naona mwanakijij bora aweke zawadi ya michango bora kutoka Bongo maana Cafe zinakomba bila kurudisha gharama bora tutoe tuzo kwa wachangiaji wetu wafaidike na kupunguza makali ya CRUNCH.

Unajua ukihamia makazi mapya, inabidi utumie muda kidogo kusoma utaratibu wa maisha baina ya majirani kwa ujumla. Kwa hiyo, michango itamiminika tu. Tafadhali tupe muda to-warm up na hali ya hewa ya kijijini hapa kwanza.

My more
01-15-2009, 01:46 AM
Unajua ukihamia makazi mapya, inabidi utumie muda kidogo kusoma utaratibu wa maisha baina ya majirani kwa ujumla. Kwa hiyo, michango itamiminika tu. Tafadhali tupe muda to-warm up na hali ya hewa ya kijijini hapa kwanza.

Muhimu kabisa Quemu umesomeka vizuri. Karibu kwa warm up, ukishajisikia joto unaweza kuendelea tu na shughuli siku na muda wowote.

Karibu sana na familia yako yote. Naona mwenzetu umeneemeka