PDA

View Full Version : Majina ya JF...

Steve Dii
01-11-2009, 02:41 AM
Habarini...

Pamoja na kwamba hapa members wanajiandikisha upya, mimi nadhani itakuwa vyema tuwe makini na majina ya members ambayo yanagongana na yale ya kwenye JamiiForums.

Mimi hapa nimeamua kutumia jina lilelile nitumialo huko, lakini kwa vile kumbi za kule zina mambo yake, yaani mapatano na mifarakano; basi, yawezekana kabisa mtu kuja hapa na kujiandikisha kwa jina la mbaya wake au la jina la member fulani hivi wa kule ili kuwa gear yake ya kuweza kuwaingia kiundani wale ambao hapatani nao kule.

Naandika haya kama tahadhari tu ndugu zangu, tungependa mambo yote yawe mswano bila mifarakano wala kuwepo kwa mamluki, lakini kwa vile tuko mtandaoni, mema na mabaya yote yawezekana. Basi tujihadhari tu. Akhsanteni.

SteveD.

Ach-F
01-11-2009, 11:17 AM
Nilikuwa sifahamu kama JF ina majina. Is it true JF ina majina?

duru langu
01-11-2009, 08:39 PM
Ukikuta jina lako linatumiwa na mtu mwengina
si unaingia na jina lingine kisha unaeleza kwamba
mtumiaji wa jina **** sio sawa na mtumiaji wa jina
hilohilo **** ambaye yuko JF :cool:

Steve Dii
01-11-2009, 10:24 PM
Nilikuwa sifahamu kama JF ina majina. Is it true JF ina majina?

Okay, for the sake of the argument tuseme JF haina majina. But i believe you know what i dd imply by saying 'majina ya jf'

Ukikuta jina lako linatumiwa na mtu mwengina
si unaingia na jina lingine kisha unaeleza kwamba
mtumiaji wa jina **** sio sawa na mtumiaji wa jina
hilohilo **** ambaye yuko JF :cool:

Duru, Na hiyo ndiyo moja ya tahadhari niliyokusudia kuinyonyesha... Leo hii MwK akijja hapa akakuta Nyama hatari wa JF amejiandikisha kama Nyani, you know what he might do with that name...

I have got good examples za nuisances zinazoweza kusababishwa na majina kugongana, iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi...however trivial this matter seems to be at face value.

Anyway, I don't see the need to go into details trying to support my conjecture. Let's say it is a mere opinion i thought i should've brought it forth in order to find handy ways of dealing with should something like that happen.. Thanx.

Ach-F
01-12-2009, 12:46 AM
SteveD

Usitie shaka hayo ni mazungumzo baada ya habari. Si unajua tena leo kumetokea msiba kule Old Trafford, na tetesi zinasema kwamba Scolari inabidi arudishwe Brazil maana pesa za rubo haziwezi.

mwanakijiji
01-12-2009, 01:50 AM
Unajua watu hawazingatii tu sheria zetu za hapa. Kwenye mojawapo ya sheria tulitoa tahadhari watu kutokutumia majina wanayotumia kwenye forums nyingine lengo likiwa ni kuondokana na uwezekano kama huo.

Lakini hata hivyo ni vigumu kumzuia mtu kujiita anavyotaka kwani haya majina ya kwenye mitandao mingine hatuna hati miliki nayo.

So nadhani ni upanga wenye pande mbili!

ponda
01-13-2009, 04:28 PM
hivi na hapa mna mtindo wa kufuta posting ya mtu hasa ikimsema jamaa fulani kama kule?

mwanakijiji
01-13-2009, 05:38 PM
hivi na hapa mna mtindo wa kufuta posting ya mtu hasa ikimsema jamaa fulani kama kule?

inategema unasema kitu gani; mambo ya kibinafsi ambayo hayana msingi au kuhusiana na utendaji kazi wa mtu au fedha za walipa kodi tunayapeleka kwenye ukumbi wa "Uswahilini". Vinginevyo tunabakia kuwa kumbi huru zaidi kuliko nyingine yoyote.

911
01-18-2009, 09:27 AM
Habarini...

Pamoja na kwamba hapa members wanajiandikisha upya, mimi nadhani itakuwa vyema tuwe makini na majina ya members ambayo yanagongana na yale ya kwenye JamiiForums.

Mimi hapa nimeamua kutumia jina lilelile nitumialo huko, lakini kwa vile kumbi za kule zina mambo yake, yaani mapatano na mifarakano; basi, yawezekana kabisa mtu kuja hapa na kujiandikisha kwa jina la mbaya wake au la jina la member fulani hivi wa kule ili kuwa gear yake ya kuweza kuwaingia kiundani wale ambao hapatani nao kule.

Naandika haya kama tahadhari tu ndugu zangu, tungependa mambo yote yawe mswano bila mifarakano wala kuwepo kwa mamluki, lakini kwa vile tuko mtandaoni, mema na mabaya yote yawezekana. Basi tujihadhari tu. Akhsanteni.

SteveD.

Mkuu SteveD,you are worrying too much!!Mi nadhani/nafahamu kuwa katika forums kinachoangaliwa zaidi ni hoja na sio id/mtoa hoja.Nikiwa na maana kuwa mimi na wewe tunaweza kuafikiana/kupatana katika hoja flani lakini tukaja kuwa na mitazamo tofauti katika hoja nyingine.Hiyo haitamaanisha kuwa tunajenga chuki/uhasama but we are shaping our minds!Sioni tatizo la member kuregister kwa id yeyote ile,kikubwa cha kuangaliwa ni mchango wake jamvini.Hii ya kuangalia ni nani kasema ndio inayosababisha baadhi ya member kudoubt their perceptions,supres their resevations also withhold their opinions simply because naweza nikadisturb uswahiba wangu na fulani.Tunapokubaliana/cheka pamoja tuwapo NYUMBANI haimaanishi kuwa hata tutakapokuwa OFISINI hali itakuwa hivyo hivyo,mjenga hoja aipe mashiko ili ikubalike!

Mpita Njia
01-20-2009, 05:37 PM
Unajua watu hawazingatii tu sheria zetu za hapa. Kwenye mojawapo ya sheria tulitoa tahadhari watu kutokutumia majina wanayotumia kwenye forums nyingine lengo likiwa ni kuondokana na uwezekano kama huo.

Lakini hata hivyo ni vigumu kumzuia mtu kujiita anavyotaka kwani haya majina ya kwenye mitandao mingine hatuna hati miliki nayo.

So nadhani ni upanga wenye pande mbili!

Ahaaaa!!!! KUmbe wengine tulikosea?!? lol
Mkuu ulitupotosha, tulipoona jina lako linafafa sana na lile la kule, tukaona ni ruksa na sisi ku-maintain majina yetu.
Anyway, nadhani jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa suala la majina kujichanganya linashughulikiwa kwa namna ambayo haitasababisha kuanzisha malumbano yasiyo na msingi. Na kwa kuwa mpaka sasa hivi kauna tatizo lililojitokeza hadharani kuhusiana na majina, nadhani ni mwanzo nzuri na tuombe lisijitokeze

ponda
01-21-2009, 11:43 AM

Point taken,