PDA

View Full Version : ufisadi mwingine unakuja,machinga complex

dude
01-11-2009, 10:15 PM
habari nilizozipata kutoka jikoni ni kwamba kuna ufisadi wa kutisha unakuja,lile jengo la machinga complex linategema kuwa na vyumba elfu 10,kila chumba mpangajia atatakiwa kulipia kwa mwezi sh elfu sabini,kwa machinga wa kawaida hakuna atakaeweza kupanga kwenye hilo jengo kwahiyo sio la wamachinga tena kama tulivyoambiwa maana wamachinga wengi mitaji yao inaishia elfu 30.sasa kama mnavyojua vyumba kariakoo vimepanda bei ukitaka chumba kimoja cha biashara unatakiwa kulipia si chini ya laki mbili na nusu,sasa kuna wakubwa kwenye manispaa ya ilala wameapply kupata vyumba 100 kila mmoja kwenye hilo jengo na wametumia majina tofauti ili wasigundulike,sasa mmoja akipata vyumba 100 na yeye akakodisha kwa laki mbili na nusu kila chumba huku yeye analipia elfu sabini kwa mwezi huoni huu ni ufisadi wa hatari..naendelea na uchunguzi ili nipate majina yao kabisa ndipo niyaweke hadhalani ila hicho ndo kinachokuja kutokea.

mwanakijiji
01-12-2009, 05:06 PM

Dude, Watanzania kila wakati tunatafuta nafasi ya ulaji. Na katika kufanya hivyo mara nyingi watu hawajali nini sheria inasema, ahadi zinasema, au hata kusikiliza dhamira zao. Kwani wameshaanza kupangisha vyumba hivyo?

dude
01-12-2009, 08:09 PM
kaka vyumba bado havijaanza kutolewa,saizi ni mda wa wafanyabiashara kuapply...

a2faces
01-26-2009, 03:42 PM
.......Inawezekana, kwa maana kuna watu wengine wameshaanza kupita mitaani wakidai kuwa wana - connection kwa ajili ya kupata vyumba vya biashara hapo machinga complex, unawapa pesa na picha zako then wanakupa form unajaza na wanakupa risiti na kitambulisho,jamani ufisadi huu.........nikipata mtu aliyekwisha lipa nitatuma ushahidi!!!

mfumwa
01-26-2009, 06:08 PM
kaka vyumba bado havijaanza kutolewa,saizi ni mda wa wafanyabiashara kuapply...

Hapo katika kuapply ndio ubabaishaji mkubwa, kabla ya hili zoezi lazima walitakiwa kuwa tayari wana majina ya machinga walioondolewa maeneo ya katikati ya jiji (posta, kariakoo nk), ndio wapewe. Sasa kama ni kuapply utajuaje huyu ni machninga ama la. Hili TZ ni suala la kawaida, fuatilia watu waliohamishwa masoko mapya kutoka yale ya zamani. Utakuta kule wanakohamishiwa tayari nafasi wamepewa wale hata sokoni walikuwa hawaonekani.

Kuna tatizo gani kama unataka kulifunga soko na kulihamisha, kujua idadi ya waliokuwepo katika soko la zamani, manake walikuwa wanalipa kodi na idadi yao inajulikana. Baada ya hiyo idadi unafanya sensa na wale wanaouza bidhaa zao kuzunguka soko na kuwaorodhesha majina. Soko jipya likifunguliwa unajua kabisa kwa kiasi fulani una majina halisi, japo udanganyifu huwezi kuutoa kabisa.