PDA

View Full Version : Kikwete awashtukia mafisadi!



mwanakijiji
01-12-2009, 09:53 AM
Baada ya kuandika makala kadhaa ambazo tulionesha "CCM na Urafiki wenye mashaka" (Angalia matoleo ya Cheche yaliyopita), Rais Kikwete inaonekana ameanza kuwashtukia watu wanaotaka kutumia majukwaa ya CCM ili wapige picha na Rais na hivyo kujijengea mazingira yakusasifha. Habari ifuatayo ni kielelezo.

JK akwepa kumtunuku cheti mtuhumiwa EPA

2009-01-11 15:59:33
Na Novatus Makunga, Arusha

Rais Jakaya Kikwete jana alikwepa kumtunuku mmoja wa watuhumiwa wa kesi za wizi wa fedha katika akaunti ya madeni ya nje(EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania(BoT), wakati akitakiwa kugawa pikipiki kwa makatibu wa Chama cha Mapinduzi wilayani hapa.

Rais alikwepa kugawa pikipiki hizo zenye thamani ya sh.milioni 24.5 baada ya kubaini uchangiaji huo ulijumuisha mfadhili ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa mafuta, Japhet Lema maarufu kama Njake, anayetuhumiwa katika wizi wa fedha EPA.

Mfanyabiashara huyo alihudhuria hafla hiyo ili naye atunukiwe cheti cha shukrani.

Pikipiki hizo ambazo zimekaa kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa katika ofisi ya CCM wilayani Arusha zikitafuta \'mzito\' wa kuja kuzigawa, zilikuwa zikabidhiwe sanjari na vyeti vya shukrani kwa waliozitoa,katika shughuli iliyoandaliwa na chama hicho wilaya.

Kwa mujibu wa habari za ndani ya chama hicho, waliochangia pikipiki hizo kumi na tisa ni pamoja na mbunge wa Arusha Felix Mrema na mwenyekiti wa CCM wilayani Arusha Jubilate Kileo.

Rais Kikwete pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, aliwasili katika uwanja wa CCM wilayani hapa majira ya saa kumi jioni na baada ya kukaribishwa kuzungumza, ikitegemewa baadaye ndipo ataanza kazi ya kugawa pikipiki hizo, akasema kamwe hataweza kufanya hivyo bali atawaachia viongozi wa wilaya wajigawie wenyewe.

``Nimeziona lakini sitaweza kugawa moja baada ya nyingine, mimi sijui mlikozipata, lakini wenyewe mnajua mtakaa mtagawana wenyewe,``alisema.

Hata hivyo, Rais Kikwete aliwaonya kutotafuta raslimali ambazo zitawaletea matatizo hapo baadaye na kuwataka wazidishe mshikamano na umoja kama nguzu muhimu ya mafanikio.

Aliwataka wakamilishe maandalizi ya chaguzi za serikali za mitaa ili waweze kupata ushindi mzuri na pia aliwatakia kila la heri katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata ya kati unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu. kwani ni vizuri kuwa na vitendea kazi wakati tunaelekea katika uchaguzi,``alieleza Rais Kikwete katika hutuba yake ambayo haikuzidi dakika tano.

Hata hivyo, pamoja na Rais Kikwete kuachia jukumu hilo kwa uongozi wa wilaya, mpaka viongozi wa ngazi mbalimbali wanaondoka, pikipiki hizo zilikuwa hazijagawanywa katika kile kilichoonekana kila mmoja kukwepa kufanya shughuli hiyo na kumrushia mpira mwenzake.

Mara baada ya Rais Kikwete kuondoka, Mwenyekiti wa CCM wilaya Bw.Kileo alikuwa wa kwanza kuongea na kueleza kwamba shughuli ya ugawaji itafanywa na katibu wa wilaya, lakini baadaye katibu wa wilaya naye alieleza shughuli hiyo itafanywa na katibu wa uenezi na siasa.

Jitihada za kumpata Katibu wa CCM wa wilaya ya Arusha, Bw.Mohammed Nyawenga ambaye aliondoka na Rais Kikwete kwenda uwanja wa ndege hazikufanikiwa kwani simu yake ilikuwa inaita bila ya kupokelewa.

Katibu wa uenezi na siasa wa wilaya hiyo, Bw.Semmy Kiondo alieleza kuwa anachofahamu watu ambao wangekabidhiwa vyeti vya shukrani ni Mrema na Kileo na alipoulizwa kwanini Lema alihudhuria shughuli hiyo alijibu kuwa alikuja kama wanachama wengine.

Dua
01-13-2009, 12:56 AM
Tunangoja tu na I can bet you this is the president ambaye atashitakiwa Tanzania mara akiondoka madarakani. Time will tell. Nyie mwacheni awaonee huruma rafiki zake lakini atakapokwenda jela ndio atajua kilichomtoa kanga manyoya.